Mwamba leo hujajitendea haki kabisa, naona mengi umeyazungumza kihisia kuliko uhalisia. Unachojaribu kukionesha ni kama westerners wanao jaribu kum'demonise Russia. Na kumfanya Ukraine mtakatifu.
Na ufatiliaji wangu wote wa Geopolitics, sijawah mnasa Russia akifanya ujangili wa namna hiyo.
Maelezo yako yanataka kutwambia hivi
1. Issue ya Donbas ni ya kupangwa na Putin iwe kama ticket kwake ya kuingilia Ukrane kwenda kuiba ilo eneo.
2. Pili ni kumhusisha Putin katika njama za mauaji ya hao Raia 14,000 wa Ukraine wenye asili ya Urusi katika maandalizi yake ya sababu za kuivamia Ukraine kuiba eneo.
3. Unajaribu kutuambia hawa Azov pia ni mipango ya Putin katika kuwatengeneza kama sababu ya yeye kuingia hapo Ukraine kuiba hayo maeneo ili kuwafanya EU kuwa tegemezi kwake.
Tuanze hapa, kama sio NATO unaizungumziaje hii... Unataka kutwambia kwamba alitumwa na Putin amtengenezee mazingira?
View attachment 2232980
Una data za kutosha kuhusu dai hili? Unaweza kutwambia kiasi gani uchumi wa Russia kua imara unategemea EU kua tegemezi kwake? Je chakula alone na Gas kinatosha kua worth a trillion dollar economy?
Umefanya tafiti vizuri? If Ukraine is that important to EU? Unajua sababu za EU kumchinjia baharini huku wakisita sita kumpa uanachama?
Kwa comparison? Unajua kua Gas and Oil iliyogunduliwa hapo Ukraine yeye tu kwa matumizi yake ambayo ni madogo kulinganisha na Nchi nyingi za ulaya haimtoshi, kiasi cha kumlazimu kufanya import kutoka nje tena sio mbali bali Russia. Je ataweza kuiepeleka ulaya?
If that's the case unaeza kutueleza huyu alimaanisha nini dhidi ya Russia? So na huyu pia alipangwa na Putin namna gani amtengenezee mazingira ya kuivamia Ukraine?
View attachment 2232986
Ardhi ya kilimo wanayo ila hawadhalishi kila zao wanalohitaji, na kimbuka sio kila zao linalimwa popote, sawa ma korosho huezi kuta inalimwa Tabora kwa wingi. Africa eneo kubwa liko wazi kwanini tunaagiza chakula kutoka nje? Je kauli yako ya Ukraine kuwalisha EU kwasababu EU hawana mashamba ni sahihi au batili?
Tunarudi tena kuuliza if that's case, unaizungumziaje hii nayo, Hawa wote walikuwa wanapangwa na Putin?
View attachment 2232996
Maandalizi yote ya miaka 8 ya kuwatrain hao Nazi kutoka kwa Pentagon, Hizo Bio Labs zilizoenea hapo Ukraine, Hizo money laundering zilizokuwa zikifanyika Ukraine, Fedha zote walizomwaga US kuanzia kwa Obama, Trump hadi huyu Chizi Joe zote zilipangwa na Putin kama maandalizi ya sababu za kwenda kuiba eneo Ukraine ili kuwafanywa EU wawe tegemezi kwake?
Kama ni Putin wa dizain hiyo unayemzungumzia basi ni Mpuuzi sana. Ambae hakupiga hesab Reactions za EU juu yake dhidi ya Uchumi wake, na namna watakavyoansa harakati za kujitoa mikononi mwake katika harakati zake za yeye kutaka kuwaweka mikononi mwake.
China peke yake anatumia Gas and Oil nyingi kuliko bara zima la EU, so maelezo yako yanajaribu kutueleza kua Russia tunaowaita watu makini ameshindwa kum'convince best yake ndani ya BRICS kufanya biashara matokeo yake kwenda kuiba ardhi Ukraine ili awafanye Europe tegemezi kwake?
Kwamba huyu US anayelazimisha kila mtu amchunie Russia, huku anajiapiza kua atafidia Gap lake kwenye soko la EU yote ni katika Plan za mwamba kuiba eneo Ukraine ili awafanye Ukraine chawa wake hivo kuwatia mfukoni EU?
Kwamba Mwamba akaamua akubali Wawekezaji wote wakimbie nchini kwake, raia wake akose ajira kisa kuiba ardhi ya Ukraine ili EU iwe tegemezi kwake?
No way! Em tuendelee hivi hivi kujieleza kua hakuna ajuaye kiundani target zake zaidi ya zile alizozianisha ya Denazification, Demilitarization, na kuwaokoa Raia wenye asili ya kirusi walio kua wakiuwawa bila wa kuwatetea.
Hizi assumptions haziukaribii ukweli ata kwa bahati mbaya.