SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Wanafahamu sana namna ya kumshawishi mtu, wakitaka kukutumia kitu cha kwanza ni kukupeleleza una ndoto gani na kitu gani unakihitaji zaidi katika maisha... hapo wanakupata..
Ukikubali kutumika alafu usitekeleze inakuwaje?
 
Ndio tunashabikia kupigwa kwa taifa onevu la Israel, wezi wa ardhi, magaidi na wauaji... pasipo kupigwa hawawezi kuacha.

🔹 1. Qur'an 5:20 – (Surat Al-Ma’ida, Aya 20)

"Na (kumbuka) Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, pale alipowafanya Manabii miongoni mwenu, na akakufanyeni wafalme, na akakupeni asilivyowapa yeyote miongoni mwa walimwengu.
Enyi watu wangu! Ingieni katika nchi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekwisha kuwapeni..."

🔹 2. Qur'an 17:104 – (Surat Al-Isra, Aya 104)

"Na tukasema baada ya Firauni kuangamia: Enyi wana wa Israil! Kaeni katika nchi. Na wakati wa ahadi ya mwisho utakapowadia, tutawaleta kwa makundi."

🔹 3. Qur'an 7:137 – (Surat Al-A’raf, Aya 137)

"Na tukawarithisha watu waliokuwa wakionewa mashariki ya ardhi na magharibi yake, tuliyoibariki. Na yakatimia maneno mazuri ya Mola wako kwa wana wa Israil kwa sababu ya subira yao..."

🔹 4. Qur'an 2:47 – (Surat Al-Baqara, Aya 47)

"Enyi wana wa Israil! Kumbukeni neema yangu niliyokutendeeni, na nikakufadhilisha kul
iko walimwengu wote."
 
Israel imemuua kamanda colonel Ali Hossein Mohamed
View attachment 3377992
Ngoja tuulize kwanza!

@kobaz_eti hizi habari za vijana wa bibi Nyau kushambulia na kuua viongozi waandamizi wa Ayatollah ni za kweli?

Majibu: hizi khabari zinasambaa hasa kutoka kwenye vyanzo visivyo na uhakika, hasa JamiiForums na mitandao mingine isiyokuwa na uhakika wala siyo vya kuaminika.
Kwa uhakika tuliyonao vijana wa nyau ni dhaifu sana, kwa ujumla ni wachumba.
Vile vile ukizingatia vyuma alivyonavyo Kamenei, jambo hili haliwezi kutokea. Tutaendelea kukujuza kulingana na tutakavyoendelea kukusanya taarifa kutoka kwenye vyanzo sahihi, na hasa mtandao wa internet ukikaa vizuri huko kwa Kamenei.

Wasalaam.
 
🔹 1. Qur'an 5:20 – (Surat Al-Ma’ida, Aya 20)


Enyi watu wangu! Ingieni katika nchi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekwisha kuwapeni..."

🔹 2. Qur'an 17:104 – (Surat Al-Isra, Aya 104)



🔹 3. Qur'an 7:137 – (Surat Al-A’raf, Aya 137)



🔹 4. Qur'an 2:47 – (Surat Al-Baqara, Aya 47)


iko walimwengu wote."
Sheikh wangu Kosugi ya kweli haya
 
QURANI-ISRAEL NI TAIFA TEULE
🔹 1. Qur'an 5:20 – (Surat Al-Ma’ida, Aya 20)

"Na (kumbuka) Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, pale alipowafanya Manabii miongoni mwenu, na akakufanyeni wafalme, na akakupeni asilivyowapa yeyote miongoni mwa walimwengu.
Enyi watu wangu! Ingieni katika nchi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekwisha kuwapeni..."

🔹 2. Qur'an 17:104 – (Surat Al-Isra, Aya 104)

"Na tukasema baada ya Firauni kuangamia: Enyi wana wa Israil! Kaeni katika nchi. Na wakati wa ahadi ya mwisho utakapowadia, tutawaleta kwa makundi."

