Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Sababu ya kuvamia?
Au hujaelewa nilichoandika? Sijasema urusi hajapigana na nchi nyingine,bali si nchi vamizi wala chokozi(sifa mbili kuu kwa Marekani) anaposhambulia ujue ni majibu au kujilinda

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Sijui kama matusi yanajaa ndani yako hadi lazima zitoke??
BAsi jirani mkubwa au mdogo si tatizo kama wewe si mshenzi ukuionekana unafuata sheria zinazokubaliwa.
Hapo Finland iliweza kuishi na jirani Urusi kwa miaka 70. Baada ya Putin kuonyehsa hajali sheria yoyote wala ahadi wala mikataba Finland inataka sasa kujiunga na NATO. Si kwa sababu ya kutisha au kuvamia Urusi, lakini kwa shabaha kumwonyesha heri asijaribu kushambulia hapa.
Unaona ni kosa lao?
 
Putin asha peleka vyombo mpaka wa Finland vipo pale vinafanya mazoezi, hata Ukrain walianza kwa mazozi baadae mchezo wa kuwindana.
Russia ataichapa finland ikithubutu. Walishaamua vita yani ndio chaguo lao na wakiona usumbufu wanatwanga TSAR bomu.
Watu wanashabikia tu bila kutazama mbele.
 
Tunarudi palepale mkuu. Marekani kuishinda Japan ilikuwa ni speculation ambayo kwa asilimia kubwa Marekani ilikuwa na chance ya kushinda. Urusi kuipiga Ukraine sio ajabu hata kidogo, ndicho kitu tunategemea ila sasa kufikia muda huu performance mbovu na gains chache ndio tunashangaa superpower gani anaperform vibaya kwa jeshi ambalo hata kwenye majeshi 20 yenye nguvu duniani halipo.

Wakati Japan inapigana na Marekani ilikuwa haikosi 5 of the best militaries tena hapo ikiwa na second largest navy. Usilinganishe level za 1930s Japan ambayo that time imetoka kuipiga Imperial Russia, ikaipiga China na kuchukua Manchuria, ikapiga Korea peninsula yote, ikapiga Vietnam na Philippines na visiwa kibao hapo katikati dhidi ya 2020s Ukraine ambayo inapewa silaha mitumba na Poland
 
Unachekesha.

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Inaweza kudhibiti ardhi kwa ndege?
 
Uongo mwingi sana umeandika hapa
1.Gharama za maisha Tanzania zilianza kupanda kwa kasi hata kabla uvamizi wa Urusi haujaanza.

2.Hakuna mtu asiyehusika na usalama kwa tena kwa ngazi za juu anayeweza kujua kiwango kikubwa cha silaha za Tanzania zinatoka wapi. Ila ni vyema ukafahamu radar zilizojengwa kipindi cha magufuli zilizejengwa na kampuni la Kifaransa.

3.Mbolea inayoutumika Tanzania kwa kiwango kikubwa inatoka Morroco.

Tusilishe watu matango pori kijanja.

 
Ubaya hauwi wema kwa kutegemeana na anayeufanya. Ubaya ni ubaya tu. Upingwe.
Nandio hapo nikasema upingwe kote kwapamojaa
Hapa now anapingwa RUSSIA kanakwamba US anaeikalia SYRIA pale yupo MICHIGAN ama HAWAII ila huoni kelele huoni kikwazo
Hushangai au kuuliza !!!??
 
Hizi video mm sizipati hapa. Nisaidie km una link telegram

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Jeshi la Iraq mwaka 2001 lilikuwa na nguvu kubwa sana kuliko hili la Ukraine.
Ila mkuu siku Marekani ikija kuingia vitani na nchi yenye uwezo wa kushambulia hizo meli utakuja kukubaliana na maoni yangu.
Hutoamini ni jinsi ambavyo meli za Marekani zitavyo kuwa zinazimishwa hovyo.
 
Umeongea kitaalamu sana, wengi tunaangalia movies za kivita then tuna relate na uhalisia. Elimu nzuri hii.
 
Kama idea ya kujiunga na NATO ni kitisho kwa nini ujiunge wakati unajua hutaruhusiwa kujiunga na ukilazimisha unageuzwa majivu.
Unafikir wazo la Ukrain kujiunga NATO limewasaidia au limewadidimiza?
Je Finland na Sweden wafuate njia ya Ukrain, unafikiri ni busara?
Je kujiunga NATO ni mawazo ya wananchi au viongozi, kama ni mawazo ya viongozi je Ulaya kuna demokrasia ?
 
Sababu ya kuvamia?
Au hujaelewa nilichoandika? Sijasema urusi hajapigana na nchi nyingine,bali si nchi vamizi wala chokozi(sifa mbili kuu kwa Marekani) anaposhambulia ujue ni majibu au kujilinda

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
Hatuelewani?? Sababu ya uvamizi wa Urusi kutoka Moscow hadi Bahari PAsifiki (kilomita 6000) ilikuwa "kujilinda"???
Uvamizi wa koloni zake za awali katika Asia ya Kati na Kaukazi - kujilinda?
Sababu ya kuvamia nchi za Ujerumani MAshariki, Hungaria, Chekoslovakia - kujilinda??
Sababu ya kuvamia Afghanistan (nilisahau) 1978 - kujilinda???
LAbda useme ilijibu nini Afghanistan? Ilikuwa na hatari gani kutoka Afghanistan?
 
Nijibu swali moja tu: wewe unavyofahamu objectives za Russia kufanya military operation ndani ya Ukraine ni zipi. Kutaja hakuchukui zaidi ya paragraph moja. Baada ya hapo najibu maswali yako
 
Ila mkuu siku Marekani ikija kuingia vitani na nchi yenye uwezo wa kushambulia hizo meli utakuja kukubaliana na maoni yangu.
Hutoamini ni jinsi ambavyo meli za Marekani zitavyo kuwa zinazimishwa hovyo.
Fanya kujaribu kutoa scenario ambapo flagship ya USN flagship itapigwa na kombora la kizembe kama Neptune ambalo Warusi wenyewe walisisitiza haliwezi fanya lolote
 
Katika Finland nimeangalia, ni mabadiliko katika maoni ya wananchi waliolazimisha wanasiasa kubadilika. Sweden nahisi ni vile, si nchi ambako viongozi wana nguvu ya kwenda kinyume ya wananchi.
Wananchi walishangaa jinsi gani mkorofi mmoja anaweza kuingiza nchi yake katika vita na kuleta mauaji. Wameona kama Ukraine ingekuwepo NATO, uvamizi wa Putin usingetokea.
Finland ina historia ndefu kutosimama na upande wowote. Ila kwa siasa hii unahitaji imani fulani kwmaba unaweza kumwamini mwenzako.
Putin amefaulu kubomoa imani hiyo.
 
Russia imeshazivamia Finland na Poland mwaka 1939, Iliivamia Afghanistan 1979, iliivamia Chechnya na kuichukua kabisa mwaka 1999.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…