Cash Generating Unit
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 13,284
- 39,513
Hongera Sana hiki cheti fanya bendera ya Russia iwepo au colours zile za Russia itapendeza Zaid
NAKAZIA
Hongera Sana hiki cheti fanya bendera ya Russia iwepo au colours zile za Russia itapendeza Zaid
Huna hata aibu,taja hayo mataifa ambayo yanaweza kuikalisha Urusi,mwa mjibu wa NATO,walisema wameanza kujitayarisha kwa hii vita kutoka 2014,mpaka sasa hivi,Ila bado wanapigwa.Siku hiyo Urusi itakosea njia iguse kataifa kamoja ka NATO kama vile kajirani kake hapo Latvia ndio itaelewa nini maana ya kipigo cha mataifa 30, kwnza humo kwenye hayo mataifa ya NATO kunayo machache supapawa yenye uwezo ya kuiliza Urusi yenyewe bila muungano, maana ameonyesha udhaifu mkubwa sana kushindwa na haka kataifa kadogo....
![]()
Hahah, Huo mfano wa kuku alio utoa mwamba una hoja nzito sana ndani yake,
Nisahihi kabisa kwamba kama kuku wangekuwa wanaongea halafu wakasikia kuwa anae wajali kwa kuwapa chakula, chanjo, maji na sehemu ya kulala lengo lake niku wachinja au kuwauza baadae, hakika kuku hao wasingeelewa na wangemuona anae wambia hayo maneno kama mchonganishi na anachuki binafsi dhidi ya mfugaji wao.
Hiki ndio kinatokea kwa pro-West na USA tunapowambia nia ovu zilizo jificha nyuma ya neno misaada ya hao Wazungu, wanatuona kama tuna chuki binafsi na hao watu na tunaongea vitu vya kusadikika.
Inasikitisha sana kuona kizazi cha karne hii ya 21 bado kinafurahia misaada huku kikiendelea kunyonywa na kuwa tegemezi kila siku. yani kijana mbichi wa kisasa bado ana akili kama za mababu zetu enzi za ukoloni waliokuwa wanapewa zawadi ya vioo vya kujiangalia sura, nguo na shanga wao wanatoa dhahabu, Almasi, Ardhi, Nguvu kazi na n.k huku wakiendelea kumuabudu mzungu kwa vitu hivyo alivyo waletea kama zawadi na misaada pasipo kufikiri thamani ya vitu vinavyochukuliwa kutoka kwao.
Kuna kipindi nchi yetu chini ya jpm ilianza kueneza ideology ya kujitegemea kiasi kilichotufanya Tanzania tujione kama miongoni mwa nchi zenye hadhi duniani(DONA KANTRI) ikafika wakati hadi tukaanza kutoa misaada ya kibinadamu nchi jirani za Zimbabwe [emoji1269], Malawi[emoji1156] na Msumbiji [emoji1174] (ref:2019) na hata kupaza sauti kwa mabeberu kuiondolea vikwazo Zimbabwe. Hakika tungeendelea na hii spirit tungekuwa mbali sana sasaiv, lakini kwavile taifa limejaa wavivu na wapenda misaada baada ya kupotea tu kiongozi wa hiyo ideology hayati JPM ghafla tukarudi kwenye utaratibu wa kutembeza bakuri nje na kuaminishwa tena nchi haiwezi kujiendesha yenyewe. HAPA SUALA LA MFUMO NA UJINGA NDO SHIDA, NCHI NYINGI ZA AFRIKA HAZINA MFUMO IMARA NA ZIMEJAA WATU WAJINGA KUANZIA KWA VIONGOZI HADI RAIA WAKE.
☆Ili kujinasua kwenye huu mtego wa misaada maamuzi magumu na akili kubwa kwa pamoja vinahitajika, CHINA [emoji630] miaka ya 1961+ ilikuwa ni miongoni mwa nchi masikini duniani ikiwa na GDP ya around $50B, leo hii tunaongelea China yenye GDP ya $14T+ what a gap?
