SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Sema Israel wanaikuza hii kesi ili either American aingilie kati au wapate sababu ya kumuua Khamenei au shambulio lolote baya dhidi ya Iran b'se me sijaona effect iliyopelekewa na bomu la leo kupita yale ya siku 2 za kwanza
Effect zipo ila wanaficha taarifa
 
Sina cha kukudai we babu mwenye miaka yake 80 na usheee hata wakikuua leo

Wale wahuni wa pale gaza walituonyesha tobo la udhaifu wao ndio maana mpaka leo bado zinachapika ila wew umekuja kumaliza kabisaaa kila kitu kwa kuwaweka uchi ili dunia nzima ijue zile maneno za kuwasifia sana kumbe ni propaganda tu.....weupe sana wale
 
Tatizo kubwa ni Uyahudi (Judaism) na Uzayuni (zionism) ambazo ni dhana mbili zinazohusiana lakini zinamaanisha mambo tofauti katika muktadha wa historia, dini, na siasa—hasa kuhusiana na Wayahudi na ardhi ya Israeli.

Uyahudi (Judaism/Uyahudi)

Uyahudi ni dini ya kale ya Kiyahudi na pia ni utambulisho wa kitamaduni na kabila

Vipengele Muhimu:
uyahudi
  • Dini: Imani ya Mungu mmoja (Yahweh), maandiko matakatifu ya Tanakh (ikiwa ni pamoja na Torati).
  • Historia: Wayahudi waliishi katika nchi ya kale ya Israeli na Yuda, lakini walitawanywa (Diaspora) baada ya utekaji na Warumi mwaka 70 BK.
  • Maadili: Sharia (Torati), ibada katika Sinagogi, na mapokeo kama Sabato, Pasaka ya Kiyahudi (Pesach), n.k.
  • Utambulisho: Mtu anaweza kuwa Myahudi kwa kuzaliwa katika familia ya Kiyahudi au kwa kujiunga (ugeuzi).
Uzayuni (Zionism/Uzayuni)

Uzayuni ni harakati ya kisiasa na ya kitaifa iliyoanza karne ya 19, iliyolenga kuunda na kuunga mkono taifa la Wayahudi katika ardhi ya Israeli (ambayo kihistoria ilikuwa Zion).
Vipengele Muhimu:
  • Zion ni jina la Biblia linalotaja mlima Yerusalemu, kisha likawa ishara ya mji na taifa la Kiyahudi.
  • Mwanzilishi wa kisasa: Theodor Herzl (1896) kupitia kitabu chake Der Judenstaat (“Taifa la Wayahudi”).
  • Lengo kuu: Kuwarudisha Wayahudi kutoka uhamishoni ili waishi kwa uhuru na usalama katika nchi yao ya asili.
  • Matokeo:
    • Uanzishaji wa taifa la Israeli mwaka 1948.
    • Mvutano na Waarabu wa Palestina na nchi jirani.
    • Tawi la dini la Uzayuni (Religious Zionism) linasisitiza kurudi kwa ardhi takatifu ya Biblia.
  • Sio Wayahudi wote ni Wazayuni: Baadhi ya Wayahudi wa kidini wanapinga Uzayuni wakiamini kuwa ni Mungu pekee anayeweza kurejesha taifa la Israeli kwa njia ya kiroho, si ya kisiasa.
  • Sio Wazayuni wote ni Wayahudi: Kuna Wakristo Wazayuni na watu wengine wanaounga mkono Israeli kwa sababu za kisiasa, kijeshi, au za imani.
Uyahudi ni imani ya kidini na utambulisho wa kitamaduni unaotangulia Uzayuni kwa maelfu ya miaka.

Uzayuni ni harakati ya kisasa ya kisiasa iliyochochea kurudi kwa Wayahudi katika ardhi ya Israeli, na kuanzishwa kwa taifa la Israeli.
 
20250619_203953.jpg


White House spokeswoman on behalf of Trump:

"I will decide on an attack on Iran within two weeks based on the results of the negotiations"
 
Israel inacho kifanya kwa watu wa gaza ni unyama na uovu ambao hata shetani anaushangaa na kila binadamu mwenye akili timamu anatakiwa kuyapinga.
Sema hamas naye siaachie wake mateka mambo yaishe, inshort atawaua wote maana si unajua west hawana na kumfanya ni lastborn wao
 
Hivi wadau hili suala la US kuiomba PAkistan iweke kambi ya jeshi kwa kuwapa makombora ya kisasa, jet fighter za kisasa F-35 na msaada wa kijeshi na pesa, hivi hili India inalichukuliaje? mbona kama US anaisaliti India?

Kwa kuipa vifaa kama hivyo Pakistan kisa tu wapate access kuishambulia Iran ina maana US imeamua kuitoa kafara India kisa tu kuimaliza Iran? maana Pakistan wakipata hivyo vyombo India ipo matatani.. India si ni rafiki wa Israel? hi imekaaje?

Hapa nimeamini Iran inaogopeka
India = Israel.
 
Back
Top Bottom