SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Iran:
TUNAKWENDA kufanya marekebisho machache kwenye mitambo yetu ya Nuklia Fordow na kisha inaenda kufanya kazi KWA Kasi kubwa.
Hii ni baada ya matokeo ya mashambulizi yaliyofeli ya B2 12 za US.

View attachment 3379851

Operation imegharimu karibu Bilioni 900 za kitandania ndani ya DAKIKA chache bila mafanikio ya kujivunia. Imeacha MADHARA ya vitundu vichache KWA juu kama sita hivi.
Sasa kikianza kufanya kazi wataona kiashiria Cha nuclear.
Au basi ni propaganda
 
Wanasema wameshambulia access roads, maana kumbe Iran alienda ziba milango yote kwa kumwaga mchanga wakutosha
Hicho kinu kipo kama jangwani hivi Yani ambalo gari alipotiki unauhitaji barabara ndo gari lipite
 
Israeli na Marekani ni kama tu ile 'Midfield' niliyoyoipenda ya Xavi Hernandez chini na Andres Iniesta juu hapa utake usitake utapigwa / utafungwa tu

Yaani hizi Midfield zote Iniesta (Israeli) na Xavi (Marekani) zikikutafuta kamwe huwezi kutoka salama na utafungwa tu Ok?
 
Hivi ukiangalia kitu Israel anacho wafanyia watu wa gaza unaweza sema ni nani gaidi kati ya Iran na Israel.
Maana Israel anacho kifanya huko gaza ni unyama ambao hata shetani mwenyewe ana pingwa butwaa.
HAMAS na HEZBOLAH ndyo wakuwalaumu
 
Mgogoro kati ya Iran na Israel umechukua sura mpya ya hatari mwezi huu wa Juni 2025, ukibeba historia ya chuki ya muda mrefu, mashambulizi ya maneno, na sasa mashambulizi ya moja kwa moja.

Chanzo chake ni cha muda mrefu, lakini hali ya sasa imechochewa na mfululizo wa matukio makubwa yaliyoanza rasmi kufumuka upya mnamo Aprili 13, 2024, wakati Iran ilirusha makombora na ndege zisizo na rubani zaidi ya 300 dhidi ya Israel ikiwa ni mara ya kwanza kwa Iran kuishambulia Israel moja kwa moja kutoka ardhi yake. Israel ilijibu kwa shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya miundombinu ya kijeshi ya Iran katika mji wa Isfahan, ikieleza kuwa ni kulinda mamlaka yake na kuzuia mashambulizi ya baadaye.

Mwezi huu, tarehe 9 Juni 2025, shambulizi kubwa la anga lilitokea karibu na mji wa Kermanshah, magharibi mwa Iran, likielekezwa kwenye kituo cha kijeshi cha Kikosi cha Quds cha Jeshi la Mapinduzi la Iran (IRGC). Katika shambulizi hilo, maafisa waandamizi watano wa IRGC waliuawa, akiwemo Kamanda wa operesheni za nje Brigedia Jenerali Hassan Rahimi. Ingawa Israel haijathibitisha rasmi kuhusika, vyombo vya habari vya kimataifa na wachambuzi wa usalama wamehusisha Israel moja kwa moja na shambulizi hilo, wakilitaja kuwa moja ya mashambulizi ya "kisasa, cha kimkakati na chenye athari kubwa zaidi" kufanywa dhidi ya Iran mwaka huu.

Baada ya tukio hilo, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alitoa kauli kali tarehe 10 Juni 2025, akisema:



Hadi sasa, Iran inaendelea kujiandaa kwa kile inachokiita “jibu la kimkakati”, huku mashirika ya Iran kama Hizbullah, wanamgambo wa Iraq, na vikundi vya Syria vikionekana kuongeza ujasiri wa mashambulizi dhidi ya Israel na washirika wake. Nayo Israel inaendelea kufanya mashambulizi ya kijeshi nchini Syria na kuimarisha mfumo wake wa ulinzi wa angani kwa kuungwa mkono na Marekani.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa usalama wa Mashariki ya Kati, hatma ya mgogoro huu inabaki kuwa tete sana. Ikiwa mashambulizi kama haya yataendelea, kuna uwezekano wa kuingia katika vita ya wazi baina ya Iran na Israel, ambavyo vinaweza kuvuruga usalama wa kanda nzima na hata kuvuta mataifa makubwa kama Marekani, Urusi, na Saudi Arabia katika mzozo huo.
Nchi zenye nguvu za kiaarabu zinaisapoti Isarel kuimaliza Iran, hawamtaki Ayatoulah
 
Missile interceptors ndio zilikuwa zinatumika Vietnam war miaka ya 1960s.
Iran leo 2025 wanazitegemea hizo baada ya missile systems kuharibiwa vibaya. Ndio imeisha hiyo hakuna turning point.
Naamini Urusi naye anapigika vizuri, ni vile tu hawajaamua kumtoa pale, hata Ukraine alipewa silaha nzuri anamtoa vizuri tu
 
Back
Top Bottom