Mabadiliko hayo hayakuja kwa akili hizi za kutegemea msaada bali waliamua kuchukua njia yao na kuanzisha sera zao walizo ona zinawafaa kunyanyua uchumi wao miongoni mwa sera hizo zilikuwa ni sera ya ujamaa na kujitegemea, sera ya kujenga taifa lenye watu wengi kwajili ya nguvu kazi, China Kwanza na n.k
Kwetu bado tunashangalia misaada ya Kondomu, matundu ya vyoo, vyandarua na barakoa kweli tupo serious?
Urusi inatakiwa irefushe hii operation mpaka ifikie mahali vyuma vikaze kwa watoa misaada harafu nione kama nchi za Afrika hazitaweza kujiendesha bila misaada. Pia operation iendelee ili Urafiki wote wa kinafiki baina ya Afrika na mataifa ya ulaya na amerika uvurugike na kila mtu aanze kupambana na hali yake baada ya muda huko mbele naamimi kila taifa litakuwa lishajua namna ya kuishi bila kutegemea sponsors maana sponsor hufa au kuugua
I stand with Russia[emoji635][emoji635]
Ewaaa Mkuu tukumbukaneView attachment 2281023
Kama kawaida yetu Pro russia ni watu wa vitendo kama Rais wa dunia PUTIN.
Certificate of Appreciation kwenu.
NB.Kuna nyingine zitakuja maana kuna watu wengi tu hawapo kama vile Morogoro kaskazini na wengine.
Hapa kwetu Tanzania walio wengi wananunua Umeme katika rate ya 26kwh kwa Tsh 10k. Hii bei nikiwa wrong mta-nisahihisha japo kwa Meter nayotumia nagharamika kama hivyo.
Maana ake ni kua kwa bei yetu ya 10k kwa 26kwh (kilo watts hour) itanigharimu kama Tsh 385k ili nipate umeme wa 1,000kwh ambayo ndio 1 Mega-Watt Hour.
Kama wao wanalipia 790Euro per MWH Sie hapa tunalipia 155Euro per MWH (nifahamike kua nime-convert 385,000 Tsh to Euro). Fedha zote hizo ukiziweka kwenye pesa ya Tanzania. Ni kua kwa the same amount of electricity, that's 1Mega-watt Hour. Sisi tunalipia Tsh 385,000/- wao wanalipia Tsh 1,960,000/-. Hii ni mara 5 zaidi kiliko sisi.
Nimeamua kuisherehesha hii post kwa kusudi moja tu. Kuna dhana potofu watu weusi tuko nayo, most of us utasikia tunasema ooh Europe wanalipa mishahara mikubwa n.k. lakini hatuangalii expense kulinganisha na mishahara yao.
Tunashangaa sana number, nimeona Mr Tyang na Galip Vrl wamezungumzia kuhusu analysis. Hapa pia huwa kuna tatizo. Europe mtu anaweza kulipwa Euro 1,500 per month, hii ipo around 4Millions za kibongo. Zinaonekana nyingi on Paper ila ukizipeleka kwenye matumizi ni chache mno kwa mazingira yale.
Huezi kupanga chumba cha Tsh 40k, ambazo ni Euro 16 kule kwao. But nje ya Dar kwa hapa Tanzania, Tsh 40k unapata chumba safi mno.
Hii issue ni pana kwani hata concept ya GDP unaweza kuijumuisha pia.
Mfano,
Mimi leo nikilima shamba, kila chakula nikawa najitegemea. Mahindi nalima, Mpunga nalima, Mchicha nalima, Almost kila kitu nakifanya mwenyewe.
Hapa nitanufaika lakini Hizi shughuli zote hazitakuwa reflected kwenye pato la taifa since hakutakuwa na Movement of "Cash" wala Shughuli kutoka kwa kundi moja kwenda kundi lingine.
