Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Nini kinaendelea huko tuambieni

Majenerali waliouawa​

Yakov Rezantsev

Luteni Jenerali Yakov Rezantsev aliripotiwa kuuawa kwa shambulizi la Ukraine kwenye uwanja wa ndege wa Chornobaivka karibu na mji wa Kherson.
Alipandishwa cheo na kuwa Luteni jenerali mwaka jana, na alikuwa kamanda wa jeshi la 49 la wilaya ya kijeshi ya kusini mwa Urusi.
Inasemekana alishiriki katika operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Syria.
Andrei Mordvichev

Andrei Mordvichev aliuawa na shambulizi kwenye uwanja wa ndege wa Chornobaivka karibu na Kherson, kulingana na maafisa wa Ukraine.
Alikuwa kamanda wa jeshi la 8 la pamoja la Urusi la wilaya ya kijeshi ya kusini.
Kifo chake kiliripotiwa tarehe 18 Machi.
Oleg Mityaev graphic

Meja Jenerali Oleg Mityaev aliripotiwa kufariki mahali fulani karibu na jiji la Mariupol, jiji lililo kusini-mashariki mwa Ukraine ambalo limeshuhudia mapigano makali zaidi kufikia sasa.
Kikosi cha kitaifa cha Azov kinadai kumuua.
Alikuwa kamanda wa kitengo cha 150 cha bunduki za magari cha jeshi la Urusi, kitengo kipya kilichoundwa mnamo 2016, na kilichowekwa katika mkoa wa Rostov karibu na mpaka wa Ukraine.
Ukraine inadai kuwa kitengo hicho kiliundwa ili kushiriki katika mzozo katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi mashariki mwa Ukraine, ingawa Urusi inakanusha kuwa jeshi lake lilihusika katika mapigano huko.
Andrei Kolesnikov graphic

Meja Jenerali Andrei Kolesnikov, wa jeshi la pamoja la 29, aliuawa katika mapigano tarehe 11 Machi, kulingana na vyanzo rasmi vya Ukraine.
Mazingira ya kifo chake hayakubainishwa.
Baada ya Kolesnikov kuwa jenerali wa tatu wa Urusi kuripotiwa kuuawa nchini Ukraine, afisa mmoja wa nchi za magharibi aliambia chombo cha habari cha PA kwamba jeshi la Urusi linaweza kuwa na ari ya chini, na ndiyo maana maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi wanasonga mbele kwenye mstari wa mbele.
Vitaly Gerasimov

Meja Jenerali Vitaly Gerasimov, mkuu wa wafanyakazi wa jeshi la 41 la Urusi, aliuawa tarehe 7 Machi nje ya mji wa mashariki wa Kharkiv, kulingana na wizara ya ulinzi ya Ukraine.
Kharkiv, karibu na mpaka wa Urusi, imekuwa chini ya mashambulizi endelevu kutoka kwa vikosi vya Urusi.
Jeshi la Ukraine lilitoa rekodi ya kile ilichosema maafisa wawili wa usalama wa Urusi wakijadili kifo cha Gerasimov, na kulalamika kwamba mitandao yao salama ya mawasiliano haifanyi kazi tena nchini Ukraine.
Gerasimov alihusika katika vita vya pili vya Chechnya, operesheni ya kijeshi ya Urusi huko Syria, na katika unyakuzi wa Urusi wa Crimea mnamo 2014.
Andrey Sukhovetsky

Meja Jenerali Andrey Sukhovetsky, naibu kamanda katika kitengo sawa na Gerasimov, aliripotiwa kuuawa na mdunguaji mnamo tarehe 3 Machi.
Kama Gerasimov, Sukhovetsky alikuwa sehemu ya operesheni za kijeshi za Urusi huko Crimea na Syria.
Tofauti na majenerali wengine, kifo cha Sukhovetsky kiliripotiwa kwenye vyombo vya habari vya Urusi na Rais wa Urusi Vladimir Putin alithibitisha katika hotuba yake kwamba jenerali mmoja alikufa huko Ukraine.
 
