Kaka ukipenda mantiki, anza kwa kusoma ninachoandika. Sijagusa swali la nchi rafiki au sirafiki, wala sijali.
Putin alitangaza mwanzoni, hao ambao anaita sirafiki wanapaswa kununua gesi kwa rubel.
Ukijaribu kuelewa mantiki yake (iko): wangeendelea kulipa kwa € na $ kwenye akaunti ya GAzprom Ujerumani, basi kuna hatari kwamba hela hizo zinakamatwa baada ya kulipa. Hivyo anataka malipo kwenye akaunti nchini Urusi.
Na kwa sababu pesa yake imeshuka, wametafuta njia za kuimarisha ruble. Pesa inaimarika wakati inatafutwa = kununuliwa. Hapa walitangulia kulazimisha makampuni yote ya Kirusi kubadilisha mapato yao (sehemu kubwa kabisa) kwa rubel. Pia walizuia wawekezaji wa nje kuuza hisia (maana kama wangeuza -ambayo inhekuwa kwa rubel- wangejaribu mara moja kupeleka pesa nyumbani kwa kununua dollar. Pia walibana kwa jumla nafasi za kununua dollar (kwa kuuza rubel). Kwa kusema wanunuzi wa je walipe kwa Rubel, alitaka kuwalazimisha kununua rubel.
Nimeshaandika siku kadhaa iliyopita kwamba kuna mlango wa nyuma katika mpango wake, maana mikataba inasema: gesi itanunuliwa kwa €$. Basi hapa hatumii "kampuni fulani"; malipo yaende kupitia Benki ya Gazprom nchini Urusi ambayo ni benki moja iliyosamehewa bado na EU; bado haiko chini ya vikwazo.
Hivyo mlango wa nyuma ni: makampuni ya EU wanalipa gesi kwenye benki hiyo kwa €$ (jinsi ilivyo kwenye mkataba, na jinsi wanasiasa wa EU wanasema), benki inalipa kampuni ya Gazprom (inayozalisha gesi) kwa rubel.
Kwa namna fulani ni unafiki kidogo pande zote mbili. Maana sasa ni GAzprom Bank inayonunua rubel, badala hao wa EU moja kwa moja.
EU inapata gesi, Putin anapata hela anayohitaji.
Hadi sasa gesi inaendelea, hadi sasa hakuna aliyepeleka rubel kwenye benki.
Putin akitaka kuwachokoza kweli (na kujiumiza) anaweza kukataza benki ya kirusi isipokee tena dollar. Hapa anaweza kujaribu hao wa EU kwenda BEnki Kuu ya Urusi (iliyopo chini ya vikwazo) kinyume cha sheria za EU.
Hatua hii hajachukua bado, Tuone.
Nilivyosema - unafiki kidogo pande zote mbili...