Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kiev , Kharkiv, Bucha ziko huru sasa dhidi ya vikosi vya wavamizi
Na Biden juzi kasaini mpunga wa dola bilion 40 kusaidia juhudi za vita huko Ukraine. Sasa Putin atajua yeye au Biden nani Kiranja mkuu wa dunia.
 
Kama strateji ya kivita ndiyo hii ya kuwafanya chambo askari wako na vifaa vyako vya kijeshi basi ni strateji ya kijinga kwelikweli. Maana Javelin missiles na Bayraktaar drones ziliwakaanga kwelikweli kama chipsi mayai
 
Mkuu baada ya kupata muda kidogo nimepitia hoja za Galip Vrl na naweza sema nisahihi alichokiongea kutokana na alivyoelewa nilichokiandika ila haikuwa maana yangu niliyo kusudia.

Kwa anaefuatalia mgogoro huu sidhani kama yupo ambae hajui kama kuna Operation mbili ambazo Putin anapambana nazo kwa wakati mmoja.
1. Operation ya kijeshi, hapa nikati ya Russia Vs Ukraine+USA&NATO
2. Operation ya kiuchumi, hapa nikati ya Russia Vs EU&USA
Na Operation zote hizo Urusi alijua kabisa kabla ya kuanza Operation yake uwezekano wa hizo operations kuwepo ni mkubwa na naamini aliweka alternatives na mikakati mapema kabla ya kuanza Operation na ndo maana tunaona namna anavyowapiga EU kwa jiwe moja la uchumi baada ya wao kurusha 100.

na kila anae shiriki mgogoro huu kuna uwezakano mkubwa wa kujua weak points za opponent(s) wake na ndo maana tumeona maeneo mhimu nchini Ukraine ndo moto ukiwaka na mengine kuthibitiwa kwaajili yakuja kutumika kama bargaining matters wakati na baada ya mgogoro kuisha. Mfano; Juzi Urusi imewambia UN&EU bila kuondolewa vikwazo Bandari ya Ukraine hatuifungui kuwasambazieni chakula lasivyo mtakula vikwazo vyenu (Hiyo kwa EU ni weak point)


Kuhusu sababu za Urusi kuivamia Ukraine siyo kwamba nikusudi la Urusi kama Galip Vrl alivyonielewa au kufikiri ndo maana yangu. Bali nilijaribu tu kuonesha Urus ilivyotumia Upenyo wa Ukraine kuleta kelele za NATO kuanza kupambana na adui wake walio nyuma ya Ukraine na kuyatenganisha/kuyakomboa majimbo ya mashariki mwa Ukraine kwa sera ya kuyatambua kama majimbo/nchi huru, ambapo ni reality baada ya kupata huo uhuru lazima yatakuwa loyal kwa Urusi.

Sema nafurahi sana kubadilishana na kueleweshana mawili matatu na wakuu wa Jf hasa Pro-Russia kwenye Uzi huu na Pro-NATO wanaopenda kujadili hoja na siyo propaganda za BiBiSi, naamini hata Putin angekuwa anatumia JF basi angedhani Tanzania kuna jimbo la Urusi lenye warusi wazawa wanaoijua vizuri Russia.
Hongeren sana kwenu Pro-Russia[emoji120]
Safi sana Pro Russia ,hoja zinajibiwa kwa hoja.
Kwa kifupi watu wote tunaofatilia mgogoro huu Kila mtu ana Mtazamo wake.
Hata wale ambao wako upande mmoja lakini Kuna mambo Kila mtu anapata Mtazamo wake.
Na mwisho wa siku watu tunafikia conclusion.
Tuendelee kushusha nondo.
 
na kyiv mlienda kuwachukua wanaozungumza lugha yenu pendwa ?
Ha ha ha haaaa! Si umetaka tuchangie uzi huu kishabiki, sawa tuendelee!!!
====
Ile Kwenda Kiev ilikuwa Kanyaboya ili wakajishindilie kwenye maandaki Mariopol... mtego uliponasa tukaenda kuwanasa, kama ulivyoona juzi kwenye tv na mitandao.
 