Qatar will not be able to help Europe with gas supplies now, there is no alternative to Russia at this stage, said Saad bin Sharid al-Kaabi, State Minister for Energy of the Emirate.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] US haifikii Qatar kwa reserve ya gas lakini anawaambia wasijali atawahudumia.

US anajaribu kukwepa utabiri wa kuwa utawala wake utaanguka na kuinuka kwa utawala wa East. Sasa anafanya vita vya ukraine kumdhoofisha kiuchumi Urussi ila hawezi coz jamaa unaambiwa walijipanga sana yani wamejipanga vilivo
 
Hii ni JF. Lengo la Uzi ni kupashana habari, kusimuliana, kuelimishana na kujadili pale inapobidi.

Huu mnakasha umebeba yote. Ila umahususi wa huu mnakasha mzizi mkuu wake ni fact.

Sasa haiwezekani unaandika jambo halafu ukihojiwa ithibati yake unasema hayo ni mawazo yako binafsi. Hii inaonyesha ubinafsi, unasiasa za kilafi kwa sababu ni siasa za kimslahi yako binfasi. Hutaki kujibu hoja una-dictate mawazo yako. In short una elements za u-dictator.

Tena tukuulize swali: Putin kairudisha sana nchi yake nyuma sana kiuchumi kivipi?
Vita ni gharama kubwa, bidha hauzi nje, deni la Urusi limekuwa kubwa(riba) masha ya askari wengi yamepotea.....
 
US anajaribu kukwepa utabiri wa kuwa utawala wake utaanguka na kuinuka kwa utawala wa East. Sasa anafanya vita vya ukraine kumdhoofisha kiuchumi Urussi ila hawezi coz jamaa unaambiwa walijipanga sana yani wamejipanga vilivo
Kweli walijipanga..tena likuwa wamalize vita siku 2 au 3 hivi.....
 
Uchumi wa Marekani peke yake ni mkubwa mara 20 zaidi ya Uchumi wa Rusia. Ukiunganisha uchumi wa China, India na Russia kwa pamoja bado hazifikii uchumi wa USA kwa ukubwa wake, hawa wote mshirika wao mkubwa biashara ni USA au EU sasa watakataa kutumia dola kwa sababu gani?? Sijazungumzia mataifa karibia yote duniani, na wafanyabiashara wote wanapenda na wanalazimika kweka reserves na akiba zao katika US dollars. Russia anafanya vitimbi vya kitoto tu, anapambana na superpower halisi.

Hata gavana wa benki kuu ya Russia ambaye ni msomi wa Yale University ya Marekani anafahamu hivyo na alikuwa anapinga sana huu uvamizi akijua utaharibu uchumi wao.

Pia jifunze kwa nini US Dollar inapendelewa zaidi katika biashara duniani kote. Dollar ni pesa isiyoyumba kama mlevi, Ni currency stable kuliko zote duniani.

CHINA Kashamwacha US mbali sana kiuchumi ila data tunadanganywa. Inshort utawala wa marekani upo mbioni kuanguka [emoji28]
 
Labda tuna Putin mwengine pande hizi
Ndiyo atueleze!

Tanzania ilifanya operation ya kijeshi nchini Kongo dhidi ya M23. Iliitwa operation chakaza na ikawachakaza.

Putin amesema ameenda Ukraine kufanya operation ya kijeshi dhidi ya kupunguza nguvu ya jeshi la Ukraine na kuondoa ma-Nazi.

Bw. Mkubwa katuambia kuwa hizi ni vita. Kwa kweli tunamshukuru. Ila mimi nilimsikia Putin kasema ni operation. Sasa sijajua kati ya yeye na Putin yupi ndiye Putin mwenyewe?
 
Ndiyo atueleze!

Tanzania ilifanya operation ya kijeshi nchini Kongo dhidi ya M23. Iliitwa operation chakaza na ikawachakaza.

Putin amesema ameenda Ukraine kufanya operation ya kijeshi dhidi ya kupunguza nguvu ya jeshi la Ukraine na kuondoa ma-Nazi.

