Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

#Gostomel , airfield, Russians have already dug up something
 
Pro NATO Wanaumia sana kuona NATO wanashindwa kumvamia Mrusi kama ilivyokuwa kwa Iraq na kinachonishangaza kuna watu zinasema siku za Russia zimefika. Najua hii inaumiza na Pro NATO hawataki kusikia lakini vita kati ya NATO na RUSSIA ni vita ya Nyuklia na kuna uwezekano isirushwe hata risasi moja.

Ukitaja kujua Russia atatumia silaha zipi vita ya tatu ni sasa ambapo hana hata Presha NATO wakija na mipango sijui tunaimarisha mpaka wa Poland sijui tunaongeza askari Lativia, Romania, Slovakia na Hungary mwenzao hana hata wasiwasi kabisa maana kauli mbiu yetu Kremlin ni HAPA NUKES TU
Hapa Nukes tu kudadadyeki hatucheki na boya!
 

Missiles from Germany arrive in Ukraine: reports​

A shipment of 1,500 Strela anti-aircraft missiles and 100 MG3 machine guns have arrived in Ukraine from Germany, the German Press Agency cited Ukrainian government officials as saying.
German Foreign Minister Annalena Baerbock said on Wednesday that further supplies of the Strela missiles were Ukraine-bound following delays in deliveries.
The Russian invasion of Ukraine has seen Germany reverse its historical policy of not sending weapons to conflict zones.
"We are one of the biggest weapons suppliers in this situation, it doesn't make us proud but it's what we must do to help Ukraine," Reuters quoted Ms Baerbock as saying.

Tukiwaambia Russia ni simba wa karatasi muwege mnaelewa
 
Hizo silaha zinafikaje bila Urusi kuziona? Maana nimeona Drones, strellas, generators

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mipaka ya Ukraine ni mikubwa mno na mingi ipo kwenye udhibiti wa serikali hasa upande wa magharibi.
Ebu angalia eneo kama Gaza kwa mfano ni mji wenye ukubwa kama mji wa mwanza na Israel imeuzingira kila sehemu lakini bado silaha zinaingia na kuwafikia hamasi sasa jiulize zinapita wapi?
 
Embu niambie lengo la Russia kuivamia ukraine ilikua ni nini? Kwenda kuikamta kiev.? Rejea maneno ya malengo ya vita ya Rais Putin, Ukraine akijiunga NATO, akijenga upya jeshi lake, sio hili la kuomba msaada kila siku, pia akifanikiwa kurejesha yale majimbo mawili yaliyojitenga basi atakua mshindi mkubwa wa vita regardless watu waliokufa.

Urusi akichukua donbase, maana cremea tayari pia Ukraine ikikataa kujiunga nato na kupunguza jeshi, Russia ataibuka mshindi. Msitoke nje ya mada.

Conventional war imemshinda Nato pale Syria. Msijasahaulishe.
Simwoni mtu yeyote anayeona Ukraine itafukuza Jeshi la Urusi kutoka maeneo yake. Ukraine ikifaulu kujitetea katika sehemu kubwa ya maeneo yake na Urusi ikishindwa kuvunja upinzani huo, basi Ukraine itakuwa mshindi.
Urusi inaweza kujitazama mshindi ikifaulu kuteka mashariki ya Ukraine pamoja na Kiev na Kharkiv na kulazimisha mabaki ya Ukraine kukubali hayo.
Uwezekano mkubwa ni tutaona matokeo ya katikati. Kwa bahati mbaya kwa gharama ya mauaji mengi ambayo ni balaa. Putin anahitaji kuonyesha kitu ili aweze kujitangaza kuwa "mshindi".

Tangazo la mwisho wa Jeshi la Urusi lilidai tayari kuwa wamefaulu ngazi ya kwanza; yaani kuvunja nguvu ya kijeshi ya Ukraine. Ni dhahiri hii si kweli lakini wangeweza kutumia matangazo ya aina hiyo kusema baadaye "Tumeshinda!" na kujitetea hivyo mbele ya raia wao. Sasa wanasema kwamba shabaha yao ni "ukombozi wa Donbass". Wakikusanya nguvu zote hapo kuna uwezekano kwamba wanavunja sehemu ya jeshi la Ukraine inayotetea hapo.

