Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Sijajua source uliyotolea, lakini nahisi hizo silaha 1500 si za WWII itakuwa ni za kisasa kabisa, huwezi mshambulia Russia kwa mabomu ya mwaka 1939, itakuwa ni ujanja wanatumia kuwatuliza wananchi ambao wataona kodi zao zinachezewa hovyo.
 
Mzee wa conspiracy theories
 
Kuendesha vita ni gharama kwa nchi kama marekani na nchi za ulaya,ila sio kwa Urusi maana mifumo ya jeshi inatofautiana sana.
Ina maana hujui kuwa moja ya vitu gharama ni waging a war ? Huko kwengine nisiseme kitu ila kuendesha vita ni gharama sana. Logistics, vifaa n.k

Kwa upande wa kukwama uchumi ngoja waje wataalamu..
 
Kaka umejitahidi, basi nijaribu kujibu kifupi
1. Msaada kwa Ukraine na Urusi: Ujerumani peke yake inatuma Euro milioni 200 KILA SIKU kwenda Urusi. Nii sijui ni mara ngapi usaidizi wa Ujerumani kwa Ukraine. Menginevyo: ukivamia nchi tulivu heri ujiandae vema, ili usihangae kama jirani ana marafiki wengi! (ungeijua KABLA ya kuvamia 😉). Ukipuuza kutafakari na kusikiliza, usilalamike.
2. Kasi ya uvamizi:
itoshe kukumbuka habari za foleni ndefu ya vifaru na malori ya Urusi iliyokaa kwa zaidi ya wiki moja barabarani bila kusogea mbele, ilhali iliendelea kushambuliwa na komandoo wa Ukraine waliobeba makombora ya mbegani. Foleni hii ilionekana kwenye picha za satelaiti zinazopatikana hadharani (mfano Maxar). Kusubiri mahali unapopatikana kwa mashambulio ningeita "polepole". Sawasawa picha za vifaru vilivyoibwa na wakulima Waukraine waliovivuta kwa trekta zao. Si vifaru vilivyoharibika, viliachwa to njiani. Sababu zilizotajwa: vilishiwa mafuta. Mwendo wa kijeshi unaoshindwa kupeleka mafuta kwa mitambo yake naita polepole.
3. Mchezo wa Mig29: ni dhahiri hii ilikuwa mchezo wa kisiasa wa serikali ya Poland iliyotaka kujionyesha kumbe wako kabisa upande wa Ukraine (ilhali Poland inaendelea kutuma pesa Urusi kwa makaa wanayoendelea kupata; angalau gesi wanafunga mwaka huu wameandaa njia mbadala ya karibuni); haikuwa mpango wa kitaalamu. Ukitaka kufanya kitu kama hiki unakifanya bila matangazo. Wwaliitangaza hadharani bila mawasiliano ya awali, walipata jibu kutoka msemaji wa Marekani ambalo lilioekana halikujadiliwa ndani na mwishowe serikali ilisema hapana, hatutafanya. Kwa sababu NATO waliamua kutotafuta mapigano ya moja kwa moja na Jeshi la Kirusi shauri ya hatari ya mgongano ya kinyuklia. Katika kanuni za NATO swali hili litaanza pale ambako Putin anajaribu kuvuka mpaka wowote wa nchi ya NATO.
4. Mamlaka ya kuchora mistari nikisema hoja langu ninayo kabisa.
5. Umoja wa NATO: kaka nenda fanya homework kwanza halafu urudi! Hata baada ya uvamizi wa kwanza wa Urusi mnamo 2014 (Crimea, Luhansk) NATO iligawanyika jinsi ya kujibu. Sehemu ya nchi za NATO (hasa Uingereza, jamhuri za Baltiki ,Poland) zilitaka vikwazo vikali tayari wakati ule. Ujerumani iligoma pamoja na nchi nyingine kama vile Slovakia. Italia, Ugiriki na Hungaria kwa pamoja walikataa kuendeleza vikwazo vya kwanza mnamo 2016. Vilevile rais wa Ucheki. Ujerumani haikusitisha mipango yake ya kuongeza gesi kutoka Urusi kwa njia ya bomba la Nordstream2, ingawa ilikosolewa sana na Marekani na mataifa mengine ya NATO.
Ningeweza kuendelea hapa kutaja mifano, itosh, nimekuweka links za ushuhuda.. Ila sasa kwa ghafla Putin alifaulu kuunda umoja ndani ya NATO na pia nchi za Umoja wa Ulaya. Hakuna aliyepinga vikwazo vilivyoamuliwa ambavyo ni vikali kushinda vyote vilivyowahi kujadiliwa awali.

