Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

🙄🙄🙄
 
Economic potential bila values kama separation of powers, rule of law, free media, respect of property rights haina mashiko na haiwezi kuwa na ushawashi jamii nyingine.

Putin akiamka vibaya na wewe anakufulisi kama Mikhail Khodorkovsky, Boris Berezovsky, Anakufunga kama Alexei Navalny, Anaku assasinate kama Boris Nemtsov au ukimbilie uhamishoni kama Anatoly Chubais aliyehusika na sera ya ubinafsishaji ya Russia na wengine wengi wanaoishi uhamishoni.

Russia haiko predictable. Imezivamia Georgia na Ukraine huku ikiiacha na kuhaidi kutoivamia Finland kwa dai lile lile !
 
Ilikuwa zamani ambapo USA alipumbaza Nchi nyingi zika page fedha zao katika dollar ya USA.sasa hivi Nchi nyingi zimeanza kuweka fedha zao katika zahabu na fedha zingine-so kudidimia kwa uchumi wa USA hakutakuwa na madhara makubwa kiuchumi kama unavyo taka kutuaminisha.
 

Ni ukweli ulichosema tunategemeana ila tayari kuna mipaka ya kimamlaka(nchi) sasa taifa moja lisiishi kwa kususbiria huruma ya taifa lingine.

Mathalani wote tuna utashi wa kufanya kazi (viwandani,mashambani etc)
Kupitia tutakacho kipata kutokana na Hiyo kazi ndio tutumie kujihudumia na Misaada haikataliwi ila iwe ni ya dharura mfano mlipuko wa maradhi unaoitaji kudhibitiwa haraka,baa la njaa,mafuriko na n.k

Na kuhusu kupata ambacho hatuna ni kupitia surplus ya tukizalichao ivyo tutaweza kuajiri au kununua technology kwa nchi zilizo na uwezo huo.

Kuhusu ARV sidhani kama wamarekani wana huruma kuliko sisi ambao ndg zetu ndio wanaoteseka na huo ugonjwa hivyo ni lazima suluhisho lingetafutwa kama nchi ili kuokoa kizazi kisipotee.

Moja kwa kuandaa wataalamu wa kuchunguza na kutoa ufumbuzi wa nini kifanyike ili kunusuru wananchi wake.

Mbili serikali ingenufaika kwa ugunduzi wa dawa au chanjo.

Tatu serikali ingejikusanyia fedha za kigheni kwa kuuza hiyo (dawa,huduma) nje ya mipaka yake.

Nne nchi kama nchi kutambulika kimataifa kwa kutoa mchango wake wa kulinda dunia na maradhi.

Hiyo ni kwa ARV tuu unaona jinsi tunavyopoteza kuliko kuendelea.
 
Of course kwa wasio ifahamu Russia, wasio mfahamu Putin, kwa wenye vihoro nae kama wewe utawashika sana kwa hizi flow zako. But as a matter of fact, Reality or the Truth have nothing to do with your "Wishes"... With your personal taste.

We kukuruka whatever you want, tafuta vijineno as much as you can ila ukweli utabaki pale pale. Uupende usiupende it's upon you!
 
Kwa sababu Syiria ni mojawapo ya mataifa ya hovyo zaidi kwa sasa na halina cha kupoteza tena. Mataifa mengine kama Belarus ambayo ni washirika wa Putin wanajua wakitambua na kubariki rasmi huo uasi ipo siko baadhi ya maeno yao yatajitangaza huru kwa hiari yao au kwa figisu kama alizofanya Putin huko Mashariki mwa Ukraine na mataifa mengine yatayatambua rasmi na hawatakuwa na mtu wa kusimama nao.

China inajihadhiri na ujinga kama huo kwa sababu inajua kuna Tibet, India kuna Kashmir, Uturuki kuna Wakurdi, Iran kuna Balochistan, Myanmar kuna Rohingya. Tofauti ya hizi harakati za huku na za Ukraine ni kwamba hizi ni halisi wakati za Ukraine mashariki ni propaganda tu za Putin.
Leta majibu, Mkuu. Ha ha hahahaha!
 