Vita ni mbinu sio kuwa na silaha mpya au za zamani[emoji28]!

Hata ukipewa shehena ya AK 47 kama huna mbinu kipigo kitakuhusu tu. Hao si wamepewa Javelin mlizosema ni anti tanks mbona sahizi kimya wakati mlisema wanaharibu vifaru vya mrusi kama biskuti.
Wambie Ak-47 ndio iliyo ikimbiza Marekani na mashoga zake nchini Afghanistan na Somalia.
 
wakuu ila tukiacha ushabiki wa pro-max tukarudi kwenye uhalisia basi kwa pamoja tutasema Putin ni Kichwa haswaa. Kuendesha operation zote mbili(kijeshi na kiuchumi) kwa mpigo against nchi zaidi ya 30+ zenye nguvu na bado unazitoa jasho siyo jambo la kawaida. Sisi wengine kelele za wake zetu tu ndani huwa zinatuvuruga kichwa tunakimbia ndani na kwenda kushinda bar, vijiwen na n.k sembuse makelele ya USA, NATO na EU.

Mzee putin apewe heshima yake haijalishi wewe ni pro-Putin au pro-NATO penye ukweli tusimame pamoja.

Mkuu Mimi hilo nililona mapema sana.
Kuipima nchi au mtu au kikundi uwezo wake ndio mambo kama haya.
Juzi hapa nilitafakari na nikaandika thread moja kuonesha jinsi Urusi ilivyo na nguvu sana katika masuala ya Ujasusi.
Nikisema hivi,Urusi Ina Ujasusi Bora kabisa hapa duniani.
Kwa sababu majasusi wa Urusi wanapambana peke Yao dhidi ya majasusi Bora kabisa kutoka nchi za west na zaidi na bado inawamudu.
Mfano inapambana na mashirika yote ya Ujasusi ya nchi za NATO.
Na washirika wao wa Mossad,Japan, Australia, Korea kusini n.k

Urusi inapamba na Ukraine wakati imewekewa vikwazo na nchi zote tajiri za west.

Inapigana na nchi iliyofundishwa na nchi Bora kabisa kijeshi za west na inapewa misaada kutoka nchi hizo.
Lakini Urusi ikiwa peke yake na ikiwa Iko kwenye vikwazo.

Tofauti na USA akienda kuipiga nchi ndogo TU kama Iraq, Afghanistan,Syria na Libya ni LAZIMA aende na marafiki zake kutoka NATO ,mfano Ufaransa na uingereza.
Hawa ni mataifa yenye Nguvu sana za kijeshi hapa Duniani.

Aisee hiki ni kitu Cha ajabu kabisa.
 
Kutoka Peru wadau wangu.

Songa nayo:
US and NATO finance fakes about Russian special operation in Ukraine - Federation of Journalists of Peru

Latin American journalist Ricardo Sanchez Serra said that the main source of anti-Russian propaganda is the British company PR Network, which supplies Western media with content. This company is fully funded by NATO and the United States, Serra stressed.

“The buildings allegedly destroyed by the Russians in Kyiv were actually filmed in the Gaza Strip. The destruction in the Donbass was attributed to Russia, but in fact they were hit by a Ukrainian Tochka-U missile. They said that the tank that crushed the car was Russian, but it turned out that it was Ukrainian,” Serra said at a conference on the situation in the former Soviet republic, which is published on the website of the Federation of Journalists of Peru.

The journalist also revealed the deception of the European media, which reported on the bombing of cities by the Russian military - in fact, the journalists showed footage from computer games.
 
,” Zelenskyy said, just as Russia claimed its long-range missiles had destroyed a shipment of Western arms destined for Ukraine’s troops.
 
Da kusema kweli Mzee mzima USA safari hii kakutana na mbabe mwenzie.
Yaani Kila Marekani akishusha mzigo wanaume wanaula kichwa.
Aloo Urusi sio congo.
Uzuri wa mrusi anawabinya kende na plaizi taratibu tu wala hana papara. Kila wanalopanga wanakuta jamaa ana mbadala wake😅😅😅 wanaitana tena vikao kama ndugu na mshenga ukweni!
 
Back
Top Bottom