SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Yaleyale, hakuna hiko kitu
Wewe ndugu shusha update achana na hao kobazi na ndugu zao wagalatia

Mda huu wote wamejificha wanasubili bomu likianguka Tell Aviv ndo wanakuja humu kama nyuki na takbir kibao
Kwa ubishi hao huwawezi maana kwao kubishana ni thwawabu

Yote kwa yote tunakushukuru sana maana huna unapnde na unaleta habari za pande zote
 
Mfano kinu cha Natanz kilisadikiwa kuwa na Uranium inayo tosha kutengeneza mabomu kumi haiwezekani mitambo inayo rutubisha madini mengi namna hiyo ishambuliwe alafu mionzi isijuve.
Baada ya shambulizi Iran ilidai kuwa ilikuwa imehamisha vifaa vyote muhimu kutoka natanzi na Isfahan.
Hata Putin juzi kipindi anaongea na waandishi ya habari alisema kuwa mitambo ya kurutubisha Uranium inaendeleq kama kawaida na Israel hawataweza kufikia lengo lao.
Kumbuka ujujaji wa mionzi ulisha wahi kusababisha janga nchini Japan na kuuwa watu elfu 22 mwaka 2011 hivyo usichukilie poa.

View: https://www.youtube.com/shorts/uSMQfKjwQ2s?feature=share
 
Attachments

  • Screenshot_2025-06-21-12-52-13-563.jpg
    Screenshot_2025-06-21-12-52-13-563.jpg
    301 KB · Views: 19
Ukisoma vizuri historia utafahamu kwamba mataifa ya Magharibi yamekuwa yana kiwewe (Obsession) na madola ya Uajemi tokea kipindi cha kale. Amini nakwambia hata kina Ayatollah na dola la kiislamu wakipinduliwa na Iran likawa dola la Kikristo, Marekani, Israel na Uingereza hawawezi kuwaacha waajemi waishi maisha yao.

Madola yote ya kale makubwa, kuanzia Macedonia, Rome, Rashidun Caliphate, Mongol Empire, Holy Roman Empire, British Empire, Russian Empire na The Soviet Uniona yote yamewavamia waajemi kwa nyakati tofauti katika historia ya miaka 2000 iliyopita. Leo hii Marekani inafanya hivyohivyo. Chanzo kikubwa ni kwamba Iran ina utajiri mkubwa mno, lakini pia iko katikati ya barabara ya kimataifa inayounganisha Europe, Middle East, Central Asia na Far East.

Wagiriki walivyofanikiwa kuvamia Uajemi, walifanikiwa kufika hadi India na kutengeneza makoloni makubwa kama Greco-Bactria yaliyokuwa jirani kabisa na Uchina. Waislamu walipofanikiwa kutawala Iran (Sassanid Empire) ndiyo wakaleta ustaarabu mkubwa duniani kwa kuunganisha Ulaya na Asia. Leo hii Urusi, Israel na Marekani zinagombania njia ya Iran na Pakistan ambazo ni muhimu kwa biashara ya dunia na ulinzi.

Kumbukwa mwaka 1946, Joseph Stalin na Harry Truman waligombana mno kwasababu Urusi alikataa kutoka Iran baada ya vita vya pili vya dunia. Marekani alifahamu kabisa kwamba kama Urusi akikalia Iran ingekuwa basi tena kwasababu ni sehemu muhimu kimkakati. Leo hii, mbali na mengine, anayetafutwa Iran ni Uchina. Iran ikianguaka litakuwa ni pigo kubwa mno kwa Uchina, kiusalama, kibiashara na Kimkakati kutokana na umuhimu wake.

Mambo ni mengiiiii sana.
View attachment 3377610

NB: Hii njia ni moja ya sababu kubwa inayoweza kuondoa kabisa nguvu ya G7 kwenye biashara ya dunia, na kuzifanya Iran-Pakistan kuwa, THE NEW SUEZ/MALACCA CANALS. Jambo kama hili likitokea G7 itakuwa na hali mbaya.

Sababu ni nyingi mno, ila fahamu kwamba tatizo siyo Ayattolah wala Uislamu, tatizo ni lilelile la miaka yote: EXCESSIVE EMPIRIALISM.
​
Hivi ni kwanini West ipo obsessed na Rasilimali za Mataifa yenye nguvu kijeshi tu uku nchi kama Venezuela,Tanzania,Brazil ama Angola hawana shida nazo?.