Tarehe 8 Machi 2012 Urusi ilitangaza "orodha ya nchi ambazo si rafiki" yenye nchi 2 tu: Marekani na Ucheki. Baada ya uvamizi tar. 8 Machi 2022 Putin alitoa orodha mpya ya nchi zisizo rafiki inayoongeza nchi zote za Umoja wa Ulaya, halafu Albania, Andorra, Australia, Uingereza, Iceland, Kanada, Liechtenstein, Mikronesia, Monako, New Zealand, Norwei, Korea Kusini, San Marino, Makedonia Kaskazini, Singapur, Taiwan, Ukraine, Montenegro, Uswisi na Japani.
Tuseme nini ? Alifaulu kujipatia orodha ndefu vile?
Angalau Putin alifauli kubomoa mradi wa Nordstream (uliotetewa sana na chansela Angela Merkel) na kuimarisha nafasi ya Marekani katika Ulaya. Slawa Putin!!!
 
Ukisema imeshindwa,unatuaminisha kuwa vita kwa sasa imeisha kwenye ardhi ya ukraine
 
Kwa tamko hili Vita lazima, na ninachokiona ndiyo njia pekee imebakia Kwa USA na NATO maana mpaka sasa vikwazo vinawaumiza wao, na kuvifuta wanaona aibu Kwa dunia njia pekee ni kumtoa Putin kwenye power Kwa nguvu
Sijajua source uliyotolea, lakini nahisi hizo silaha 1500 si za WWII itakuwa ni za kisasa kabisa, huwezi mshambulia Russia kwa mabomu ya mwaka 1939, itakuwa ni ujanja wanatumia kuwatuliza wananchi ambao wataona kodi zao zinachezewa hovyo.
Mkuu fatilia hiyo, ni mabomu ya urusi hayo na kama nitaiona tena nakuletea link
 
Whisteling in the dark??
Definition of 'whistling in the dark'

phrase [VERB inflects]
If you say that someone is whistling in the dark, you mean that they are trying to remain brave and convince themselves that the situation is not as bad as it seems.
I waited, trying not to feel as if I were whistling in the dark.
(Collins dictionary=
 
Aisee,hii komenti Yako inamaliza Kila kitu.
Nashauri Mod wa jukwaa hili wafunge hii thread ,umemaliza kaka,nasema Tena umemaliza asiekuielewa hatavelewa Tena maishani.
Nashauri komenti itafasiriwe kwa lugha zote na isambazwe Dunia nzima.
Asante kamanda.hakika Tanzania kumbe tunao analyst wazuri TU,wewe ni mmoja wao.
NAMI naongeza Russia moja inapambana na west wote na mercerneries kutoka Dunia nzima.
Viva Russia.
 
Mtaalamu tena!! Haya, ona hali halisi:

Natural Gas Production by Country​


#CountryYearly Gas Production
(MMcf)
1United States32,914,647,000
2Russia22,728,734,000
3Iran9,097,956,245
4Canada6,751,698,275
5Algeria6,491,744,560
6Qatar6,000,936,690
7Norway5,763,408,000
8China4,559,625,595
9Saudi Arabia4,231,796,450
10United Arab Emirates3,178,738,465
11Indonesia3,143,035,000
12Nigeria3,009,650,245
13Turkmenistan2,910,379,780
14Venezuela2,832,121,740
15Malaysia2,762,798,395
16Australia2,384,327,540
17Mexico2,336,370,000
18Uzbekistan2,037,675,500
19Netherlands1,909,128,900
20Egypt1,742,018,320
 
🤣
🤣🤣
 
nato gani hao nato iliopokea kipondo afghanistan miaka 20 kisha ikakimbia? Alafu wewe mmatumbi wa buza tangu lini ukawa mrusi? ha ha ha ha

Afghanistan miaka 20 mkichokoza mrusi si mtageuzwa mariupol nyingine
 
Nini kinaendelea huko tuambieni
Acha uvivu mzee changamsha obulongata .....ukitaka watu wakuletee watakuletea wanayoyapenda wao...[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]...ingia guugo utuletee ulichokiona wewe kinatufaa tujifunze jambo kutoka kwako ...kilicho cha tofauti na wengine....[emoji5][emoji5]
 
 
Babako akikwambia urudi saa 12 jioni nyumbani wewe unaweza kumjibu kwamba kwa nini yeye anarudi saa sita usiku ?

Kifupi Urusi kashachapwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…