Galip Veryl
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 2,147
- 13,463
Ahsante, 🤩🤩🤩Da Pro Russia Kuna kitu nimejifunza.
Kwa mijadala kama hii,kwa nondo hizi mnazozitoa,aisee Kuna jambo la kitabiabama sijui niseme kisaikolojia nimejifunza .
Sijui kama ntaeleza vizuri.
Kumbe mtu kuamua kuchagua ama. Kujikuta uko upande Gani Ni suala la kitabia na kimaumbile zaidi.
Kwa jinsi ulivyo hangia hapa,kwa kuchangia ama kujibu hoja ya mdau najinsi Pro Russia wengi wanavyochangia na jinsi Pro USA wengi wanavyochangia nimegundua kwamba.
USA na west ni nchi zenye majivuno,dharau,kiburi,jeuri,matumiazi ya nguvu na mengineyo.
Hivyo hata Mashabiki wake wengi wanapenda tabia hizo.
Ndo mana utaona USA hata maamuzi yake mengi ni kama nilivoorodhesha.
Kupenda aonekane ana nguvu ama za kijeshi na kiuchumi,maamuzi yake mengi ni jeshi ama vikwazo,yeye mazungumzo kwake hua ni kidogo sana,ukimshinda kwa hoja jiandae kwa kipigo.
Njoo upande wa Urusi hata china na wenzao.wao ni hoja zaidi,kutokupoenda kutumia nguvu wala vikwazo,kupenda maridhiano na mijadala.
Angalia mgogoro huu,Urusi alianza kuisihi mda mrefu mno USA isizidi kuitanua NATO kuelekea kwake USA ikawa mbishi ,kiburi na dharau.
Mizozo mingi Urusi na china na wenzake wametaka.kuimaliza kwa mazungumzo.
Nataka kusema nini Sasa.
Kumbe mtu anajikuta Yuko kundi au upande Fulani kutokana na tabia za Upande huo kumvutia kulingana na tabia zake.
West - nguvu,ubabe,majivuno,kiburi,dharau,kujiona wanajua Kila kitu.
East - heshima,usikivu,majadiliano,upole,uungwana,kumshirikisha,ubabe,nguvu.
Reply nzuri sana katika zote nilizokutana nazo asbuh hii...
Umeeleza kiufundi zaidi mweeh.