Namely,wao wanataka Rasilimali za N/korea,Urusi ama Iran nchi tu,Nchi ambazo zina uwezo wa kuleta maafa makubwa kwenye Nchi zao uku wakizipa mgongo Nchi zenye rasilimali kama kama hizo hizo wanazozitaka.

Ni kama kibaka anaelenga kukaba watu waliojihami na silaha tu uku watu wasio na silaha kwake sio target.
"Ukiwa na Vito vya thaman na una Silaha kwake unakuwa easy target ila ukiwa na hivyo Vito na huna silaha kwake sio target".
ama ndiyo wanafuata Kamba isiyokatika pembamba?.
 
Picha hii wapo: Qassim Suleiman, Hossein Salami, Mohamed Baqeri na Saeed Izad. Qassim suleiman alouwawa miaka michache iliyopita, salami ameuwawa na Israel majuzi, na bakheri pia ameuwawa na Israel majuz. Leo alfajiri Israel wamefanikiwa pia kumuua Saed Izad (aliyezungushiwa duars nyekundu)

Pamoja na kuondokewa hasa viongozi wao wakubwa wa jeshi bado Iran imeonyesha resistance. Tusubiri
20250621_134420.jpg
 
Njia ya Uajemi ina mambo makuu mawili:

Mosi, inapunguza urefu wa safari kwa siku zisizopungua 15 tofauti na ile ya Suez Canal ambayo kwa meli hutumia siku 30 hadi 45, kutoka Asia hadi Ulaya. Hivyo kutoka Persian Gulf, hadi St.Petersburg itakuwa ni njia fupi zaidi kama watatumia The North-South Corridor.

Pili, North-South Corridor itakuwa nje ya makucha ya G7 na NATO. Jambo ambalo kiusalama na kiuchumi ni jema kwa mataifa mengi. Hivi leo hii unadhani, Marekani ikifunga Suez-Canal kuna mtu Ulaya au Asia atapiga kelele ??? AU leo hii ikitokea vita kati ya Marekani na Uchina, na Marekani akawaambia Singapore wafunge Malacca Strait, unadhani Uchina anayetegemea nishati kutoka Persian Gulf atatoboa kweli ???

Mambo ni mengi sana, japo hii njia siyo chanzo kikuu cha mgogoro. Sasabu zipo lukuki. Israel, Saudi-Arabia, Qatar nao wana mpango mkubwa wa kutengeneza njia mpya kukwepa Suez Canal, jambo ambalo litawapa nguvu kubwa mno kwenye biashara ya dunia dhidi ya UE.

View attachment 3377673
​

NB: Kinachoendelea saa hizi hakina utofauti na kile kilichokuwa kinafanyika karne za 18 na 19 kwenye kugombania ujenzi wa SUEZ CANAL na The Berlin Baghdad Railway ili kutawala biashara ya dunia

Mkuu huonekani kabisa

Tunaomba uchambuzi wa hii vita inavyoenda wewe unaona nani mpaka mda huu anaendelea kuwa mshindi na anajichukulia point tatu muhimu
 
Hana upande anaopendelea wakati kila shambulio la Iran hudai yote yamekua intercepted ilhali chini kunawaka,we sema anapost yanayokufurahisha
At least yeye anapost mashambulizi ya pande zote, je wewe umewahi kupost mashambulizi ya Israel kwa iran?
 
Hivi ni kwanini West ipo obsessed na Rasilimali za Mataifa yenye nguvu kijeshi tu uku nchi kama Venezuela,Tanzania,Brazil ama Angola hawana shida nazo?.

Namely,wao wanataka Rasilimali za N/korea,Urusi ama Iran nchi tu,Nchi ambazo zina uwezo wa kuleta maafa makubwa kwenye Nchi zao uku wakizipa mgongo Nchi zenye rasilimali kama kama hizo hizo wanazozitaka.

Ni kama kibaka anaelenga kukaba watu waliojihami na silaha tu uku watu wasio na silaha kwake sio target.
"Ukiwa na Vito vya thaman na una Silaha kwake unakuwa easy target ila ukiwa na hivyo Vito na huna silaha kwake sio target".
ama ndiyo wanafuata Kamba isiyokatika pembamba?.
Venezuela si unaona vurugu lake, mafuta ya angola na almasi wanavyo,savimbi walimtelekeza walipopewa dili,tanzania wanayo,barrick, acacia
 
Back
Top Bottom