Kuhusu sababu za Urusi kuivamia Ukraine siyo kwamba nikusudi la Urusi kama @Galip Vrl alivyonielewa au kufikiri ndo maana yangu. Bali nilijaribu tu kuonesha Urus ilivyotumia Upenyo wa Ukraine kuleta kelele za NATO kuanza kupambana na adui wake walio nyuma ya Ukraine na kuyatenganisha/kuyakomboa majimbo ya mashariki mwa Ukraine kwa sera ya kuyatambua kama majimbo/nchi huru, ambapo ni reality baada ya kupata huo uhuru lazima yatakuwa loyal kwa Urusi.
Ha ha ha ni kweli jomba ndio maana nikasema kila mtu kuna point anaielewa kulingana na kile alichonacho kichwani.
Kwa mfano mie na baadhi ya wengine tunaona Issue ya Putin kuwawahi ama kujiingiza mwenyewe kwenye mtego aliokuwa anatengenezewa moja wapo ni katika kuivunja unipolarity na kuiweka dunia kwenye multipolarity.
Na hii imekuwa ikitamkwa mara kwa mara na waziri wa mambo ya nje wa Taifa hilo Ladrov.
Na kwa kiasi kikubwa kafanikiwa how? Kama hivi...
1. Kuondoa Imani ya mataifa mengine dhidi ya hizi International community ambazo of course zimekuwa kama fimbo ya kuwanyoosha mataifa mengine.
2. Kawavua nguo mataifa haya ni kudhihilisha yaliyo vifuani mwao hasa kwenye swala la white supremacist. Hawa jamaa ni wabaguzi mno, migogoro mingine inayoendelea duniani wameifumbia macho ila kona ni Ukraine as if pale ndio kuna watu tu kwingine kuna mbuzi na bata.
3. Kuna issue zingine kama usemavyo ngumu kuzielewa mpaka zifanyike, mfano ISSUE ya RUBLE, Nani aliwazs hata kwa bahati mbaya kua Putin na team yake waliwaza kuibomoa dollar 😂 hawapo.
Nani aliwaza hiyo Currency ya Ruble itapewa nguvu na hao hao wanaojikuta viongozi wa dunia kwa kuiongezea demand sokoni? Kupitia basic needs kama nishati?
4. Kawapa Confidence mataifa mengine kua yanaweza kujitegemea na kuishi nje ya Unipolarity, kuishi nje ya WESTERN HEGEMONY. mfano wa hili angalia mataifa yalioanza kumvimbia US baada ya huu mgogoro 🤣
5. Hata US anajua, kwa kunukuu kauli za Biden, kua dunia inaenda kupata New World Order, akiwasisitiza wakurugenzi aliokuwa anazungumza nao kua they should take a lead... Hii inaleta tafsiri ipi... Ni ile ya mapigano kati ya Old World (Westerers) na New World (Easterners).
Na hapa ninaweza sema kua lengo la Westerners (
kutokana na kile nachokiona nje, hapa nisinukuliwe as if ndio malengo ambayo yameandikwa kwenye nyaraka zao) lilikuwa lile ambalo limefail toka awali, mwanzo wa hii OP.
Wanajua hawawezi kupigana directly na Russia. Shida yao kwao ni Putin... Target yao kubwa ilikuwa kuuharibu uchumi wa Russia, ile kufumba na kufumbua kuzua migogoro ya ndani kwa ndani, wananchi wapate hasira waingie barabarani kumpindua Rais wao.
Hii irejee kwenye kauli zao hao viongozi kiaso cha dementia Joe alifikia hatua ya kuzungumza wazi kua PUTIN inabidi aondolewe madarakani. Na hilo pia la kutaka kufanya mapinduzi kupitia ubomoaji wa uchumi PUTIN alilisema mwenywe na akidai westerners wameshindwa katika hilo... 🤗
Na mengineyo zaidi commets isiwe ndefu ikakerrrra...
Sema nafurahi sana kubadilishana na kueleweshana mawili matatu na wakuu wa Jf hasa Pro-Russia kwenye Uzi huu na Pro-NATO wanaopenda kujadili hoja na siyo propaganda za BiBiSi, naamini hata Putin angekuwa anatumia JF basi angedhani Tanzania kuna jimbo la Urusi lenye warusi wazawa wanaoijua vizuri Russia.
Hongeren sana kwenu Pro-Russia
Tuko pamoja jemedari 👊
wakuu ila tukiacha ushabiki wa pro-max tukarudi kwenye uhalisia basi kwa pamoja tutasema Putin ni Kichwa haswaa. Kuendesha operation zote mbili(kijeshi na kiuchumi) kwa mpigo against nchi zaidi ya 30+ zenye nguvu na bado unazitoa jasho siyo jambo la kawaida. Sisi wengine kelele za wake zetu tu ndani huwa zinatuvuruga kichwa tunakimbia ndani na kwenda kushinda bar, vijiwen na n.k sembuse makelele ya USA, NATO na EU.
Mzee putin apewe heshima yake haijalishi wewe ni pro-Putin au pro-NATO penye ukweli tusimame pamoja.
Hapo ndipo utaona power ya Uzalendo dadeki... Inabidi tuwape pongezi pia warusi wote (hapa nalenga Raia sio Sie ma Pro) kwa utulivu waliouonesha.
Nahisi hili ni jambo kubwa ambalo tunapaswa tulione pia... Wananchi wa Russia kipindi kama hiki wamejionesha wako pamoja than before, indicator ya kuthibitisha hii kauli angalia kwenye Approval rate ya Putin kabla na baada ya Special OP.
Trust juu yake imeongezeka, pembeni anazungukwa na team makini so mipango nayo yaja imenyooka. Kila kitu bam bam 🤣🤣🤣
Mwisho nimesahau, kuna Post zile za mwanzo kuna hoja kama maswali hivi uliyatoa jana nilikuwa na usingizi nikayapitia juu juu tu😂... Ukipata mda anzisha ule uzi unaosema af tutajadiliana huko taratibu moja baada ya lingine... Usisahau kututag tu.