Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

The Greek court has ordered that the Iranian oil tanker seized in instruction by the US be released.

Iran seized two Greek tankers in retaliation. They will have to ask nicely for their release.
Wahenga hii tunaisoma hivi; "Mahakama ya ugiriki imetoa amri ya kuiachia mara moja meli ya irani iliyokamwatwa na ugiriki chini ya maelekezo ya USA"

"Na serikali ya ugiriki itabidi iombe radhi meli zake mbili zilizoshikiliwa na Irani ziachiwe" Mahama Ugiriki.

Funzo; Maamuzi hayo yamefichua Uonevu na uovu wa USA kwa nchi zingine kupitia mgongo wa nchi washirika wake.

Naomba niunganishe na dot, kwa alichokisema mzee wa akili nyingi Mh.Rais V. Putin juzi kama siyo jana (nitatumia lugha yetu)

"Kuna aina mbili za taifa, taifa lililo huru na taifa linalo tawaliwa.Taifa huru hufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na taifa lingine, ukiona taifa haliwezi kufanya maamuzi yake lenyewe basi jua hilo taifa ni koloni(taifa linalotawaliwa na taifa/mataifa mengine)" V. Putin.

Funzo kutoka kwa Putin; katika hii dunia kuna mataifa huru machache sana, mataifa mengi yanafanya uamuzi kwa kufuata shinikizo au matakwa ya mataifa yenye nguvu. mfano ni hayo maamuzi ya UGIRIKI juu ya kukamata meli ya Irani chini ya maelekezo ya USA. Kwa mjibu wa Putin(na ndo uhalisia) mataifa mithili ya Ugiriki siyo mataifa huru bali ni Makoloni.

OMBI: naomba Russia iendeleze operation yake na iendelee kushinda kila aina ya jaribio linalofanywa na hao mabeberu wanao tamani waendeleze uviranja wa dunia, hii itasaidia pia nchi nyingi kuamuka na kuondokana na hii dhana ya ukoloni mamboleo. tuna hitaji dunia iliyo na balance of power, tunahitaji mataifa yajiendeshe na kufanya maamuzi yake yenyewe bila kuingiliwa na taifa au mataifa mengine. Hiyo ndo dunia itakayokuwa salama leo, kesho na hata milele.

Mungu ibariki Urusi na operation yake dhidi ya hayo manyambisi ya dunia.
 
Wabongo bwana... mgogoro wa Urusi na Ukraine unatuhusu nini sisi? Sisi tuhangaike na mgogoro wa serikali na wamasai Ngorongoro; na mgogoro wa M23 Kongo.
Kama haukuhusu mbona viongozi wako wa serikali kila kukicha wanasema umesababisha ugumu wa maisha huku kwetu?, Tofauti ni hiyo M23 ya miaka mingi sijawahi sikia ikihusisha hata kuipandisha bei pipi hapa kwetu
 
Tangu kuundwa kwa UN na mataifa kama US kushiriki missions mbalimbali za peace keeping dunia imeshuhudia utulivu mkubwa, amani, ustawi na maendeleo makubwa kuliko wakati wowote duniani.

Karne ya 20 baada ya vita vya pili vya dunia na karne ya 21 kimekuwa ni kipindi cha amani kuliko kipindi kingine chochote hapa duniani. New world order imeleta utulivu na demokrasia kwa mabilioni ya watu duniani na sehemu kubwa ya dunia imeshuhudia maendeleo kila sekta tofauti na karne nyingine zozote.

Ungerudishwa karne ya 19 au ya 18 wewe ungeweza kuwa mtumwa aliyehasiwa au mateka wa vita anayelima shamba la miwa Kilombero.
 
Kama haukuhusu mbona viongozi wako wa serikali kila kukicha wanasema umesababisha ugumu wa maisha huku kwetu?, Tofauti ni hiyo M23 ya miaka mingi sijawahi sikia ikihusisha hata kuipandisha bei pipi hapa kwetu
Maendeleo = Watu + ardhi + siasa safi + uongozi bora

Otea wapi tunapokwama,
 
Hizi ni comedy tu, Japan ni nchi ya tatu kwa ukubwa wa uchumi dunia.Japan Inauzidi uchumi wa Russia mara 4 kwa kila kitu.
 
Tupe chanzo cha habari yako.
 
Wabongo bwana... mgogoro wa Urusi na Ukraine unatuhusu nini sisi? Sisi tuhangaike na mgogoro wa serikali na wamasai Ngorongoro; na mgogoro wa M23 Kongo.
Raha sana mwamba... Hii ya ndani tutaanza kupekuliwa IP address kutafutiana sababu za kupotezana kusiko julikana.

Hizo za nje unazodoa tu na kuzungumza utakalo.
 
Hili tukio linaumiza Sana bora wangefia kwenye mapambano, yaani wakihukumiwa wengine mataifa ya ulaya kutasababisha vurugu Kwa raia kwenye nchi zao
 
Serrikali ya Russia, taasisi na kampuni zake zinadaiwa bilioni 120 na benki za mataifa ya magharibi.
 
Hakuna mkubwa wa dunia zaidi ya Rais wa Marekani.
 
Nilishalifanya hilo zamani za Pilato huko.....
 
Ujinga mtupu wa conspiracy za kiwendawazimu.

Na sisi tukiwaakaribisha Rothschilds na Rockefeller Africa tutaendelea kama Ulaya na Marekani ?
 
Mtoto wa darasa la kwanza hafundishwi hesabu za hasi na chanya.
Ukiwa kidato cha nne hukuwa na ubongo uliokomaa kiasi cha kuweza kufundishwa historia ngumu ya Ulaya na dunia kwa ujumla wake.
 
Za ndani kabisa "Uk ameshapata sabab ya kuingia Ukraine kwenda kuokoa raia wake,

Vikao vya kibabe vinaendelea ingawaje mkuu wa wajeda na wa ujasus wakiwa wanasitasita kuunga mkono op hiyo.

Ingawaje wanasiasa wanakazia kuwa inapaswa kufanyika kwa matarajio kuwa nato wataingilia ili kuongeza nguvu.

Chanzo;Mchambuzi toka karume mchikichin
 
Putin angelijua hii vita ingewagarimu muda mrefu hivi asiingeivamia Ukraine. Nawasikitikia matajiri wa Russia wamepata hasara kubwa sana kwa Nchi za Magharibi kufunga account zao na Mali zao kutaifishwa . Naona kama wataishi maisha ya mnyama Dickdick wa Serengeti National park. Ubwa kabisa Putin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…