Bw. Mkubwa katuambia kuwa hizi ni vita. Kwa kweli tunamshukuru. Ila mimi nilimsikia Putin kasema ni operation. Sasa sijajua kati ya yeye na Putin yupi ndiye Putin mwenyewe?
Operesheni wanatumia nini na vita wanatuma nini mkuu.....
 
Hapa atakuwa wanawatishia Ulaya, US mafuta yake mengi na gesi yake nyingi anachukua Mexico, Canada na Uarabuni.
Pia anachimba nchi kwake.

Isingekuwa EU Russia angekula vikwazo hadi kwenye hiyo gesi yake.

Alokwambia Us ana gas nyingi nani? Na US anareserve kubwa tu ya mafuta sio producer mkubwa wa mafuta. Msidanganywe na west propagandas hali ya Europe kwa sasa ni mbaya sana maisha yako juu hizi hbr huwez pata kwenye media zao.

Gap la Russia kwenye nishat halizibiki kirahis qatar kawatolea nje, huko saudia kuna visima vimelipuliwa ma waasi wa Yemen.

Hii ligi si mlianzisha?? Taifa moja vs mataifa 30 wtf???
 

Russian general who said war would take hours is killed in Ukraine​

Lt Gen Yakov Rezantsev, 48, was killed in an airstrike in the southern city of Kherson
1648313983205.png

1648314058368.png

1648314271013.png

1648314308118.png

1648314401021.png

1648314780127.png
 
Mnadanganywa na nani?

GDP ya China ni kiasi gani? GDP ya US ni kiasi gani huko ambako hamjadanganywa?
CHINA Kashamwacha US mbali sana kiuchumi ila data tunadanganywa. Inshort utawala wa marekani upo mbioni kuanguka [emoji28]
 
tatizo hapo sio exchange, exchange imekua ikifanyika miaka yote, hapa ni kuwa europe iwe na reserve ya ruble kwajili ya kupay bill za gas, sasa nan yuko tayar kukalia hifadhi ya ruble ambayo leo iko juu kesho chini keshokutwa kati? haifloat free na mengineyo ndio maana ht urusi yenyew imewekeza kwe euro/dollar, issue sio exchange hapa
US inataka dollar itumike kila mahala hasa kwa nchi zenye petroleum, hii itafanya dollar iwe kwenye demand kubwa na wataprint za kutosha.

Kuikataa dollar ndicho kilimponza Gaddadi na Sadam, Russia kwa kufanya hivi itafanya ruble kuwa kwenye demand kubwa na kui strength.

Wawe na reserve ama wafanye exchange kama Gazprom itapokea ruble kwenye mauzo ya gas, basi US Federal Reserve itakuwa imepigwa biiiig MF cause ruble itakuwa kwenye demand.

Inawezekana kutumia ruble, issue sio kuwa stable, issue ni sanctions.

China yenyewe huwa inanunua gas Iran kwa yuan.

Hata Euro haipo stable kama dollar, Sadam alitaka ku switch toka kwenye $ kwendaa kwwnye euro, you know what happened na mwenzake gaddadi alitaka gold.

Wafanya biashara wengi wakubwa sana kwenye industry hivi sasa huko Asia wanatumia bitcoin.
 
Nafikiri unajaribu kulikimbia swali langu. Ulisema Russia anatumia mbinu za kizamani. Tuambie mbinu mpya ni zipi? Hili ndilo swali langu.

Swali la pili lilitokana na nukta yako kuwa Russia haikuwa united kwenye hili la kumvamia Ukraine:Nani kakwambia hawakuwa united kwenye uvamizi huu? Hapa napo haujajibu.

Nimekuuliza swali, umejibu hili suala lipo wazi! Nionyeshe huo uwazi nami niuone.

Msingi wa hoja yako kwenye nukta ya pili haukubaliani na historia, na historia ni fact. Kinachoonekana haufanyi uchambuzi bali unaelezea kile unachokiona kupitia vyombo vya habari.

