Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Wee jamaa,
Hivi billion 14 unaijua au unajisemesha TU[emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndo mwongo wameojiwa na video tumeona mpaka kwa rafiki zako BBC.
 
Wewe ndo mwongo wameojiwa na video tumeona mpaka kwa rafiki zako BBC.
Kumbe unaamini kweli Warusi walimkamata jenerali wa Kanada Trevor Cadieu huko Azovstal???
hadi unatumia matusi???
Basi sema:
1) kwa nini Warusi hawakumtangaza (jinsi walivyotangaza wafungwa wengine kutoka nchi za magharibi)???
2) Je kama alikuwa jenerali wa jeshi la Kanada hadi mwanzo wa Aprili - aliwezaje kuingia Azovstal? Maana anaondoka kanada, anasafiri hadi Ulaya (yaani ndege hadi Poland au Uturuki, hakuna ndege tena zinazofika Ukraine), anavuka mpaka kuingia Ukraine, anaelekea Mariupol - anakuta jeshi la Kirusi linalodhibiti mji wa Mariupol isipokuwa eneo dogo la Azovstal - je anapitaje? Anaingiaje ???
3) Alihusika kivipi na maabara ya biolojia kama
a) maishani mwake hakujifunza punje kuhusu habari za biolojia au maabara???

maana utaalamu wake ni kuongoza vikosi vya vifaru, alipofaulu akiwa meja mwaka 2007 huko Afghanistan kiasi kwamba alianza kupanda ngazi haraka na kuwa jenerali.
b) alifika wakati tu mwezi wa Aprili ambako shughuli zote za aina hiyo hazikuweza kutekelezwa tena? Au waliunda maabara hayo tangu mwanzo kwenye vilindi chini ya kiwanda cha feleji???
Basi mtaalamu mkubwa, tuelimishe, utupe mwanga !!!!
 
Vyovyote iwavyo lakini ni lazima wanunue kwa Rubo,
Hatutaki ujinga sisi.
 
Mkataba gani umevunjwa? Ninajua mkataba wa Helsinki wa 1974 ambako Urusi / USSR ilikubaliana na wengine wa Ulaya
1) mipaka ndani ya Ulaya isibadilishwe tena kwa nguvu
2) kila nchi ina haki kuamua yenyewe kama inataka kushirikiana au kutoshirikiana na nchi nyingine.

NATO hakuvamia nchi nyingine za Ulaya. Lakini nchi nyingi ziliogopa Urusi kwa sababu ziliwahi kuvamiwa na Urusi na kuwa koloni au nusukoloni za Urusi. (Kwa nini hakuna anayejua Urusi ilikuwa na himaya kubwa ya ukoloni???). Urusi ilivamia nchi nyingi tangu 1945.

Hivyo nchi nyingi zilizogopa Urusi ziliomba kupokelewa katika NATU na EU. Ni haki yao au hapana?? Je nchi ina haki kupatana wengine umoja wa kuteteana (si kushambulia)??
 
Uwezo wa wanajeshi wa NATO Huwa unapimwa dhidi ya nchi kama Iraq,Libya, Syria na Afghanistan.
Sio Urusi.
Huyo wali nadhani hawajui "Spetsnaz"
Hawa watu wanahofiwa na NATO yote.

Inasemekana Hawa askari wa Urusi ndio askari wanaopata mafunzo magumu,makali,ya hatari na ya kutishia kabisa hapa duniani.

Hawa askari maalumu kabisa wa Urusi wanaogopeka kabisa hapa duniani kwa uwezo wao.

Ni kwamba katika Vijana makini kabisa w a Urusi,mafano 100 wanaoenda kufanya mafunzo ya Hao Spetsnaz,wanaofaulu na kama watano TU,wengine wanafeli na wengine wanakufa wameumia kama vile kuvunjika viungo na ajali nyingine hivyo wanakua unfit.
Putin aliwahi kutamka kua askari kama Hawa Spetsnaz hawapo mahali popote duniani.

Maandishi wa habari mmoja wa west aliwahi kumuuliza Spetsnaz mmoja kuwa.

"Inasemekana ninyi Spetsnaz Huwa hamsikii maumivu kabisa."?

Huyo Spetsnaz kwanza alicheka,kisha akajibu kwa upole kabisa kuwa,

"Hapana sio kwamba Huwa hatusikii maumivu,Bali tumefundishwa kuyavumilia maumivu..

Hawa Spetsnaz nasikia wanawasaka kwa usongo sana Special forces fulani hivi wa Uingereza wamesikia wako Ukraine.
Wamejichanganya na wanajeshi wa Ukraine.
Hao wa UK nasikia nao ni wanyama balaa.
Sasa sijua mara baada ya taarifa zao kuwa wamo Ukraine kuvuja na kusikia kua wanasakwa,sijui kama hawajasepa.
 
Jesus Mlokozi asantt sana kuniletea taarifa ambazo Huwa nazipenda kuliko zote hapa JF kwa Sasa.
Mimi furaha yangu ni kuona silaha za NATO ama zinateketezwa, ama zinakamatwa na watoa huduma wa Urusi.
Hizi ndo habari Huwa napenda.
 
Habari za kuyeketezwa,kuteka, ama kuharibu silaha za USA ama NATO ndio habari zinazonibariki sana katika mzozo huu.
Yaani ni kuwatia hasara TU Hawa wakoloni.
 
Da ila wee jamaa kumbe ni mweupe sana ,ukweli Huwa sisomi komenti zako ila nimeona nijaribu kusoma hii nimegundua kumbe huijui Urusi vizuri.
Nikisema mweupe simaanishi wewe ni mjinga,namaanisha ni mtupu kwenye ufahamu juu ya Urusi.
 
Ameenda kumpa pole mke wa rais. Tena rais aliyechaguliwa na kura nyingi halisi, tofauti na mtu huyu huko Moscow.
Anampa pole ya Nini Sasa wakti hajafiwa,
Hajashindwa vita ,
Wala hajaumia.

Sisi tulitarajia angeenda kumpa hongera kwa ushindi mnono dhidi ya taifa vamizi,

Maana tumekua tukiaminishwa humu kuwa Ukraine wanashinda,na NATO wanawapa silaha Sasa pole ya Nini kwa mtu anaeshinda?
 
Da ila wee jamaa kumbe ni mweupe sana ,ukweli Huwa sisomi komenti zako ila nimeona nijaribu kusoma hii nimegundua kumbe huijui Urusi vizuri.
Nikisema mweupe simaanishi wewe ni mjinga,namaanisha ni mtupu kwenye ufahamu juu ya Urusi.
mkosoe kwa hoja , matusi mwisho fb

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
uvamiz

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…