Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LoL jeshi la Urusi ni jeshi la kiungwana kabisa.
Safi kabisa
 

Biden publicly calls Putin "a Butcher," and later in a speech he says ''for God's sake this man cannot remain in power"​


In the most extraordinary display of gross ineptitude, diplomatic malfeasance, and Presidential lack of judgment, illegitimate U.S. President Joe Biden today called Russian Federation President Vladimir Putin "a butcher."

As if that wasn't bad enough, Biden later gave a speech in which he ended by saying (of Putin), "For God's sake, this man cannot remain in power."

What is the world to make of these grotesque statements? Is regime-change in Russia now official US Government Policy?
Moreover, let's talk facts: for eight years, Ukrainian Presidents Porochencko and Zelensky waged actual war against Russian-speaking Ukrainians in Luhansk and Donetsk. That warfare killed 13,000 to 14,000 citizens of Donetsk and Luhansk. Are they called "Butchers?" No.But somehow, Russian President Vladimir Putin, who met his responsibility to protect, is called "a Butcher" for putting and end to Ukraine slaughtering people in Donetsk and Luhansk!
President Joe Biden is clearly out of touch with reality, and severely unable to discharge the duties of his office. No President of a nuclear power has EVER referred to the President of another nuclear power in such terms, nor has any US President EVER called for regime change in another nuclear power. These occurrences are utterly astonishing.
Biden should be removed from Office by Congress via the 25th Amendment to the US Constitution, immediately before his ignorant, dementia-addled mouth gets us into a nuclear war.
 
Usijifanye mjuaji

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora kujifanya mjuaji katika kitu unacho kijua ,kuliko kujifanya mjuaji kwa vitu usivyo vijua utaonekana kituko.

Yeye ameniuliza eti Qtaar asipo muuzia Ulaya na Marekani atamuuzia nani?
Kwa maana hiyo alikuwa hajui ya kwamba asilia kubwa ya gesi ya Qtaar inauzwa barani Asia na sio Ulaya.

Trump aliiwekea vikwazo vya mafuta Iran na wana siasa wa nchi za magharibi wakawa wanasema eti Iran itaanguka na kusambaratika ndani ya mwaka lakini sasa hivi ni mwaka wa 5 Iran inadunda tu.
 
1. Kuifananisha kijeshi Urusi ya sasa inayopigana km 0 kutoka nyumbani kwake na jirani yake Ukraine na USA ya mwaka 1975 iliyokuwa inapigana Vietnam km 14,000 kutoka nyumbani kwake ni ujuha.

2.North Korea haikushinda vita na South Korea. North na South Korea ziligawanya mwaka 1945, Wakomunisti wa North Korea waliivamia South Korea mwaka 1950 wakilazimisha kuifanya nchi moja mwaka 1953 walirudishwa nchini kwao na mpaka ulirudishwa ulipokuwa mwaka 1945.

3.Marekani ni kweli aliiharibu Vietnam ila na yeye alikipata cha moto, alipoteza wanajeshi elfu hamsini, Russia pia ameshapoteza wanajeshi 10,000 na majenerali 7 kwa kipindi cha mwezi mmoja tu na uchumi wake unazidi kudorora haya madhara yatakuwa ya muda mrefu. Ni uongo kusema Ukraine pekee ndiye atapoteza
 
Mtazamo wako...Putin kairudisha nyuma sana nchi yake kiuchumi...
Kama.. wewe ulivyorudisha familia yenu nyuma .... niwashauri tu mhamie kwetu mama yako ntamheshimu ...wamekuwa kama mbuzi wanakula majani tu... Jumatatu mchicha, jumanne matembele, jumatano mnavu, alhamis sukuma wiki, ijumaa kabichi, jumamosi chinizi, jumapili kisamvu ....
 
Kuna mambo hata hayahitaji maelezo yapo wazi. Upo sahihi kuwa kusema Ukraine pekee ndiye atapoteza ni uongo.
 
Da! ila kusema kweli Vladimir Putin ni pasua kichwa kwa nchi za west.

Hawa west kitu ambacho wamebakiza ni kujaribu "kumroga" TU bwana Putin.

Kawafukuza Syria,
Kamtuliza kubwa la maadui Yankee huko Venezuela,

Kawadhibiti Ukraine.

Putin kweli kawa put in ma west.
 
Kuwa na production kubwa sio kuwa na reserve kubwa anachofanya US anachukua huku na huku ndomana anaonekana anaproduction kubwa, tunazungumzia reserve kubwa WW

View attachment 2165503
Inabidi nianzishe darasa la statistics..

Watu hamjui kabisa kusoma data..

Sikia production maana yake you change a raw material au you extract it from its raw product into a usable form..

Reserve ni akiba ulioyonayo now na baadae, hata sisi na Msumbiji we have very big proven reserve ya Natural gas tunaweza kuwa kwenye Kundi la watu wenye reserve kubwa Africa.

Consumption ni matumizi ya end product ya siku na siku, mfano sisi tunayo natural gas but hatuna viwanda vya kuibadili kuwa LPG so tunaagaiza, pia tunatumia kiasi kidogo sana Kwa ajili ya kuzalisha umeme.

