Yote tisa kumi ni dini hii ni kansa inayotutafuna wototo wa Africa.
Maarifa yetu yamemezwa na hofu ambayo haipo.
Angalizo.
Sijazungumzia Mungu mkuu wa kila kitu ila dini.
Africa tulikua tunamtambua Mungu na hata kwenye kabila zetu ana jina la kikabila hivyo .
Dini ni biashara ila sisi hatutambui hili ila naamini kitakuja kupatikana kizazi majasiri,wajuzi na wenye msimamo kuisimamisha Africa.
Tukiweza kurudi kwenye tamaduni zetu na kuzienzi tutafika.
Dini zilikuja kuua ubunifu na utamaduni wetu Kwa asilimia kubwa Sana
Nakumbuka kigoma mwaka 1989 kijijini maeneo ya kasulu kulikuwa na ligi ya ng'ombe katika mchezo ule kuna mchezaji alichezewa vibaya na mwenzake akavunjika mguu yaani ugoko ulikatika katikati Kati ya goti na kiganja cha mguu
Alichukuliwa na kupelekwa nyumbani kwako akakandwa na dawa za mitishamba Kwa siku Ile maana muda huo ilikuwa unapelea Saa mbili kasoro usiku,
Kesho yake asubuhi aliendelea kukandwa na mitishamba, Ila ilipofika Saa Saba mchana alikuja mtaalamu akachukua vigoda viwili akavuweka Kati Kati ya uwanja palipokuwa hakuna kivuli kisha akamchukua mgonjwa akamuambia akae juu ya kigoda kimoja na kigoda kingine akaambiwa aweke kisigino cha mguu wake uliovunjika, kiufupi asilimia kubwa ya ule mguu uliovunjika kivuli chake kilionekana ardhini, Yule mtaalamu akaanza kuchanja chale kile kivuli cha mguu uliovunjika,
Na ule mguu ulikuwa unajitajika kunyooshwa ili ukae sawa, Yule mtaalamu alianza kunyoosha kivuli cha mguu mpaka kikakaa sawa na mguu wa mgunjwa ukakaa sawa, akaanza kupaka dawa kivuli cha mguu sehemu aliyotumia alipomaliza kuna nyingine alipaka kwenye mguu wenyewe, kutoka hapo jamaa alibebwa kwenye machela hakutakiwa kutembea Kwa wiki moja na alikuwa anapiga dawa tu, baada ya wiki jamaa alianza Kwa kutembea japo Kwa kuchechemea lakini hakufungwa hogo wala kitu chochote hata miti hakufungwa
Sasa jiulize waafrika Kama tungekuwa na technology yetu hiyo kulikuwa na umuhimu wa kutumia x-rays ambapo kila ukipiga inakupunguzia umri wa kuishi?
Kuna sehemu Kati ya mbeya na iringa sikumbuki sawasawa, jamaa anauza asali lakini kwenye kibamda cha kuuzia hakuna muuzaji, hapo unakuta asali imeandikwa bei yake pembeni kuna ungo Una pesa, unachotakiwa kufanya ni kuchukua asali inayolitaka pesa ya manunuzi unaweka kwenye ungo kama unahitaji chenchen chukua inavyotakiwa usizidishe kisha ondoka, jamaa anakuja jioni anakuja kuchukua asali iliyobaki na pesa yake anaondoka,
Sasa jiulize technology hiyo waafrika wangekuwa nayo tungefunga kwenye masuper market tungeokoa kiasi gani kwenye technology inayotumika kwenye hayo maduka??, Computer, camera za CCTV, walinzi, cashier mitambo ya kuscan bidhaa nk, tungeokoa kiasi gani????, Na nchi za ulaya wangetuuzia nini maana hawana resources,
Watu zamani walikuwa wanaweza kuita nyuki,Simba, nyoka,fisi,mamba na walikuwa na uwezo wa kutuma Hadi radi kwenda kuangamiza, sasa jiulize kama wataalamu hawa wangejiunga na kutengeneza umoja ambao wanakuwa Kwa maslahi ya kulinda taifa tungehitaji mizinga,rada na bunduki za wazungu????
Babu yangu alipokuwa mdogo walikuja Dar kuja kuchukua chumvi na kuipeleka nyumbani songea alibeba pishi tatu za chumvi walitbea Kwa miguu kutoka dar Hadi songea alifika akiwa anaumwa Sana na kichwa Baba yake akampatia dawa ya miti shamba hilo tukio lilitokea akiwa na miaka kama 20 hivi basi toka siku hiyo mpaka amefariki anamiaka 93 lakini hakuwahi kuumwa kichwa, yaani ataugua magonjwa yote lakini kichwa hajawahi kuumwa tena toka atumie dawa, katika vitu alivyolaani babu ni kutukumuuliza Baba yake kuwa alitumia dawa gani kumtibu, maana wakati Baba yake anafariki babu alikuwa vitani mashariki ya Kati alipigana Vita ya pili ya dunia yeye akiwa kama Askari,
Sasa jiulize kama utaalamu huu ungekuwepo tungehitaji panaldo????
Kwa hiyo matatizo mengi yanatufika waafrika Kwa kuziaacha mila na tamaduni zetu kisa dini zilizoletwa na ngozi nyeupe,
Sikatai kulikuwa na makosa flani kwenye Mila zetu tulichotakiwa ni kuchuja kuacha zile Mila potifu na zile zingine kuzirekebisha na kiziimarisha, kama kuna watu walikuwa wanatumia utaalamu wao kuumiza watu wengine tungeanzisha umoja WA wataalamu ambao katika majukumu yao ni pamoja kuwaadhibu wale wanayotumia utaalamu wao kuwadhuru wengine,
Ungejusikiaje MTU kakuibia simu unaenda Kwa mtaalam unalipia 10k, mtaalamu akachukua tube ya baiskeli anaijaza upepo Yule mwizi aliyeiba tumbo linajaa, Anatoka alikokuwa anakuja mpaka nyumbani kwako anakurudishia simu yako na yeye anapata unafuu, kwenye kitu kama hiki ubaya wake ni nini??????