Sidhani kama Pakistan watakubali hili..
US akiweka hapo kambi ndio NATO, EU, Israel na nchi zingine hasimu wa Iran watapeleka askari wa miguu kuingia Iran.. ipo wazi anga pekee haitoshi kuangusha utawala wa Ayatollah..
Tukumbuke pia Trump anapita kule kule alipopita Bush kwa kusema Iraq wana WMD, hii ni cheap propaganda ambayo imepitwa na wakati ili kuhalalisha nchi mbali mbali kuivamia Iran...
Tukumbuke kwamba wakati ule late 1990s na early 2000s , US walikuwa na ushawishi mkubwa sana duniani kote, nchi zilizoivamia Iraq ni zaidi ya 40...
Leo hii watu wameutambua ukweli, support anayopewa Trump ni ndogo...
Na naelewa katika namna ya kumtongoza Asim Munir Chief of Army Staff of Pakistan huko Washington walipokuwa na kikao, itakua amemueleza Iran ni hatari kwenu pia ikiwa na nuclear... itakuwa kamuambia Iran ni hatari mashariki ya kati leo kwa Israel kesho ni kwenu...
Lakini sidhani kama Pakistan itanunua huo utopolo..