Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

NDo nikakuambia inahitajila muda ili tueleweshane dada yangu.
Baba au mama kumchapa mtoto sio kwamba hampendi.
Hata kwenye familia zetu Huwa inatokea mzazi wakazozana na mtoto inafikia hata hatua ya kutozikan,hii Dunia Ina mambo mengi sana dada.
Putin ni mtu muungwana sana narudia Tena na Tena kukuambia.
Ila inahitaji darasa refu.
Any way kama tunaona mzozo huu kama ushabiki wa Simba na yanga Mimi Sina la kukuambia.
Mkuu mfano wako ni batili Russia na Ukraine siyo kama baba na Mama...maana ukisema hivyo Utahalalisha Ubabe wa US,Israel,Saudi Arabia ,China etc...
Vita haijawahi kuwa Kitu kizuri hats siku moja(vita ni uharibifu na Mauaji)
*kwa MTU mwenye hekima.
 
Ukraine sio Adui wa Urusi dada yangu,amini nakuambia,Hawa ni ndugu wa damu kabisa .
Mchawi hapa ni USA TU,ndio mchonganishi.
Anachokifanya Urusi kwa Ukraine ni kama baba au mama kumchapa mtoto wake,au kaka kumpiga mdogo wake ikiwa atakua ame misbehave.
Hii IPO hata kwenye familia.
Adui wa Urusi ni mmoja TU, USA.hata Hawa EUROPEAN wanapelekeshwa TU na USA kugombana na Urusi .
Ndio maana unaona miradi ya Gesi na mafuta wanafanya sana EU na Russia.
USA hapendi miradi hii istawibkwa sababu Urusi anafaiduka sana kiuchumi hivyo kumwezesha kutengeneza masilaha ya Hali ya juu kama hayo. Na hii ndio chuki ya USA ilipo.
Jombaa unajisumbua kujielezea kwa huyo dada .....hapo ameziba maskio hata hakuelewi ....we utaona majibu yake ya kipro america ...
 
New mechanisms for paying for Russian gas in rubles will not begin to operate from March 31, this is a time-consuming process, said Dmitry Peskov, press secretary of the Russian President.
Galip SV Liwagu View attachment 2169199
Baada ya kuona EU wamemkazia kulipa Kwa ruble kaamua kuback down,watu tulisema humu hiyo kitu itakua ngumu tukaishia kutukanwa matusi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hata Mimi geologist naweza kuchaguliwa kuwa waziri wa Mambo ya nchi za nje kweli?wakiwachagua Nyie wenye fani za siasa inatosha!
Kwangu Mimi kukiwa na amani duniani na uchumi imara inatosha...S
Ungejua wewe jinsi ulivyo juu kwenye geopolitics basi tuu.kumbuka uko Dada peke Yako kwenye mtanange huu na unatoa hoja mujarabu kabisa.
Uko peke Yako kama kitoto Cha mwisho pekee Cha kike katika familia ya watoto madume 11.
Na wote tunakusikiliza na kukuheshimu,na kwa kujua hili unadeka.

Shida Yako ni moja TU hutaki kukubali kama USA ndio mchonganishi wa mgogoro huu. Na hapa ndio pahahitaji darasa kubwa.
Ni kama vile kumgeuza Mwislamu kuwa mlokole.au kinyume chake.
 
Dada yangu acha kufananisha maisha ya kusadikika na maisha halisi, katika maisha halisi ni mwenye nguvu mpishe.

Katika maisha yako ya kila siku jifunze kukaa mbali na maslahi ya wenye nguvu tofauti na hapo yata kukuta ya kukuta.

Mwenye nguvu siku zote linapo kuja suala la kuitetea maslahi yake hayo masuala ya taifa uhuru,sijui sheria za kimataifa ,sijui haki za binadamu ni takataka mbele yake.

Na hiyo ndiyo kanuni inayo iongoza dunia tangu kuumbwa kwake na ndiyo ikayo ongoza mpaka mwisho wake.

