Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Finland's foreign minister is "optimistic" about settling differences with Turkey over the country's NATO membership.

In his opinion, it may take several weeks to resolve the issue.

20220502_010825 (1).png
 
The Prime Minister of Poland called on Norway to share with Ukraine windfall profits from rising oil and gas prices, writes Bloomberg.

“Should we pay Norway huge money for gas - four or five times what we paid a year ago? It is not right. They must share this superprofit. It's not normal, it's not fair. This is an indirect profit from the war,” said Mateusz Morawiecki, offering to share the profit with a number of other countries.

20220502_010825 (1).png
 
Kusema NATO haijapeleka jeshi kwa sababu Ukraine sio member ni kujiFicha kwenye shamba la karanga!

Swali, hizo nchi zote walizowahi kupeleka ma/jeshi zilikuwa wanachama!?

Kubalini tu wanaiogopa Urusi!!! Na wao wenyewe wamesema kwa lugha ya 'kuavoid direct confrontation with Russia'

Peleka jeshi Puti aminye kitufe chekundu. Kuna anayetaka kubaki historia kwenye hii dunia!?
Ni kweli wanamwogopa Putin maana tangu mwaka 2008 (uvamizi wa Georgia) alianza kutenda kama mkorofi. Marekani inaona anasumbua kwa sababu wenyewe wanapendelea kuendelea kama wakorofi wakuu duniani....
Nchi za Ulaya wanamwogopa kwa sababu walijenga umoja na maendeleo makubwa tangu kuachana na ujinga wa vita waliouchezea kwa karne nyingi. Waliweza kupunguza majeshi na kutumia pesa kwa ustawi wa jamii na kuwekeza katika uchumi.
Putin anawalazimisha kuwekeza tena katika silaha na jeshi. Hawapendi, hadi Februari walifunga macho na kumpa Putin vikwazo vichache tu...

Marekani imesema waziwazi wanaona nafasi ya kupunguza uwezo wa Urusi kwa miaka kadhaa. Wanalipa silaha tu, Waukraine wako tayari kutekeleza upande wa kufa na kuua. Wanaona wanaweza kulipiza kisasi kwa vita ya Vietnam ambako Warusi waliwatendea Marekani vile (Urusi ilituma silaha, ndegevita na kwa siri hata marubani), Wavietnam walichukua kazi ya kufa na kuua, halafu Marekani ilishindwa.
Ni mchezo mchafu . . . .
Ila Ukraine wanatumia nafasi kutetea uhuru dhidi ya ukorofi wa Putin . . .
 
Kitakachokwenda kutokea sasa ni NATO kuweka wajeda wao rasmi sijui kama watakubali kushindwa coz wajeda wa Ukraine waliokua wanategemewa ndio hao washakamatwa hahaha naona kama vita ndio imeanza sasa ila huyu comedian angekubali mashart ya urusi wasingefika huku sema alikaza pole yake!
Niliwaambia hii vita imeisha na Russia ameshinda. Fikiria drone zilisumbua lakini dawa imepatikana within short time. Nguvu ya Russia ni vifaru na ndio vimeanza kazi . Russia ameongeza wanajeshi na mifumo ya ulinzi wa anga. Majeshi ya Ukraine yanajificha kwenye mitaro na maporomoko wanaogopa battle . Russia anawaona maana anga la mashariki kalishika anaona hata mabondeni .

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Russia iliwateka jumla ya wanajeshi wa Ukraine 2,439 waliokuwa wamejificha kama panya kwenye mashimo kwenye kiwanda cha chuma huko Azovstal, Mariupol. Wanajeshi hao waliojisalimisha kwa majeshi ya Russia baada ya kuzingirwa na kupigwa na njaa, kiu, ukosefu wa dawa za kutibia majeruhi wao n.k. kwa miezi takribani miwili.

Maafisa wa serikali ya Russia pamoja na vyombo vya habari vya serikali ya Russia wameonelea kuwa ni muhimu wapiganaji hao wakapiwa hadhi yao stahiki ya kutambuliwa kama Wanazi mamboleo (neo-Nazis) na hivyo ni kikundi cha wahalifu. Status hiyo itawalazimu mateka hao kufikishwa kwenye mahakama maalumu nchini Russia ili kuhukumiwa kama wahalifu wa kikundi cha kigaidi cha Wanazi mamboleo.

Familia za mateka hao zalia na kuhaha kutokana na hatua hiyo...Zaomba mateka hao wachukuliwe tu kama wafungwa wa kivita ili wasiingie kwenye upanga wa Pilato!


SmartSelect_20220522-204734_Chrome.jpg
Screenshot_20220522-204830_Chrome.jpg
Screenshot_20220522-205056_Chrome.jpg
SmartSelect_20220522-205143_Chrome.jpg
 