🔹 3. Qur'an 7:137 – (Surat Al-A’raf, Aya 137)

"Na tukawarithisha watu waliokuwa wakionewa mashariki ya ardhi na magharibi yake, tuliyoibariki. Na yakatimia maneno mazuri ya Mola wako kwa wana wa Israil kwa sababu ya subira yao..."

🔹 4. Qur'an 2:47 – (Surat Al-Baqara, Aya 47)

"Enyi wana wa Israil! Kumbukeni neema yangu niliyokutendeeni, na nikakufadhilisha kuliko walimwengu wote."
 
Vita hatuangalii nani kafa peke yake, tunaangalia chanzo (Causes) na malengo (Objectives) ya kijeshi, kisiasa, kiuchumi na kimkakati. Unaweza ukapigana vita halafu usitekeleze malengo yako kama ambavyo ungetumia diplomasia. Nadhani dunia ya leo hii ni lazima tuzingatie haya. Marekani aliua watu milioni 4 nchini Vietnam lakini hakutumiza malengo na kuishia kupata hasara nyingi kuliko faida.

Sasa kwenye vita ya Iran na Israel inabidi kitaalamu tunaanzae na kitu kinatwa Jus Ad Bellum (The Law Relating to the Use of Force). Hapa tunaangalia nini chanzo cha vita, na nani ameanzisha vita. Sheria za kimataifa hasahasa, The United Nations Charter 1945 zimeharamisha kabisa vita (War of Aggression). Vita ambazo zinaruhusiwa chini ya sheria za kimataifa ni zile za kujihami tu (Self-Defense) kama nchi, au vita zinazoruhusiwa na jumuiya ya kimataifa (Collective Self Defense) chini ya United Nations Security Council (UNSC).

Sasa tukianza na hapa, Jus Ad Bellum tunafahamu fika pasi na shaka kwamba Israel ndiyo amevunja sheria za kimataifa kwa kuivamia Iran kijeshi bila uhalali wowote ule. Hoja zao ni kwamba wanafanya hivyo kwasababu Iran imetishia kuwafuta na ina siku chache mno kuweza kutengeneza silaha za kinyuklia. Hizi hoja ni mufilisi kwasababu kisheria, vita za kuvamia kabla ya kuvamiwa (Anticipatory Self Defence/Pre-Emptive Attacks) haziruhusiwi.

Kisheria tukisema kila taifa livamie jingine ili kujilinda kwasababu za vitisho na bila kuwa na ushahidi wa kutosha nadhani dunia ingenuka. Dunia ikiruhusu hichi anachofanya Israel ina maana leo hii, Korea Kaskazini ambayo iko kwenye vita na Korea Kusini tokea mwaka 1953, inakuwa na ruhusu kuvamia jirani yake. AU India anakuwa na ruhusa ya kuvamia Pakistani bila hata uhalali wowote.

Hili nalisema kwasababu Jus Ad Bellum, husaidia katika kuleta mwafaka wa kidiplomasia ambao unahitajika mno kipindi hiki. Mwaka 2001 walisema Iraq ina silaha za maangamizi (WMDs) na baadaye ikafahamika ni wongo wa Israel, Marekani na Uingereza. Tena walivamia Iraq bila ruhusu ya UNSC. Hivyo tukizingatia haya, mpaka sasa Israel ni taifa la kihalifu, na hata NATO wakiingia nao watakuwa wanavunja sheria za kimataifa.

MALENGO YA KIJESHI: Israel anasema amevamia Iran ili kuzima kabisa mpango wake wa nyuklia. Ameua wanasayansi wengi mno na kulipua maeneo muhimu yenye vinu, lakini wiki sasa hajaweza kufanya chochote. Kaua viongozi wengi wa Iran na amefanya oparesheni ya kijasusi yenye ubora wa hali ya juu mno ndani ya Iran, lakini huwezi kushinda vita kwa kutegemea vikosi vichache vya makomando wanaotumia Drones.

