Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hakuna tatizo mbona hata Ukraine anao wazee vitani? tulia mmetaka vita ndefu sasa mtaipata
 
Labda Putin wa Buza, kwahiyo Ukraine alipotangaza kuwa miaka 18 mpaka 60 wanaume wabaki ulifikiri wanakata vitunguu? vita hii NATO ametaka kuwa iwe ndefu sasa tulia hata Warusi wanao wazee
 
Mdau eeh... Au basi tu (Nimeiga intro yako)

Ni hivi mdau, mie nimependa Galip Vrl alivyopangua hoja. Ni kwa namna hiyo tunapata kujifunza na kupanua uelewa wetu, kua team moja isiwe kigezo cha kukubaliana kila jambo kisa limesemwa na member mwenzetu.

Hatupo kushambuliana wala kubishana hapa bali tupo kuelimishana au sio mdau? So mambo yanapendeza kama hivyo yaani. Itapendeza kama Mr Tyang nae akirudi kupangua hoja za Galip Vrl hakika mjadala utapendeza.

Every truth is perspective but not every perspective is truth. Kila ukweli ni mtazamo lakini sio kila mtazamo ni ukweli.

Umetoa mfano mzuri hapo mdau, MI6, Mossad, Pentagon + CIA na Intelligence nyingine ya mataifa zaidi ya 30 wameshindwa kung'amua mbinu za Putin na nini anataka. Sie tubaki na kile tunachokiona tu mbele yetu.

Ama tukiamua kuelezea ili kutowachanganya watu basi tuseme kwa kutanguliza neno "maoni yangu kwa kile kinachoendelea ni kadha wa kadha".

Maana hapa mwingine ambaye hana uwezo kama wa Galip Vrl wa kutazama mambo kwa kina kalibeba hilo kalipeleka kijiwe cha kahawa kuwaambia Putin anataka kuchukua eneo la mashariki awafanye Ulaya kua tegemezi wake ili kustablize Uchumi wake kitu ambacho na mimi naungana na Galip Vrl kusema si kweli.
 
Putin mwezi wa 3 huu bado unasumbuliwa na Zelensky.

Hebu njoo Tanzania tukupige makamanda waliomchakaza IDD Amin kwa muda mfupi bila kuwasahau M23 kule Congo.
 
Samahani, lakini nakumbuka askari wasio wachache wa Gaddafi walihamia upande wa upinzani. Ona hapa taarifa ya malta times, marubani mawili ya Gaddafi yalipeleka ndege zao Malta baada ya kuamriwa kutupa mabomu Bengazi.
Updated: Libyan fighter jets arrive in Malta
Kulikuwa na majenerali na makanali kama vile Abd el Fattah Yunis, Khalifa Haftar, Suleiman MAhmoudi, El Hariri na wengine waliohamia upande wa upinzani pamoja na sehemu za vikosi vyao.
 
Pro Russia ni hazina ya taifa.
Wewe ni kichwa,"kichwa Kwerikweri"
In Jiwes voice
 
CIA hawafanyagi kazi kindezi na katu hamuwezi kuhisi wapo nyuma ya plotu. Unakijua kisa cha Patrice Lumumba.
Kifupi wanatumia resource za local.
Whatever ila Gadafi alikuwa mwiba kwao na bila wao angekuwepo mpaka leo.
 
Hizo ndege zimepigwa kwenye air combat chap zikashushwa na hizo drone uchwara
 
Yaani hawa jamaa wanatabia kama skirts wanaziba juu chini kuko wazi, sasa hapo kuna umuhimu gani wa vikwazo?????

Kitu pekee kinachowashinda ulaya sasa hivi ni kuona aibu kuomba msamaha Kwa Putin, lakini wanaumia pakubwa
Ha ha haa aisee Pro Russia mma vijineno kwa kukera .
"Tabia za Sketi,imeziba juu chini Iko wazi"
 
Hivi ndiyo vichwa vya Pro-Russia halisi, mahaba zero. Mnachuja ukweli wa kila taarifa mnayoipata haijalishi imetoka kwa nani.

Salute sana Mkuu 🤩👊
Ha ha ha kawaida tu Mkuu...😌

Yah ni kweli, jomba weye unashangaa Pro-Putin kupingana kwenye Issue ya Magu... Mbona hapa kitaaambo tu baadhi CDM wameungana na baadhi ya CCM kusimama upande wa Russia na hao hao baadhi wameungana kusimama upande wa Westerners.

Issue ni huwa ni kufanana kwa mitizamo, kisha kuungana kwa kile kilichopo mbele yenu kwa wakati huo 😂😂😂. Nyote mnavaa surual wa kiume na wa kike lakini haimaanishi kisa wamevaa wote surual basi wana jinsia moja.

Ko kupishana nje ya Russia we enjoy tu jomba.

Yah uko right mkuu, kufunzana na kuelimisha sio kukubalian kwa kila jambo bali kuelekezana kukubaliana kwa mambo yaliyo mengi.

Binafs mahaba sina, ila napenda kutizama vitu au kukaa upande wa vitu vinavyo make sense!

Pale nitakapoambiwa kua
A ni sawa na B,
B ni sawa na C,
C ni sawa na M... Basi nategemea pia kuona A ikiwa sawa na M, Otherwise logically hiyo equation haiko sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…