South america ipi unayoizungumzia.

Brazil ni member tayari BRICS na Argentina tayari kashatuma proposal ya kujiunga chama kubwa.

Linapokuja suala la mpira ni hao miamba wawili wenye legacy hiyo ni moja.

Mbili watapewa offer ambayo hawataweza kuikataa Russia ni supa pawa.

Tatu huku Africa especially magharibi wana wanasoka bora compared to other parts of africa hivyo sidhani kama hata wanathubutu kujaribu kukataa fursa mpya RUSSIA hata kwa kimawazo tuu.

Nne kama wataalamu wa kudhibiti system za mataifa mengine anao atashindwaje kuipromote iyo ligi international hata mimi nisieupenda mpira nikatamani kuona.

Russia sio zimbabwe.
Uurraaa.
 
Unafahamu Russia na nchi nyingine nyingi ziliachana na Gold Standard mwaka 1914 vilipozuka vita vya kwanza vya dunia?

Unafahamu UK na USA ni nchi zilizochelewa kuachana na gold standard, UK akiachana na huo mfumo rasmi mwaka 1931 na US mwaka 1971?

Nchi inawekaje pesa zake katika dhahabu??
Sidhani kama una uelewa na unchojaribu kuelezea.

Gold standard imekufa na hairudi tena, acheni ndoto za ajabu ajabu.Muda wa miaka 50 iliyotumika hapa duniani ilitosha kuelewa matatizo yake na jinsi gani huo mfumo ulikuwa haukidhi mahitaji mapya ya mfumo wa uchumi wa karne ya 20 na kuendelea.
 
Hakuna ligi yoyote ya football ya BRICS, BRICAS au whatever the hell itakayoanzishwa. Hakuna timu itafanya ujinga wa kusafiri kutoka South Africa kwenda kucheza Russia au India kwa wacheza Cricket, hakuna timu ya Brazili itajisumbua kuzunguka huko China, India na Russia kila wiki kucheza mechi.

Kama ungekuwa unafahamu mahusiano ya West Africa na Ufaransa kijiografia na Utamaduni ungekuwa umeshaelewa hakuna mchezaji wa Africa magharibi utamtenga na Paris, Monaco, Lile n.k kama daraja lake la mafanikio ya kisoka. Hakuna anayeifikiria Moscow anapochipuka, huko wanaenda kumalizia soka lao tu wakishachoka.
 

Yondo sista on the beat😃😃😃

Turudi kwenye mjadala.
Dunia haijatoka kwenye mfumo wa gold kwamba ni kitu cha kushangaza.

Huko nyuma kabisa ilikua bidhaa kwa bidhaa tukaona tunapunjana nakupa kuku unachukua gunia la mahindi.

Tukahama tukaja chumvi ilikua adimu sanaa zama izo mfano wa dhahabu.Sasa baadae zilipokuja kugundilika njia mbalimbali za kupata chumvi tofauti na ya kugema baharini iyo nayo ikafa.

Tukaja sarafu za shaba,fedha,dhahabu kila taifa na yake iyo nayo ikafa.

Ukaja mfumo wa gold nao hukutoa jibu kutokana na hiyo unequal exchange.

Ukaja huu mfumo wa makaratasi na sarafu kwa mbalii nao hautoi majibu ya uwiano wa kufanya biashara bado manung'uniko ni mengi.

Sasa mataifa yenye uthubutu wanataka kusimamisha fedha zao kwa ajili ya kufanya biashara.

Kwa hiyo ukiangalia huo mtiririko ni wazi dollar inaenda kutumika New York tuu maana inaenda kukosa nguvu na ushawishi wake.

Hivyo dunia tunaenda kuingia kwenye mfumo wa mseto wa sarafu kutoka mataifa au mabara yenge nguvu.
 

Sasa unapangia watu maisha

Huna hoja hayo ni makasiriko😃😃😃.

Moscow anapochipuka nimependa inamaana EU na US wanazama.

Ni ngumu kibinadamu ila nmekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…