SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Jeshi la Israel muda huu limetoa wito walio eneo la kalashan Ikuhama haraka
20250620_002515.jpg
 
Hii ndio maana halisi ya kutawala anga yaani ndege zinaruka juu ya mji mkuu zinapita kwa dharau hivyo huku kiongozi yuko shimoni
Subirini mpaka kesho muone Wairan watajibuje mapigano haya kwa njia missiles na Drones - Iran si Hazibollaa ah Hamasi hapa Israel imejiingiza kwenye choo cha KIKE na kujinasua hawezi - too late,labda mjomba wao (Merikani) iwanasue nasikia Trump amekwisha mpigia simu Ayatollah ili wamalize vita hii kwa njia us Kidiplomasia!!!
 
IRAN News: jeshi la Iran limetoa wito muda huu kuwa walio karibu na nuclear site ya dimona huko Israel wanapaswa kuhama haraka

View: https://x.com/IranNewsX/status/1935814444413546684?t=OYkYqUlgY9X4zucx9suVOg&s=19

Na mimi nilijua tu kwamba nuclear power reactor hiyo italengwa na makombora ya Iran tu eventually, halafu hipo tu exposed kwenye jangwa LA Negev, hawa jamaa watakuja kutuletea balaa nawambieni, halafu wanajuaje kama Iran hawana bomb la thermonuclear mpaka sasa? Najua Waisrael wanayo,ndio maana hawataki mataifa mengine ya mashariki ya kati wawe nayo,anataka atambe tu yeye.
 
Iran na yeye anaharibu kila mara kutoa taarifa, vita kipindi inaanza Israel alishtukiza, hio nuclear reactor ya Dimona Iran haipaswi kutoa angalizo, waweke vyuma tu... Iran nao wanazingua wakati mwingine... wanatoa taarifa kila muda adui anajipanga..
 
Tatizo kubwa ni Uyahudi (Judaism) na Uzayuni (zionism) ambazo ni dhana mbili zinazohusiana lakini zinamaanisha mambo tofauti katika muktadha wa historia, dini, na siasa—hasa kuhusiana na Wayahudi na ardhi ya Israeli.

Uyahudi (Judaism/Uyahudi)

Uyahudi ni dini ya kale ya Kiyahudi na pia ni utambulisho wa kitamaduni na kabila

Vipengele Muhimu:
uyahudi
  • Dini: Imani ya Mungu mmoja (Yahweh), maandiko matakatifu ya Tanakh (ikiwa ni pamoja na Torati).
  • Historia: Wayahudi waliishi katika nchi ya kale ya Israeli na Yuda, lakini walitawanywa (Diaspora) baada ya utekaji na Warumi mwaka 70 BK.
  • Maadili: Sharia (Torati), ibada katika Sinagogi, na mapokeo kama Sabato, Pasaka ya Kiyahudi (Pesach), n.k.
  • Utambulisho: Mtu anaweza kuwa Myahudi kwa kuzaliwa katika familia ya Kiyahudi au kwa kujiunga (ugeuzi).
Uzayuni (Zionism/Uzayuni)

Uzayuni ni harakati ya kisiasa na ya kitaifa iliyoanza karne ya 19, iliyolenga kuunda na kuunga mkono taifa la Wayahudi katika ardhi ya Israeli (ambayo kihistoria ilikuwa Zion).
Vipengele Muhimu:
  • Zion ni jina la Biblia linalotaja mlima Yerusalemu, kisha likawa ishara ya mji na taifa la Kiyahudi.
  • Mwanzilishi wa kisasa: Theodor Herzl (1896) kupitia kitabu chake Der Judenstaat (“Taifa la Wayahudi”).
  • Lengo kuu: Kuwarudisha Wayahudi kutoka uhamishoni ili waishi kwa uhuru na usalama katika nchi yao ya asili.
  • Matokeo:
    • Uanzishaji wa taifa la Israeli mwaka 1948.
    • Mvutano na Waarabu wa Palestina na nchi jirani.
    • Tawi la dini la Uzayuni (Religious Zionism) linasisitiza kurudi kwa ardhi takatifu ya Biblia.
  • Sio Wayahudi wote ni Wazayuni: Baadhi ya Wayahudi wa kidini wanapinga Uzayuni wakiamini kuwa ni Mungu pekee anayeweza kurejesha taifa la Israeli kwa njia ya kiroho, si ya kisiasa.
  • Sio Wazayuni wote ni Wayahudi: Kuna Wakristo Wazayuni na watu wengine wanaounga mkono Israeli kwa sababu za kisiasa, kijeshi, au za imani.
Uyahudi ni imani ya kidini na utambulisho wa kitamaduni unaotangulia Uzayuni kwa maelfu ya miaka.

Uzayuni ni harakati ya kisasa ya kisiasa iliyochochea kurudi kwa Wayahudi katika ardhi ya Israeli, na kuanzishwa kwa taifa la Israeli.
Umetisha sana mkuu
 
Back
Top Bottom