Jiulize kwa nini ikiwa kama ni boxing watachambua uwezo wa wapiganaji mmoja mmoja kabla ya mchezo kuanza kisha kubainisha nguvu ya huyu ipo juu kuliko mwenzake. Halikadhalika na nguvu za jeshi baina nchi na nchi wanafanya vivyo hivyo. Unafikiri kilichoangaliwa ni kipi? Sasa kuna utofauti kati ya uchambuzi na kukielezea kile unachokiona. Kuelezea unachokiona; haya yanaitwa ni mawazo binafsi juu ya suala fulani na wala hayamaanishi kuwa ni fact ijapokuwa yanaweza kuwa ni fact.

Putin hana namna akubali yaishe kwa muktadha upi?

Nilichokisikia mimi kutoka mdomoni mwa Putin kupitia vyombo vya habari yeye ameiita ni special military operation. Wewe unasema ni vita! Sasa sijaelewa baina ya huyu niliyemsikia na wewe unayeandika yupi ni Putin!?
Nimependa unavyojenga hoja zako.
 
tatizo hapo sio exchange, exchange imekua ikifanyika miaka yote, hapa ni kuwa europe iwe na reserve ya ruble kwajili ya kupay bill za gas, sasa nan yuko tayar kukalia hifadhi ya ruble ambayo leo iko juu kesho chini keshokutwa kati? haifloat free na mengineyo ndio maana ht urusi yenyew imewekeza kwe euro/dollar, issue sio exchange hapa

Mzee baba kasemaje? Ambaye hataki aache sasa mnampangia maamuzi cha nchi yake? Ila bongo [emoji119][emoji119][emoji119]
 
Hizi habari za hali kuwa mbaya wewe umezipata wapi kama hazipatikani kwenye media zao?

Qatar asipowauzia gas Marekani na Ulaya atawauzia nani wenye uwezo wa kumpa pesa anazozitaka?

Waasi wa Yemen kulipua kisima cha mafuta Saudi Arabia ni sawa na kuchota maji kwenye bahari na pipa ukafikiri yamepungua.

Ukiwa mjinga jiupeshe kubwatuka sana, utaaibisha ukoo wenu.
Alokwambia Us ana gas nyingi nani? Na US anareserve kubwa tu ya mafuta sio producer mkubwa wa mafuta. Msidanganywe na west propagandas hali ya Europe kwa sasa ni mbaya sana maisha yako juu hizi hbr huwez pata kwenye media zao.

Gap la Russia kwenye nishat halizibiki kirahis qatar kawatolea nje, huko saudia kuna visima vimelipuliwa ma waasi wa Yemen.

Hii ligi si mlianzisha?? Taifa moja vs mataifa 30 wtf???
 
Kaka hili jambo lipo wazi...Urusi haikuwa na nguvu za kivita ambayo sisi wote tulidhani.

Achana kabisa na nchi za magharibi...yale madude ya kutungukia ndege toa EU ni balaa...Ujerumani jana wamepeleka mengime 1500.

Putin hana namna ni kukubali yaishe.

Ni uamuzi wa busara kwa urusi kuachana na hii vita.
Siyo kweli mkuu, hii operation ya kijeshi urusi angemaliza ndani ya wiki mbili tu, tatizo NATO na USA wameingilia Kati kumpa silaha Ukraine

Hayo makombora 1,500 ambayo ujerumani kampa Ukraine ni makombora ya urusi yaliyobaki ujerumani mashariki baada ya Vita kuu ya dunia,

Na ninavyoona Putin anapoteza muda ili vikwazo walivyoweka NATO viwaume wananchi waanzishe maandamano, Spain madereva wameshaanza kuandamana, huku Saudia mitambo yake ya mafuta inapigwa mabomu, maana yake mifumo ya ulinzi wa makombora wa marekani umeshindwa kufanyakazi,

Kinachofata ni Saudia kupunguza uzalishaji wa mafuta na bei ya mafuta itapanda tegemea machafuko ulaya, ndiyo maana NATO wanatafuta kila sababu wapigane Vita na urusi wapate sababu ya kuwaaambia raia wao kuwa mfumuko wa bei umesababishwa na vita
 
Back
Top Bottom