Haina uhakika, inategemea kama wanaweza kujifunza na kusahihisha udhaifu walioonyesha hadi sasa. Kinyume inawezekana pia, mfano sehemu kubwa zaidi ya wanajeshi wao kugoma. Tunapaswa kutazama.

Kwa jumla Putin alipata matokeo ambayo ni kinyume ya mengi aliyolenga. Amefaulu kuunganisha NATO kiasi hakuna aliamini wiki 4 iliyopita. Amefaulu pia kuunganisha Umoja wa Ulaya. Uwezekano mkubwa sana amefaulu kurudisha nchi yake nyuma kiuchumi. Kisiasa tayari, baada ya kunyamazisha kila sauti iliyoweza kumkosoa (magazeti, redio, runinga). Kiutu pia, tumwite "Mirambo Mrusi" (nilisoma jina Mirambo lilimaanisha maiti, na yale aliyojenga kwa vita zake yaliporomoka haraka...)
 

Missiles from Germany arrive in Ukraine: reports​

A shipment of 1,500 Strela anti-aircraft missiles and 100 MG3 machine guns have arrived in Ukraine from Germany, the German Press Agency cited Ukrainian government officials as saying.
German Foreign Minister Annalena Baerbock said on Wednesday that further supplies of the Strela missiles were Ukraine-bound following delays in deliveries.
The Russian invasion of Ukraine has seen Germany reverse its historical policy of not sending weapons to conflict zones.
"We are one of the biggest weapons suppliers in this situation, it doesn't make us proud but it's what we must do to help Ukraine," Reuters quoted Ms Baerbock as saying.

Tukiwaambia Russia ni simba wa karatasi muwege mnaelewa
Strela zinarudi nyumbani...
Maana ni makombora ya Kirusi ambazo zilikuwa silaha za jeshi la Ujerumani Mashariki; baada ya maungano ya Ujerumani 1990 zilirithiwa na Jeshi la Ujerumani; hapo zulitumiwa kidogo kwa mazoezi. Strela zilitakiwa kuharibiwa na kutupwa lakini Wajerumani walichelewa kutekeleza mpango huu. Sasa zinanangaliwa kwenye ghala ya jeshi Ujerumani na zile zisizo na kutu kutumwa Ukraine.... Maajabu ya vita
 
Najua watawasingizia Urusi,this is a false flag. Ninavyojua jeshi la Ukraine ambalo limejaa Nazis,wameua wananchi in collaboration with the West,halafu wasingizie jeshi la Urusi,ili wapate sababu za kuanzisha WWIII.These nuts and psycopaths will not rest until they have started WWIII for the sole purpose of annihilating Russia and so create conditions for a Global Government.
Nikisoma unachoandika - sidhani unajua kitu chochote.
 
Mwezi umeisha unasema ivi ivi

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Hakuna sehemu yoyote Kremlin waliposema itachukua muda gani kumaliza Operation yao hivyo ikichukua muda mzuri zaidi ndio Putin anataka kwa sababu Urusi na Ukraine ndio nchi zinazozalisha ngano kwa wingi duniani hivyo operation ikichelewa Ngano itakuwa inatokea Urusi na njaa itaibuka duniani baada ya hapo tunarudi mezani kupanga njia ya kulipana tena, ITS RUBBLE AGAIN
 
Simwoni mtu yeyote anayeona Ukraine itafukuza Jeshi la Urusi kutoka maeneo yake. Ukraine ikifaulu kujitetea katika sehemu kubwa ya maeneo yake na Urusi ikishindwa kuvunja upinzani huo, basi Ukraine itakuwa mshindi.
Urusi inaweza kujitazama mshindi ikifaulu kuteka mashariki ya Ukraine pamoja na Kiev na Kharkiv na kulazimisha mabaki ya Ukraine kukubali hayo.
Uwezekano mkubwa ni tutaona matokeo ya katikati. Kwa bahati mbaya kwa gharama ya mauaji mengi ambayo ni balaa. Putin anahitaji kuonyesha kitu ili aweze kujitangaza kuwa "mshindi".

