SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Mkuu upo sawa na ni ukweli ulio wazi US akiingilia hii vita military base zake zote zitafutwa middle East Aircraft carrier itapigwa

Lakini nakuhakikishia kwa Anga la Iran lilivo uchi US akiingilia Iran na utawala wa ayatollah ndio utakua mwisho kuna mambo mengine yanaitaji U discuss kwa kutumia logic na sio Emotional
 
Sa hapo umelewa au unajitoa akili, aliye anzisha vita nani na pia lazima ufahamu jawabu la Iran hawasimamishi vita mpaa aliye anzisha vita ainue mikono.
Maelezo ya huyu waziri kwa namna moja ama nyingine anahitaji sana mazungumzo yafanyike ya kusitisha hiyo vita; kwa sababu na yeye anaogopa kufa kama hao viongozi wengine.

Ameongea kwa lugha ya kiungwana sana bila kumkwaza yeyote.​
 
Dingii ni kwerekweche Iran kasharusha tena madude baada ya kupgwa mda mfupi uliopita
Iran ni kenge sana Israel anapafanya hamna huko ukobazini
 
Sa hapo umelewa au unajitoa akili, aliye anzisha vita nani na pia lazima ufahamu jawabu la Iran hawasimamishi vita mpaa aliye anzisha vita ainue mikono.
Unajua kusoma vizuri hao Iran hali mbaya apo wanaomba poo kwa Israel apunguze moto 🔥 🔥 akiacha nao wanatulia walitaka maongezi ya amani na rais cyphurus Israel ikawakataa
 
Najua sababu. Wewe unayojua ni ipi
Hapo juu si unamkosoa Ayatollah ili mtu abaki katika nafasi yake si lazima amsikilize yeye ata Rais wa Iran? Sasa niambie huyo Waziri wa Ulinzi wa Israel kilichokamtoa nini kama wakisikilizana na Netanyahu? Au Rabin aliuawa sababu gani hapo Israel?
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Iran italipa "gharama kubwa sana" kwa vifo vya raia wa Israel.

Akizungumza katika eneo kulikotokea shambulizi la kombora kwenye jengo la makazi huko Bat Yam, Netanyahu anayaita "mauaji ya kukusudia ya raia, wanawake na watoto", na anasema Iran ni "tishio" kwa Israel.

Aliongeza kuwa "nina huzunika" kwa waliouawa, na kwamba "mioyo yetu iko pamoja na familia", huku akiwataka watu kufuata maagizo ya usalama kutoka kwa maafisa.
 
Jeshi la Ulinzi la Israel linasema ving'ora vimelia katika maeneo kadhaa kote Israel baada ya kutambua makombora yaliyorushwa kuelekea nchini humo kutoka Iran.

Jeshi la Wanahewa la nchi hiyo "linafanya kazi ya kuzuia na kushambulia pale inapobidi ili kuondoa tishio," linasema.

Inaongeza kuwa watu wanapaswa kuendelea kufuata maagizo kutoka kwa Kamandi ya Masuala ya Ndani ya Nchi.

Wakati huo huo, Televisheni inayomilikiwa na serikali ya Iran imesema 'makombora ya kulipiza kisasi' yamerushwa dhidi ya Israel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…