SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Zimeaanza kushuka....
waisrael wa bonyokwa mkae mkao kuliwa....
Nyau anaomba poo sasa...


View attachment 3370389
Aise huyu Iran ni habari nyingine kabisa.

Siku ya tatu mfululizo Mazayuni hawajapata usingizi kila ikifika usiku ni mwendo wa makombora tu kudadadekiii.😂

Miji ya Israel itageuka magofu kama Gaza.

What goes around comes around.
 
Watu wengi nchini Israel wamekubwa na mshtuko asubuhi ya leo baada ya mashambulizi mawili ya makombora ya Iran yaliyoua takriban watu 10, wakiwemo wanawake wanne wa familia moja katika mji wa Tamra, na mvulana wa miaka 10 na msichana wa miaka minane katika mji wa Bat Yam.

Maafisa wa Israel walikuwa wameonya kuwa nchi hiyo itakabiliwa na siku ngumu, huku wakifanya mashambulio yasiyo na kifani dhidi ya Iran.

Israel imedokeza kuwa hii itakuwa tukio la muda mrefu - ambalo linaweza kuchukua wiki, sio siku - lakini lengo lake la mwisho bado haliko wazi.

Jana usiku, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema mashambulizi ambayo tayari yametekelezwa si kitu ikilinganishwa na yale ambayo Iran itashuhudia katika siku zijazo.

Mamlaka za Israel zinasema kuwa ni haki kwa hatua kama hiyo kuchukuliwa kwa sababu Iran ilikuwa inafikia kiwango kibaya cha utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Wengi wanahoji hilo, na Iran imekuwa ikisema mara kwa mara kwamba mpango wake wa nyuklia ni kwa madhumuni ya amani, jambo ambalo Israel inaendelea kukataa.

Wakosoaji wa waziri mkuu wanasema hivi ni vita vya kujichagulia, na kwamba diplomasia inasalia kuwa njia pekee ya kutatua suala linalozunguka mpango wa nyuklia wa Iran.
'Asubuhi ya huzuni na ngumu sana' - rais wa Israel
Wakati huo huo, Rais wa Israel Isaac Herzog ameandika kwenye X, "Asubuhi ya huzuni na ngumu sana," alisema wakati nchi hiyo inaamka ikiwa imeshambuliwa na Iran katika maeneo yake ya kati na kaskazini.

"Mashambulizi ya uhalifu ya Iran" yaliwaua na kujeruhi "Wayahudi na Waarabu, raia wa Israel na wahamiaji wapya, wakiwemo watoto na wazee, wanawake na wanaume," Herzog anasema.

Aliongeza: "Niko pamoja na familia wakati huu wa maombolezo mazito na msiba huo mbaya. Ninawaombea majeruhi wapone na kupatikana kwa waliopotea. Tutaomboleza pamoja. Tutashinda pamoja."
 
Ngoja ni tune on nishudie vimondo maana katika hili Iran kani suza moyo kitu kina dodge interceptions za iron Dome kwa Kasi ya mwanga kina impact
Ni hatari aise. Hakuna cha THAAD wala Arrows 3 wala THAAD vyuma vinapita bila kupingwa mkuu.

This time Israel ameyatimba na atajuta kuingia kichwa kichwa akidhani ile ni Gaza.
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Iran italipa "gharama kubwa sana" kwa vifo vya raia wa Israel.

Akizungumza katika eneo kulikotokea shambulizi la kombora kwenye jengo la makazi huko Bat Yam, Netanyahu anayaita "mauaji ya kukusudia ya raia, wanawake na watoto", na anasema Iran ni "tishio" kwa Israel.

Aliongeza kuwa "nina huzunika" kwa waliouawa, na kwamba "mioyo yetu iko pamoja na familia", huku akiwataka watu kufuata maagizo ya usalama kutoka kwa maafisa.
Kobazi wanasema yupo Greece
 
Back
Top Bottom