Hivi huko ni kujigamba?! Hizo nuclear za Uk zitaipiga Russia saa ngapi wakati Uk itakuwa imeshafutwa kwenye ramani na hypersonic missles carrying nuclear warheads?! Hypersonic missles cannot Be detacted...mnashitukia tu mmeshatwangwa...ukitaka uelewe vizuri mchezo wa vita vya nuclear soma vizuri nuclear doctrines za West (na hasa USA) na Russia...doctrine ya USA ni first strike yaani awe wa Kwanza kurusha makombora. ..na ndiyo maana USA hupenda silaha za nyuklia ziwe karibu na nchi zilizo karibu na Russia kama Ukraine, Poland na hata Rumania ili makombora hayo yatumie muda mfupi kwa first strike kwa miji kama Moscow...
Doctrine ya Russia kuhusu nuclear ni kutumia nuclear anytime dola ya Russia ikiwa hatarini kiusalama....Russia pia ana strategy ya 'dead hand' kwa maana kuwa kama leaders wa Russia wamekuwa wiped makombora ya nuclear automatically yanabonyezwa..
Ndiyo ni kujigamba. Nchi zote zenye silaha za nyuklia wameshajadili kila uwezekano tangu miaka 60 hivi..... hii ni sababu kwamba wote wana nyambizi zenye roketi za nyuklia. Tabia ya nyambizi ni, inatembea chini ya maji inaweza kurusha roketi kutoka mahali chini ya maji ambako haionekani.
Kwa lugha ya wanajeshi hii ni uwezo wa pigo la pili (second strike capability). Kwa hiyo wanahakikisha tishio la kumwangamiza adui halizuiliki.
Kwa hiyo: kesho saa 10 roketi hizo zinapiga Uingereza zinafika haraka na mifumo ya kuzuia makombora inashindwa kuzipiga. Uingereza yote inalipuka, wanaobaki ni mchungaji na kondoo 15 kwenye milima ya Uskoti..... Wote wengine wanakufa. Lakini nyambizi za Uingereza haziathiriwi, ziko chini ya maji. Wanapata taarifa kwa njia ya redio. kamanda anachukua bahasha kutoka droo anaifungua, anamwambia afisa mahusika atume roketi kwenye shabaha A, B, C - na saa moja baadaye Urusi ni historia, angalau miji yake mikubwa. pamoja na Moscow, Petersburg . . . .
Ila hata kama wangeshambulia Uingereza pekee, bado wangepata majibu kutoka Ufaransa na Marekani... majibu hayo yatatosha hata kwa wafugaji wa mbuzi huko Tuva.
Kinyume chake ni vilevile. Hapo ni sababu kwamba silaha hizo ni silaha za kutishana, si za kutumia.
Ni mchezo mchafu, mchezo ghali sana, - na pia mchezo hatari kiasi . . .
 
Ndio uposhaji wenyewe huo. Unaposema Marekani imesikitika wakati habari nzima hakuna sehemu inkaosemwa Marekani kwa akili yako ndogo hiyo kiasi huoni ni upotoshaji wa makusudi? Habari ya drone imetolewa na Wizara ya Ulinzi wa Russia. Wewe kwa kijaikili chako hicho, unategemea nini toka Wizara ya Ulinzi ya Russia?
Aha haaa, kwa hiyo issue ni kusikitika na siyo idadi ya drones zilizoangushwa. Hapa ndiyo naanza kuelewa kwa nini wahenga walisema, bora ukose mali kuliko kukosa akili. Unabisha ili mradi ubishe.
 
ICBM za USA hizi hapa:-

Active​

KAMA NA HAPA HUJAELEWA KUWA RUSSIA IS A SUPER POWER. Basi wewe hutaelewa maisha yako yote.
Hiyo Supa Pawa inawasaidia nini?? Walipigwa Kyiv, walipigwa Kharkiv, wanapoteza watu maelfu kukamata vijiji huko Donbass, jeshi lao la anga halidhibiti anga juu ya Ukraine . . . . Super Power inawasaidia nini??? (na uchumi tuangalie tu..... )
 
Ukitaka kujua Nato wapo hoi mcheki BIDEN anavyohangaika mara Japan mara Korea mara kule. Anaogopa kuanguka kwa mfumo wa dola . Anahofia msimu wa baridi hajui Putin amepanga kitu gani na washirika wake. Ndani ya US wanahoji matumizi ya fedha zao .

BIDEN haungwi mkono kila anapokwenda mf South Korea wanamwita muuaji na hawataki kuchonganishwa na North Korea

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Ndio uposhaji wenyewe huo. Unaposema Marekani imesikitika wakati habari nzima hakuna sehemu inkaosemwa Marekani kwa akili yako ndogo hiyo kiasi huoni ni upotoshaji wa makusudi? Habari ya drone imetolewa na Wizara ya Ulinzi wa Russia. Wewe kwa kijaikili chako hicho, unategemea nini toka Wizara ya Ulinzi ya Russia?

Kwa hiyo taarifa ingetolewa na the pentagon ingekuwa amini kwa kweli.
 
Urusi alianza kwa mzuka sana, akawa na limsafara la kilomita 60, tukajua Ukraine kwisha habari yake, nyuzi humu zikarindima kila uzi ukituahidi namna show itaisha kwa siku chache, ila Mrusi akasahau hamna kitu kigumu duniani kama kujaribu kupiga watu kwao hususan wenye uzalendo na nchi yao, utaanza kwa nguvu ya soda ila mwishoye utasubiriwa uanze kuhema na ndio kimemkuta Mrusi, leo hii anahemeshwa na kutafuta pakutokea.....

Hii ramani hapa inaonesha alivyokuwa amekaba maeneo, ila yanavyomtokea puani.....

timelapse-russian-forces-ukranian-counterattacks-t.png



In recent weeks, Russia has lost substantial ground that it initially captured after the start of its invasion in Ukraine.

When Russian President Vladimir Putin ordered the invasion in February, the Kremlin anticipated a quick takeover of Ukraine. However, Russia was met with surprisingly strong resistance from the Ukrainian people, who have put up an intense fight to protect their country.

As the invasion has continued, Russian military forces have largely been confined to the eastern part of Ukraine, including the Donbas region, with a report released Sunday by the British Ministry of Defence stating, "Russia's Donbas offensive has lost momentum and fallen significantly behind schedule."

Ule msafara uliogopesha sana, Putin akachimba biti kuwa salama ya askari wa Ukraine ni kuweka chini au kumkamata raisi wao.Kumbe Putin alijazwa upepo ya machuma ila vitani hakuna kitu.
 
Back
Top Bottom