Wakati Israel analipua vinu vya nyuklia vya Iraq mwaka 1981, Iran alijifunza somo moja kubwa ambalo ameenda nalo kwa miaka zaidi ya 40 mpaka kufika 2025. JIPANGE MAPEMA. Iran amesaidiwa na Korea Kaskazini katika kuchimba mahandaki yanayofika zaidi ya mita 300 kwenda chini wakitumia ULTRA HIGH PERFOMANCE CONCRETE (UPHC) ambazo ni bora kabisa duniani.

Hivyo ili kuzuia kabisa miradi ya nyuklia ya Iran inabidi uwe na makombora ya kuweza kupenya chini zaidi kupitiliza mita 300. Marekani ndiyo taifa pekee lenye makombora aina ya GBU-57 (Bunker Buster) lenye uwezo wa kupenya mita 200 kwenda chini. Israel hana hayo makombora aina ya GBU-57, yeye anatumia GBU-28 ambayo yana madhara lakini hayawezi kuvuka mita 30 kwenda chini, tena kwenye ULTRA HIGH PERFOMANCE CONCRETE (UPHC).

Marekani akiingia kuisaidi Israel ndiyo wanaweza kuuzima kabisa mpango wa nyuklia wa Iran. Japo, ili ifanyike hivyo ni lazima mambo yafuatayo yawepo:

Mosi, mfumo mzima wa ulinzi wa anga wa Iran inabidi uwe umezimwa au kuharibiwa kabisa. Mpaka sasa, wamefanikiwa kulipua mifumo mingi kwa kutumia majasusi waliokuwa wanafanya kazi ndani ya Iran ndiyo maana baadhi ya ndege za Israel ziliweza kupenya.

Pili, Israel anatakiwa atumia nguvu kubwa mno ya anga, mamia ya ndege za kijeshi (Strategic Bombers) kuangusha hayo makombora. Ndege ambazo zinaweza kutumika ni zile za Marekani kama B-2 Spirit ambazo ndizo za kisasa zaidi mpaka sasa duniani, zikisindikizwa na ndege nyingine nyingi. Hili ni rahisi kwasasabu Iran hana Credible Airforce kama Israel.

Haya mambo mawili mpaka sasa VIABILITY yake siyo rahisi. Mifumo ya ulinzi wa anga wa Iran haijaharibiwa yote na Marekani bado hajaingia kwenye vita. Akiingia nayo haitakuwa rahisi kwasababu huwezi kuwapiga Iran kwa kutumia anga peke yake, itabidi kuwe na wanajeshi wa chini. Ndege kuingia zinaweza kudunguliwa, ndiyo maana mpaka sasa Israel mbali na uwezo wake wote hajaweza kusababisha madhara makubwa kuweza kuwazuia Iran wasiwashambulie tena.

NGUVU YA IRAN: Iran hana CREDIBLE AIRFORCE wala CREDIBLE NAVY, ila Iran is a rocket and drone republic. Israel inatumia mifumo ya ulinzi wa anga kama The Iron Dome, David Sling-Shot, Arrow na THAAD, ambayo ni ya kisasa mno duniani, lakini imelemewe vibaya mno na Drones na Missiles za Iran.

Fahamu kwamba, umbali wa kutoka Israel hadi Iran ni kilomita 1500. Hivyo uwezo wa Iran kuishinda mifumo hiyo ni wa kipekee sana na unashangaza. Marekani akiingia itabidi ahakikishe kabisa anatumia kambi za jeshi za mbali kutunza ndege zake (Strategic Bombers), kwasababu hawezi kutumia Qatar, Saudi Arabia, Turkey wala UAE kufanya mashambulizi dhidi ya Iran, makombora ya Iran yasifike na kuleta madhara.

Sehemu ambayo Marekani anaweza kuweka ndege zake zikawa walau salama ni Diego Garcia, ambako umbali wake hadi Iran ni kilomita 4000. Kushambulia Iran kutokea Diego Garcia, will be a logistical nightmare, kwasababu ndege hizo inabidi zisishuke na zijazwe mafuta Mid-Air jambo ambalo pia ni hatari mno ukizingatia uwezo wa Iran.