Hata ww hapo kama ujipendi au huipendi familia yako jaribu kucheza au kuhatarisha maslahi ya wenye nguvu.
Sasa nimekuelewa mkuu ...ila kwa majibu yako haya Vila shaka sitokuta ukilalamika kuhusu ubabe wa USA,Israel ,China and others.
Vizuri kwa kuwa wazi!
 
Ungejua wewe jinsi ulivyo juu kwenye geopolitics basi tuu.kumbuka uko Dada peke Yako kwenye mtanange huu na unatoa hoja mujarabu kabisa.
Uko peke Yako kama kitoto Cha mwisho pekee Cha kike katika familia ya watoto madume 11.
Na wote tunakusikiliza na kukuheshimu,na kwa kujua hili unadeka.

Shida Yako ni moja TU hutaki kukubali kama USA ndio mchonganishi wa mgogoro huu. Na hapa ndio pahahitaji darasa kubwa.
Ni kama vile kumgeuza Mwislamu kuwa mlokole.au kinyume chake.
Nyie hamnielewi,Naamini mchonganishi Ni USA Mimi nataka Russia achapane na USA.
 
Mkuu unajibu points zangu kwa urahisi sana siyo deep..
Unajua kuwa wakati Putin alisema utawala wa Kiev umevamiwa na wauza unga.Akimaanisha Ukraine IPO kwenye mikono ya watu wabaya(wasio upande wake) akimaanisha tokea ile Euromaidan .Na utakumbuka hata chokochoko hizi zimeshika kasi tangia 2014 na has a baada ya ishu ya Crimea.
Ukweli ni kwamba hayupo radhi na utawala ule wa sasa kutokana na anajua haupo upande wake.anachojaribu kufanya ni bora ya nusu Shari kuliko Shari kamili.
Ukija kwenye conditions Ukraine nae ana zake ...jaribu kufuatilia .
Uharibifu kwenye vita ni jabo lisiloepukika rejea vita zote(Korean war,Vietnam war,Iraq invasion ,Isreal-Arab war etc) unachuangalia ni malengo makuu ya vita yametimia(yanaweza kuwa zaidi ya moja) .
Mfano malengo kuu LA vita ya sasa ni;

1,Kubadili utawala na kuweka kibaraka(hii itafanya malengo mengine yaenge smoothly)
2,Kuizuia Ukraine isijiunge na NATO hata EU( kabla ya vita) kumbka situation inaweza ukabadili au ku-modify malengo.
3,kuchukua majimbo mawili au ikiwezekana kuidesolve kabisa Ukraine..rejea lugha walizokuwa wakionge viongozi wa Russia kuwa Ukraine imeundwa na Russia (kwenye baadhi ya vifaru vyao nilikuwa na Bendera za USSR)
4,kuikalia kimabavu Ukraine ..
5,kulidhoofisha jeshi lake na kulifaya liwe dhaifu(demilitarization)
#kumbuka baada ya maendeleo ya vita ndio yamefanya Russia na Ukraine ku-change na ku-midify baadhi ya malengo yao...mfano Ukraine baada ya maafa na uharibifu amekubali kutojiunga na NATO ,kwa upande wa Russia baada ya kuona Regime change ni ngumu kutokana na Wananchi kushikamana na Serikali yao na Upinzani wa kijeshi aliokutana nao unlike ule wa Crimea(casualties in military personnel na vifaa) na gharama za vita kutokana na vita kuprolong so kaamua. Utawala uendelee ila baadhi ya matkwa yake yafuatwe ikiwemo ilo LA NATO ambalo pimekubaliwa naCrimea +Donbass,Demilitarization ambayo bado hayajakubaliwa.

