Siku nikipata muda nitaanzisha uzi wa malengo makuu ya Russia kwenye hii operation. Najua wengi wanajua ni NATO ila hiyo ilikuwa kama entry gate tu ya putin kuingia na kuanza kukamilisha malengo yake mama kwa masilahi ya nchi na watu wake. Kuhusu kujiunga NATO siyo issue sana kwa Urusi issue ni NATO kuweka millitary bases karibu na mipaka yake, hapo hata uwe Mna NATO kwa miaka 20 Moto utawaka.
Ngoja nigusie tu lengo kubwa la hii operation ya Urusi, lengo kuu lililojificha nyuma ya pazia nikuifanya Ulaya hasa "EU" waendelee kumtegemea Urusi katika kuendesha uchumi na maisha yao ya kila siku, Putin anaamini hiyo ndo njia pekee ya Urusi kubaki imara kiuchumi na kiushawishi.
Je Ukraine anahusika je hapo?; Ukraine ndo nchi pekee huko ulaya inayoelekea kufanana na Urusi kwa suala la Rasilimali na bidhaa za kilimo yani reserve ya mafuta, gas, umeme, mazao na n.k, hivo basi putin alivyoona uhusiano wa Ukraine na watumwa wake wa EU unaelekea kukua hadi kuanza kushirikiana mambo mengi, akastuka ili awa wahi mapema kabla hawajaanza kuweka mitambo yao ya ku utilize oil and gas reserves iliyopo mashariki mwa Ukraine, pili anajua vizuri kabisa "EU" hawana ardhi ya kilimo kama aliyo nayo na Ukraine na anae walisha kila siku ni yeye na Ukraine, kwa hiyo ili abakie kama tegemezi kwao nilazima Ukraine awe underdog kwake.
Sasa basi ili hilo lengo likamilike nilazima yeye au vibaraka wake ndo wawe controller wa hayo maeneo mhimu yanayo windwa na westerners kwa lengo la kujiondoa kwenye utegemezi wa Urusi. na njia pekee iliyokuwepo kufanikisha hilo lengo nikuyachukua hayo maeneo kijeshi maana kisiasa tayari Zelensky alikuwa ashaoelewa na westerners, so Urusi iliona kuendelea kutumia siasa nikuendelea kujimaliza wenyewe. Na ndo maana Tangazo la kwanza kabla ya kuingiza vikosi Ukraine, Putin alitangaza kuyatambua majimbo ya DRP na LRP kama states huru maana ndo target yake na ndo kuna rasilimali nyingi mfanano na za Urusi zinazotegemewa sana na Westerners. Unganisha na Dot za kuyathibit maeneo ya Crimea, Zaporizhzhya nuclear power plant, Mariupol, snake island na Odesa(still on fire)
Naomba niishie hapa, details zaidi zitakuwa kwenye Uzi (nikipata muda mzuri one day) ila Russia yupo tayari kutumia hata nukes ili tu Ukraine mashariki iwe chini yake. Inahitajika akili ya utulivu sana kuelewa plans za Kremlin chini ya Putin maana hata EU, G7,NATO na UN wazielewi kabisa ndo maana kila siku wanaishia kuingizwa choo cha kike tu.
Nawasilisha.
Mkuu, kula tano.
Yaani ni kwasababu tu kwamba tupo JF mtandao ila natamani siku moja tukae kikao tupate kahawa na kashata mjadala makini uendelee.
Kwa kuongezea tu ni kwamba si tu Mr Putin ni strategist bali pia ni tactician yaani mbinu zake ni siri yake mwenyewe na hata bwana Shoigu hustukizwa.
Nilisema humu na nikawaelezea wale mazee waitwa Siloviki ambao wengi ametokea nao ilokuwa KGB .
Hawa wakiongozwa na Nikolai Patrushev ni watu ambao huwezi kuwabadilisha mawazo kuhusu mstakabali wa Russia katika jukwaa la dunia ikiwa ni mmoja wa "super powers".
Hawa wataka Russia iheshimiwe na iogopwe.
Putin kuita hii ni special military operation ni wazi kuwa inajidhihirisha kwa raia wa Russia kwamba usalama wao na taifa la Russia ni lazima uwe kwa kuhakikisha Ukraine haiwi kichaka cha NATO.
Wao waamini kuwa Marekani anaitumia Ukraine (proxy war) kutaka kuiharibu Russia na kuondoa utawala wake yaani "regime change" na kisha kuchukua rasilimali ulozieleza.
Patrushev ambae ni mwenyekiti wa baraza la Usalama aliwahi kunukuliwa mwaka 2015 akiliambia gazeti la Kommersant kwamba Marekani ingependa kuona Russia kama taifa halipo kabisa.
Juzi wametoa orodha ya watu ambao Russia inaamini kuwa ni majasusi wa nchi za Magharibi na kwenye orodha hiyo wamo Boris Berezovsky na Alexei Navalyn.
Petrushev ni jasusi mahiri sana na mwaka 2016 anadaiwa kushiriki mkakati wa kuhakikisha Montenegro haijiungi NATO katika nchi za Balcans na kukafanyika mapinduzi.
Kisha kuna mazee aitwae Sergei Naryshkin ambae ndio aongoza idara ya ujasusi wa nje yaitwa SVR ambayo hucheza kama mdogo wake KGB ambayo kwa sasa yaitwa FSB ambayo ujasusi wake ni wa jumla yaani ndani na nje ya Russia.
Naryshkin alifanya mafunzo pamoja na Putin enzi zao na yeye akatupwa Brussels huku Putin akiachwa Dresden Ujerumani mashariki kuchunguza wageni wote wanoingia Ujerumani.
Na mwisho kuna Sergei Shoigu ambae huenda kuwinda maporini pamoja na Putin na hupigwa picha pamoja. Shoigu ni waziri wa Ulinzi . Huyu si mwanajeshi lakini ndie aliefanikisha kuchukuliwa kwa Crimea mwaka 2014 na Russia kuingia Syria mwaka 2015 bila kupingwa. Shoigu humwambii chochote kuhusu suala la "Maslahi ya Taifa".
Na bila kumsahau mzee Sergei Lavrov ambae ni waziri wa mambo ya nje tangu 2004!, utamwambia nini mwanadiplomasia nguli huyu?
Huyu mzee amekuwa akijaribu bila mafanikio kustaafu lakini Putin amekuwa akimkatalia kwa sababu ya uzoefu wake na ndie msemaji wake mkuu.
Jambo la kijifunza hapo ni kwamba rasilimali na maslahi ya taifa hutakiwa huenda pamoja na ukipata viongozi wanojitambua na kutambua umuhimu wa masuala haya mawili basi mstakabali wa taifa kimaendeleo husimama imara.
Jambo jingine ni mkakati wa kitaifa, malengo na maono ya taifa ambayo kutegemea ujasusi wa hali ya juu kuhakikisha taifa haliyumbi wala kuyumbishwa khasa pale taifa hilo linokuwa na rasilimali za kudumu ambazo huweza kutumika kuliendeleza taifa hilo.
Mwisho ni kuhusu ujasusi kwamba ni sanaa ya taifa zima yaani "statecraft" katika kutumia uwezo wa kiakili masuala kama mipango ya maendeleo, sera ya nje na uhusiano wa kimataifa. Yaani sio tuambiwe umuhimu wa ziara za raisi nje ya nchi lakini yaje magazeti ya hukohuko nje yakebehi ziara hizo kwa kuangalia namna tunojidhalilisha kwa matumizi ya kodi na rasilimali za nchi.