USA na CHINA ni top consumers na top producers sababu wanamatumizi makubwa sababu ya wingi wa viwanda na vitu vinavyotumia Hydrocarbons, wanatumia vyanzo vya ndani na nje, Marekani, Ulaya, tuweke na India wasiponunua Mafuta/Gesi Yako Maana yake more than 20-50% ya Mauzo yako yatapungua na kuua Biashara kwa ujumla, so nishati zinazotoka nje ya nchi zinakuwa cheaper kuliko za ndani ili kushindana na Uzalishaji wa ndani.

Nadhani wote tumesikia Juzi Russia imetoa punguzo la bei kwa India, then will be kwa China na wengi tu wanafata
 
Wewe ni mshabiki kumbe! Wenyewe Urusi wamekiri kupateza askari wewe hujui!! Na vikwazo pia hujui! ...
Ewaaa!

Unarudi kule kule pa awali na pengine penye asili yako.

Unalazimisha mawazo yako au unachokiamini wewe kiwe ukweli mtupu kwa wengine. Ukihojiwa unaleta visingizio ili kuifukia mada na unafanya makusudi.

Sasa umejibu nisichokuuliza, nilochokuuliza hujajibu.

Tuambie hiyo ya kusema wamepotoza askari wengi sana tuambie ni askari wangapi Russia imepoteza ambayo wewe ndiyo unayosema ni wengi?
 
Siko tayari kwenda back and forth na wewe kwa majibu yako ambayo (naona) hayatoshelezi kujibu mswala nliyokuuliza. Ni ama umechagua kutokujibu 'dodge' au umeshindwa kutoa majibu murua kutetea hoja zako za awali, vyovyote itavyokuwa ningekushari unapotoa hoja kutokana na 'opinions' zako ni kheri udhihirishe kbs kwamba hayo ni maoni yako tu na sio kuweka kama 'facts'. Hakuna atakayekulaumu kutoa maoni ila utalaumiwa ukitoa 'facts' zilizopikwa.



Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Sasa mbona tunaambiwa moscow inaretreat tena!?

Urusi wanaonesha ni watu tofayti kbs. Ingekuwa nchi nyingine hapo ingeshawaua hao waliosarenda

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Umeandika mengi lakini mzizi haswa wa mantiki ya maandishi yangu hujauelewa.

NK walirudishwa nyuma sana na majeshi ya nchi 21 yakiongozwa na US ikafika mahala mabomu mengine yakawa yanaangukia China.

Nguvu ya msaada wa kijeshi aliyopatiwa NK ni kuwa China aliingiza jeshi la ardhini huku Soviet wakapeleka ndege jeshi angani. Yaani; China mashambulizi yao ni ya chini na Soviet mashambulizi yao yakawa yanafanywa kutokea angani. Hili likasaidia kusogeza mipaka mpaka walipofikia maamuzi ya kukaa mezani na kuepusha vita.

Hoja hapa ilikuwa wapi?
Hoja hapa ni kuwa NKorea ilishindwa kupigana na Taifa kubwa lililoingia na nchi nyengine 20 kupambana dhidi yake na kurudishwa nyuma. Msaada aliyopatiwa NK ndiyo uliyomsaidia naye kusonga mbele na kuongeza kilometers za mraba mpaka wakafikia eneo kwa leo hii ndiyo mpaka wa ardhi baina ya NK na SK. NK haikushinda vita! Ila kitendo cha kurudishwa nyuma kisha wakaweza tena kusonga mbele kinatafsirika kama ushindi.

Ijapokuwa NK aliweza kurudisha na kupata kilometers za mraba lakini kilichotokea ni nini kwa upande wao? Hasara ambayo ni kubwa sana! Nchi ilibakia kuwa gofu na raia wengi walikufa. Halikadhalika kwa Vietnam vilevile. Kwa maana: Angalia hasara aliyoifanya US kwa Vietnam; ijapokuwa alishindwa hiyo vita Ila uharibifu aliyouacha ni mkubwa sana kwa kuanza na miundombinu ya nchi, majengo au makazi ya watu kwani US waliua raia wengi sana.

Nukta hapa usiiangalie tu kuwa US alikipata cha moto. Nukta hapa angalia na upande wa pili walipata hasara kwa kiasi gani? Hasara ilikuwa kubwa sana kwa Vietnam pia. Na hii ndiyo hekima ya historia inatuthibitishia: Ukipambana na Taifa kubwa, hata ikiwa umemuonyesha joto atakachokifanya kwenye nchi yako ni kukufanyia uharibifu mkubwa mno!

Kwa tafsiri nyengine: Tanzania kivita ina uwezo wa kuipiga Rwanda. Lakini Rwanda ina uwezo wa kuiachia Tanzania hasara kubwa sana kwani inaweza ku- target na kupiga sehemu zenye manufaa makubwa Tanzania na kuisababishia hasara kubwa Tanzania ijapokuwa Tanzania itashinda vita. Na kinyume chake ndiyo vivyo hivyo kama maelezo yangu ya juu yanavyosadifu.

Kingine unadai Russia wameshapoteza askari 10,000 hizi data umezitolea wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…