Mkuu unapoangalia jambo ushabiki na upenzi weka pembeni utakuwa unafanya uchanganuzi mzuri
Kwanza kabisa nisiwe mnafiq I Stand With PUT IN ila kwenye masuala haya tukiamua kujadili kama haya hua tunaangalia kwa facts kabisa tunaeka ushabiki pembeni nandio nnalolifanya
-huko juu nilikwambia kabisa kwamba sababu ya RUSSIA kuingia UKRAINE sababu yakimsingi nikutokujiunga na NATO na wala sio EU kama uliposema hapo juu nandio maana kwenye makubaliano takwa lakujiunga EU kina RUSSIA hawakulipinga sababu EU ni Muungano wakiuchumi wala sio kijeshi na khofu ya RUSSIA sio KIUCHUMI ni KIJESHI nandio maana anaipinga UKRAINE isiingie NATO nasio EU
-PUT IN alisems utawala wa UKRAINE umevamiwa na wauza unga hili nishakwambia huko juu halina tofauti na lililofanywa kwa SADDAM na IRAQ walipo ambiwa kua wanasilaha zamaangamizi kwaupande wako jiulize ZELENSKY nasirikali yake kweli wanauza unga ama walikua wanatafutiwa sababu wakumbane na walichokumbana nacho na kuhusiana na suala la CRIMEA nahisi hili RUSSIA aliishamalizana nalo tokea 2014 now anadeal na DONESTK na LUHANSK n.k
-UKRAINE kweli anaweza akawa na term zake ila hizo term hazina maslahi kwake kama ilivyo kwa RUSSIA mfano wakat vita inaanza ZELENSKY alikua anasema kwamva wao taifa huru wanahaki yakujiunga na taasisi waitakayo ikiwemo NATO kujikinga dhidi ya RUSSIA leo tayari hajiungi na NATO faida kwa RUSSIA
Malengo kama unavyosema yote ama mengi yamefikiwa kwa %kubwa nandio maana nakwambia UKRAINE kapoteza kwenye hii VITA
Tayari UKRAINE imekaliwa kijeshi since day one vita zilipoanza maana tunaona majeshi ya PUT IN ndani ya UKRAINE
Tayari UKRAINE hatakaa ajiunge na NATO kuhusiana na EU hii haikua kipaombele cha RUSSIA kwa UKRAINE
Tayari majimbo hayo unayoyasema kwa asilimia kadhaa ama mia yapo chini ya RUSSIA na hayatarudi tena labda vizuke vita huko mbeleni
Tayari UKRAINE ipo dhoofu kabisa kwenye masuala ya kijeshi mwezi mmoja kabla na baada ya vita UKRAINE nitofauti kabisaaa
Vita kufa watu kawaida na miundo mbinu kawaida ila ndio hasara zenyewe ama kushindwa kwenyewe kunatokea humo humo MKUU
UKRAINE itakua kama SYRIA tunaona AK ASSAD yupo madarakani ila bado kuna maeneo yapo chini ya majeshi ya US pia usitegemee kama UKRAINE itakua tena stable kama awali sababu baada ya kutwaliwa CRIMEA 2014 Maeneo mengine hayakutulia na bado maeneo mengine baada ya hii vita hayatatulia na majeshi ya RUSSIA hayataondoka yote kama SYRIA na US
Kwampaka hapa UKRAINE ndio kapoteza karejeshwa nyuma kimaendeleo miaka kadhaa
 
Sasa nimekuelewa mkuu ...ila kwa majibu yako haya Vila shaka sitokuta ukilalamika kuhusu ubabe wa USA,Israel ,China and others.
Vizuri kwa kuwa wazi!
Mkuu suala la kulalamika ni kawaida ya mwana damu lakini kulalimika halijawahi kubadilisha chochote.
Kila siku watu wanalalamikia kuhusu vitendo vya Israel dhidi ya wapalestina je ni kipi kilicho badilika?

Hata hapa nchini kwetu kuna mambo ya hovyo na kinyume cha sheria yanayo fanywa na viongozi wetu na watu wanalalamika lakini haijawahi kubadilisha chochote.
Ukraine sio taifa la kwanza kuvamiwa na halitakuwa la mwisho kuvamiwa.
 
IMG_20220330_145237_287.jpg


⚡️It is reported that the first payment for gas in rubles today was made by the "Istituto per le Opere di Religione" - the Vatican Bank, having bought rubles for 10 million euros in the Central Bank⚡️
 
Back
Top Bottom