Hili suala la B-2 kupiga kinu cha nuclear cha Iran kuna watu niliwaambia hapa, GBU-57 bado haiwezi kuharibu hivyo vinu... na analysis niliyoweka hapa jf ndicho kitu kimetokea, wamepiga pa kuingilia lakini mitambo ya ndani yote ipo salama...
Niliandika hivi.. kwenye hii post
hapa 👇
Na kweli Israel haina kombora kufumua hivyo vinu hadi US imeingilia kati na kutumia GBU-57, na bado hawajafanikiwa kuharibu hivyo vinu...
Israel na US hakuna walilofanikiwa, hakuna cha regime change wala kuzuia Iran kuwa na nuclear, vyote hivyo wamefeli na ni aibu..
Kwa aibu Trump anaomba amani vita iishe, Trump ni kituko, amefahamu fika hawatoweza kuharibu mpango wa nuclear wa Iran. Pia wamefahamu kuwa hawana uwezo wa kuharibu hivyo vinu pasipo kushuka ardhini...
Nionacho US ameamua walau aonekane ameishambulia Iran, walau aonekane hajarudi nyuma na hajaiogopa Iran, mara tu baada ya Trump kushambulia vinu, Trump anaomba amani.
Ukweli ni kwamba hii ni namna ya kuiokoa Israel, US na Israel wamepiga mahesabu ya kujumlisha,kutoa , kugawanya na kuzidisha wameona hii vita ni hasara kubwa, Israel imeona haiwezi kuhimili, Trump pia ameona hana support ya wananchi na wabunge...
Wananchi wengi wa Israel maelfu wanakimbia nchi, makombora yanashuka kwa hali ya kutisha, licha ya kambi za US zilizopo kuanzia Iraq, Jordan na meli zilizopo baharini zinazozuia na mitambo ya ulinzi wa anga ya israel bado imefeli kuzuia...
Nionacho Iran ishambulie zaidi kwa makombora mazito zaidi Israel kabla hawajafikia makubaliano, Israel inajitahidi kuepuka hii vita kwa sababu wanaona wanashindwa na nchi inazidi kuharibiwa, wananchi wanazidi kukimbia nchi...
Iran ihakikishe Israel inalipa kwa ilicho kianzisha... Iran iwatandike vilivyo.