Tangazo la mwisho wa Jeshi la Urusi lilidai tayari kuwa wamefaulu ngazi ya kwanza; yaani kuvunja nguvu ya kijeshi ya Ukraine. Ni dhahiri hii si kweli lakini wangeweza kutumia matangazo ya aina hiyo kusema baadaye "Tumeshinda!" na kujitetea hivyo mbele ya raia wao. Sasa wanasema kwamba shabaha yao ni "ukombozi wa Donbass". Wakikusanya nguvu zote hapo kuna uwezekano kwamba wanavunja sehemu ya jeshi la Ukraine inayotetea hapo.

Haina uhakika, inategemea kama wanaweza kujifunza na kusahihisha udhaifu walioonyesha hadi sasa. Kinyume inawezekana pia, mfano sehemu kubwa zaidi ya wanajeshi wao kugoma. Tunapaswa kutazama.

Kwa jumla Putin alipata matokeo ambayo ni kinyume ya mengi aliyolenga. Amefaulu kuunganisha NATO kiasi hakuna aliamini wiki 4 iliyopita. Amefaulu pia kuunganisha Umoja wa Ulaya. Uwezekano mkubwa sana amefaulu kurudisha nchi yake nyuma kiuchumi. Kisiasa tayari, baada ya kunyamazisha kila sauti iliyoweza kumkosoa (magazeti, redio, runinga). Kiutu pia, tumwite "Mirambo Mrusi" (nilisoma jina Mirambo lilimaanisha maiti, na yale aliyojenga kwa vita zake yaliporomoka haraka...)
analysis nzuri sana kiongozi
 
Strela zinarudi nyumbani...
Maana ni makombora ya Kirusi ambazo zilikuwa silaha za jeshi la Ujerumani Mashariki; baada ya maungano ya Ujerumani 1990 zilirithiwa na Jeshi la Ujerumani; hapo zulitumiwa kidogo kwa mazoezi. Strela zilitakiwa kuharibiwa na kutupwa lakini Wajerumani walichelewa kutekeleza mpango huu. Sasa zinanangaliwa kwenye ghala ya jeshi Ujerumani na zile zisizo na kutu kutumwa Ukraine.... Maajabu ya vita
Hapo ndo ujue Russia ni hatari kwenye teknolojia ya silaha, yaani kama silaha alizoziacha huko Ujerumani karne ya 20 huko wakati tupo karne ya 21 na mjerumani anachofanya ni kufuta vumbi tu. Nasema hivi NATO kwa Russia ni kusanyiko la nzi makelele mengi sikioni lakini hata hawaumi
 
Screenshot_20220326-092659.jpg
 
urusi yasema sasa itaelekeza nguvu zake kwe lengo lake kuu ambalo ni kuikomboa eastern Donbas baada ya operaion yake across ukraine yote kufanikiwa tayari
Je ni kweli operation ya urusi ndani ya ukraine imeshafanikiwa kiasi cha urusi kurudi kwenda kudeal na donbas au imekwama kaona ni heri akadeal na donbas tu? wenye connections zenu kremlin na white house leteni info
Iko hivi mtu mzima akiwa anaenda kunya kichakani huaga kiutu uzima kwa kusema anaenda kukata gogo la kuni

Putin sasa hivi anapigwa kila upande na Ukraine kwenye maeneo yote aliyovamia.Majeshi yake sasa anataka aya withdrawal in actual fact anakimbia vita ndipo anakuja na propaganda kuwaanata ku concentrate kwenye eneo moja tu la Donbas !!! Kipigo alichopata kwa Ukraine ndicho kinamkimbiza anaaga kitu uzima kuwa sikimbii vita naenda Donbas!!!!
 
Back
Top Bottom