SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Yaleyale yaSahaff wa iraq ya saddam Hussein
 
Jamaa ni Snitch sana.
 
Huyu dada si ndiye yule Israel ilishambulia kituo chake cha habari akiwa live?
Wenzangu na mm hii ni kwa Kiswahili ujumbe wa Jenerali Mwandamizi wa IRGC na mwanasiasa, Mohsen Rezaei:

"Tayari tumewaadhibu Waisraeli kwa ukali, lakini bado haitoshi. Lazima adhabu yetu iwe kama bima ya usalama kwa baadaye, ili adui asithubutu kurudia tena vitendo hivi.

Adui alikusudia kuleta vurugu nchini kwa kuwaua makamanda wa jeshi, lakini jaribio hilo lilishindikana ndani ya saa 48 za kwanza. Hatua iliyofuata, walitaka kuigeuza Iran kuwa kama Syria na kuisababishia hali ya vurugu kwa miaka 10, lakini leo hii, Israel yenyewe imekuwa kama Syria.

Katika saa 48 zilizopita, tumetumia mbinu mpya: mchanganyiko wa makombora ya Fattah na Sejjil, yakiwa pamoja yanavuruga sana mifumo ya ulinzi ya adui.

Mapatano yoyote ya kusitisha vita kwa sasa yatapelekea vita kuanza upya. Hatupaswi kumpa nafasi adui, ambaye sasa yuko katika hali dhaifu, ajipange tena kupitia kusitisha mapigano.

Hadi sasa tumetumia chini ya 30% ya uwezo wetu wa kijeshi. Tunaongeza mashambulizi taratibu ili watu waondoke kwenye maeneo ya hatari.

Vifaa vyote vilivyoboreshwa (nuclear materials) vimeshahamishiwa sehemu salama.


Netanyahu ameambia Marekani: "Nisaidie au uitishe kusitisha vita."

Hata kama Marekani itaingia vitani na kufanikisha kuharibu kituo cha nyuklia cha Fordow, bado haiwezi kuifanya Israel kuwa na ulinzi mkubwa zaidi ya ilivyo sasa.

Israel ilishambulia maeneo kama Natanz, kituo cha nyuklia Isfahan, Khandab, na Arak, lakini vituo hivyo vilikuwa tayari vimehamishwa. Vitu vyote walivyolenga kuviharibu vilikuwa vimehamishiwa sehemu salama. Wataalamu wetu wa nyuklia na vifaa muhimu bado vipo. Kwa hiyo, mashambulizi hayo hayakufanikisha chochote kikubwa.

Wananchi wa Iran hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu mwisho wa vita hivi. Israel lazima iadhibiwe kiasi cha kuogopa kabisa kujaribu kuleta vurugu tena nchini mwetu miaka ijayo.

Tangu Februari-Machi, tulielewa wazi kupitia uchambuzi wetu kwamba vita vitatokea. Baada ya hapo, tukaongeza mara 5 uwezo wetu wa makombora na teknolojia ya mtandao (cyber).

Mpaka sasa hatujatumia uwezo wetu wa nchi kavu, baharini, mafuta, wala Mlango wa Hormuz. Hatujatumia pia washirika wetu wa kimataifa. Ingawa washirika wetu wameomba kuingia vitani, tumeamua bado si wakati.

Tumeendelea kutangaza kwa wakazi wa maeneo yaliyovamiwa (occupied territories) waondoke karibu na maeneo ya serikali, jeshi na ujasusi. Hatutaki kuwapiga watu wa kawaida. Moja ya sababu ya kuongezeka kwa mashambulizi ya makombora ni kuwapa watu muda wa kuhama.

Hawawezi kujenga kituo cha kijeshi karibu na hospitali, alafu watushambulie kutoka pale, kisha kutarajia tusijibu.
 
Russia waliomba watoe msaada Iran ikasema haijafikia hatua ya kuomba msaada, hayo amesema chief of staff wa Iran na Putin kasema, na ingetokea Russia kutoa msaada media za west zingesema, ndege zingeonekana kwenda Iran...
Russia ya kwake yamemshinda huko na Ukraine ndio atie msaada thubutu
 
Haki hii ni balaa, Hii ni Telaviv na Haifa kweli?

Makombora ya Iran yameleta uharibifu mkubwa sana

My take: Wanaoumia na hii vita ni raia wa kawaida kati ya mataifa hayo mawili
Hivi inamaana nchi nyingine zimeshindwa kabisa kuwaambia hawa watu waache kupigana??


View: https://x.com/WarMonitors/status/1935657429225669023?s=19
Your browser is not able to display this video.
 
Israel kajiandaa kaanzisha vita kwa kushtukiza na bado anapata tabu aisee angekua anawaza vizuri angewapotezea hao waajemi maana sio watu kabisa..
Mkuu Israel anapata tabu kivipi? yaani unataka asipigwe hata kidogo? ulitaka apige yeye asiguswe?
Mimi naona Israel bado anaenda vizuri tu na sasa anaingia Iran muda na saa anayotaka, ndani ya week 2 hizi tutaongea mengine kwani Iran kashatepeta.
 
Mbona Iran siskii zaidi ya kushambuliwa maeneo yake mahususi ya Nuclear program au Iran inaficha taarifa za uharibifu unatokea nchini kwake ?
 
Israel inazuia waandishi wa habari kuchapisha habari zinazoonyesha madhara waliyopata kutokana na mashambulio ya Iran, ni ishara kuwa Israel imeathirika sehemu kubwa kiasi cha kuona aibu, na tutegemee kupokea taarifa zisizo za kweli kutokana na kuminywa uhuru wa wanahabari.
==

Serikali ya Israel imetoa maelekezo mapya yanayoweka masharti kuhusu namna vyombo vya habari vya ndani vinavyoripoti vita inayoendelea dhidi ya Iran.

Waraka uliotolewa na mkaguzi wa kijeshi wa Israel, Brigedia Jenerali Kobi Mandelblit, umetangaza sheria mpya kuhusu kile ambacho mashirika ya habari ya Israel na waandishi wa habari wa ndani ya nchi hiyo wanaruhusiwa na hawaruhusiwi kuchapisha kuhusu athari za mashambulizi kutoka Iran.

Sasa, ni vizuizi vipya gani ambavyo waandishi wa habari wanakabiliwa navyo, na je, uhuru wa vyombo vya habari nchini Israel unasimama vipi ukilinganisha na mataifa mengine?


View: https://www.instagram.com/p/DLHGVLjtFdh/?igsh=dXR6N2lqbG1ib21w
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…