Marekani akitumia manowari kufanya mashambulizi, unaweza kukumbuka tu, jinsi ambavyo The Houthis na roketi zao na drones za bei ya chini walifanikiwa kuzitesa manowari za kijeshi za mataifa ya NATO kwenye bahari ya shamu na kwingineko hadi kufanya washindwe kusogea karibu. Sasa Iran taifa ambalo lina maelfu ya Drones na Missiles za kisasa unadhani litazifanyaje manowari za Kimarekani ???

Hata kama watashinda, na kweli Marekani akiamua anaweza kumshinda Iran, madhara yatakuwa makubwa mno kwake. Wanasema itakuwa A Pyrrhic Victory au Ushindi wenye gharama kubwa mno kwa mshindi. Iran ana Anti-Ship Missiles zenye uwezo mkubwa ambazo zitaleta changamoto kubwa mno kwa American Carrier Fleet.

KUVAMIA KIJESHI: Israel hawezi kuvamia Iran kijeshi kwa kutumia jeshi la mguu. Marekani ndiyo anaweza kuivamia Iran kijeshi kwasababu ana kambi nyingi zenye kuizunguka Iran zenye wanajeshi wasiopungua 40000. Hili nalo ni gumu mno kwasababu litaleta madhara makubwa na it's a logistical nightmare.

Mwaka 2003 Iraq ilikuwa na watu 27 lakini ilimshinda Marekani kufanya FULL & EFFECTIVE OCCUPATION. Kijiografia Iran ni nchi kubwa mara mbili kwa Iraq yenye watu milioni 92 wenye historia ndefu hapa duniani. Kuvamia Iran kijeshi kutaleta madhara yasiyotabirika.

MWISHO: Tujikite kwenye MILLITARY OBJECTIVES, ambapo Israel anataka mambo mawili ambayo hajafanikiwa mpaka sasa:

1. Total Destruction of Iranian Nuclear Program.
2. Total Decapitation of Iranian Regime.

Kufanikisha hilo la kwanza, itahitaji zaidi ya kulipua vinu vya kinyuklia. Itahitaji kuua mamia ya wanasayansi wa Iran, jambo ambalo litafanikishwa endapo Marekani ataingia kwenye vita na kuivamia Iran kijeshi. Israel huo uwezo hana.

Lengo la pili lishaanza kufanywa, na limeonesha madhara na kuzua taharuki (Paranoia, Mistrust and Hysteria) kubwa ndani ya utawala wa Iran, japo bado halijawazuia Iran kuzidisha mashambulizi makubwa dhidi ya Israel, hasahasa kipindi hiki ambacho vita imeleta gharama kubwa mno kiuchumi kwa Israel.

Kupigana vita bila kutimiza malengo (Objectives) is a big waste of resources and a recipe for disaster.

=======================================================
​
Hongera kwa uchambuzi mzuri.
Vita si vizuri kila mtu anatakiwa kuvipinga ila ukifika wakati kupigana for existence inabidi.
Israel anasema anafight for existence. Iran aliapa kuifuta Israel.
Binafsi mpaka Sasa sijaona Iran inawezaje kuifuta Israel duniani. Na sioni kama Israel objectives zake ni inshu ya ku exist.
Nafkiri hapo kabla walisema hili ila sasa wanataka hayo mawili kuhusu nyuklia na regime change.
Ninavyoona ni bora nyuklia kuliko regime change. Khamein hawezi kubali kurudi matopeni na maendeleo yote yaonekane si kitu.
Naona Iran inaadaliwa kuwa Libya hasa involvement ya US ktk mgogoro.

Hoja yangu.
Iran hakujiandaa kisaikolojia, kimkakati wala kivita na Israel kwa sababu sijui kama ana mpango wowote kumzuia US maana US anaingia direct au indirect ingawa Trump hapendi vita lakini naona anaingia.
Swali Pakistan na India waliwezaje ku weponize nyuklia zao? Kwamba US alikaa kimya au walificha au walaitumia mbinu gani?
Je Tanzania tukianza kurutubisha kwa lengo la nishati uranium yetu yatatukuta haya au yanaikuta Iran kwa kuwa ni Muslim nation au ni hasimu wa US na Iran?
Naomba insight yako.
 
Back
Top Bottom