Taarifa za muda mchache uliopita zinaonyesha hali inazidi kuwa mbaya kwa jeshi la Urusi, kwa sasa ina upungufu mkubwa wa wapiganaji, kutokana na wanajeshi wengi wa Urusi kuuawa kwenye Vita ya Ukraine, hali hiyo imepelekea Bunge la Urusi kujadili mswada utakao waruhusu wazee na Raia wa Kigeni kujiunga na Jeshi kwa ajili ya Vita ya Ukraine. Hii ni fedhea kwa Jeshi la Urusi ambayo inajinasibu kuwa na Jeshi kubwa duniani.
Safari hii lazima Putin Afundishwe adabu na ndo kwaanza mapema kabisa hadi November nazani akili itakuwa imemkaa sawa.
________________________________________
Bunge la Russia linatarajiwa kujadili mswada utakaoruhusu raia wenye umri wa zaidi ya miaka 40 na raia wa kigeni wanaoishi nchini humo wenye umri wa kuanzia miaka 30 kujiunga na jeshi.
Hatua hii ni ya Russia kuimarisha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine, baada ya kupoteza wanajeshi kadhaa katika vita vinavyoendelea.
Taarifa iliyoandikwa kwenye wavuti wa habari za serikali ya Russia, Duma, imesema kwamba hatua hiyo ni ya dharura, inayolenga kutumia ujuzi wa watu wazee wenye uwezo wa kivita.
Kwa sasa, wanajeshi wenye umri wa kati ya miaka 18 na 40 ndio wanaoruhusiwa kujiunga na jeshi la Russia.
Russia imepata pigo kubwa sana kwa kupoteza wanajeshi na silaha katika vita vya siku 86 sasa, ambapo Ukraine umefanikiwa kuwashawishi raia wake kupigana na kupinga uvamizi wa Russia.
Japo Russia imedhibithi Mariupol, imeshindwa kufikia malengo yake katika vita hivyo pamoja na kushindwa kudhibithi Donbas, mashariki mwa Ukraine.
Wakati huo huo, waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu amesema kwamba Russia imeanda kuunda vikosi 12 vya jeshi katika sehemu za magharibi, kwa matayarisho ya kile ametaja kama vitisho vinavyoongezeka katika sehemu hiyo, akisema vinatokana na Finland na Sweden kuomba kuwa wanachama wa NATO.
Chanzo VOA
View attachment 2232267