Mfano wa kwanza huo, wa pili. Imagine katika mazingira kama haya. Mchicha nanunua kwa John, Karanga kwa Ayubu, Mahindi kwa Mabula, Mchele kwa Mwamposa, Mafuta kwa Mangi, Ndizi kwa Rutashobya. Hapa kunakuwa na Movement kubwa ya Cash, kunakuwa na shughuli nyingi. Hizi zote zinakuwa reflected kwenye hii kitu tunaita GDP. Pato la Taifa. So GDP inapea.
Hii mifano miwili sikidhamiria kuileta kwenye reply ya kaka mkubwa hapa. Imenibidi niitoe kwani yafanana na kile nilichokua nataka kukisema kupitia reply yake.
Mifano hiyo miwili inaweza kuwapa majibu katika nyanja hizi.
[emoji842]Kwanini Nchi kama Russia, Kwanini Nchi kama Singapore au South Korea.
[emoji842]Kwanini Mkoa kama Dar es Salaam, na Kwanini Mkoa kama Mbeya, Ruvuma n.k
[emoji842]Of course itawapa majibu kwanini tulisema yule anayejiita Yoda tulimwambia hajui kitu upande huu alipokuwa analinganisha Pato la Taifa GDP na Thamani ya Kampuni Sokoni (Market Cap.)
Dar, kitunguu unanua, Mchicha unanunua, Muhogo wa kutafuna unanunua, Maji Visima hakuna mnanunua kwa kifupi Most katika vitu unahitaji ni kazi za watu. So mzunguko wa fedha na wingi wa shughuli ambazo ndio Uchumi wenyewe ni mkubwa, So there we go, unaambiwa kua Dar ina 17% of Tanzania GDP.
Mind you Uchumi sio Pesa, Uchumi ni shughuli za kibinadam ambazo of course ni issue zinazohusiana na fedha. Lakini Uchumi kama Uchumi sio how much you have bank au mfukoni.
Again ukichimba deep, utakuta all these stuffs zina mahusiano kiasi na flan na Culture, I mean life style ya watu. Anyway tuishie hapa nisije kuwachosha bure issues zenyewe ziko out of topic.
Nimekuvulia kofia🙌Leo ni mwendo wa kukupiga spana tu, mpaka akili ikukae sawa, Naenda kujibu hoja yako ya kwanza mpaka ya mwisho kwa mlinganisho wa Russia Vs USA.
1."Mrusi ni mchoyo wa kila kitu na ndo maana ni mataifa machache yanayo ongea Kirusi" FUSO
☆JIBU: Urusi ni miongoni mwa mataifa machache duniani yanayotumia lugha yake asilia kama lugha ya taifa, hata sisi Tanzania tupo kwenye list hii kwa kigezo cha kiswahili chetu, lakini Mpaka muda huu USA anatumia lugha ya muingereza (english) kama lugha yake ya taifa. Hivo basi hoja yako ni dhaifu kwasababu Russia ana lugha yake asilia ila USA hana zaidi ya kutumia lugha ya malikia kwa kuivisha jina la kihuni American english.
2. "Pesa zake nyingi anatumia kutengenezea silaha badala ya kusaidia nchi zinazo endelea" FUSO
☆JIBU: Mosi, kila nchi inatumia pesa kulingana na vipaumbele vyake, let say Urusi inatumia pesa zake nyingi kwenye silaha halafu USA inatumia pesa nyingi kwenye kampen ya kueneza Ushoga duniani(kupanga nikuchagua)
Pili, Nchi huru siyo lazima isaidiwe, maana ya kuwa huru nikujitegemea na kuendesha uchumi wako mwenyewe. Aliekuwa Rais wa USA D.Trump aliwahi kusema, "kuendelea kuzisaidia pesa nchi za Africa zilizo dai uhuru wa kujitegemea ni ujinga, kama nchi haziwezi kujitegemea zenyewe bila misaada basi zitawaliwe tena na wanao zisaidia mpaka zitakapo acha kuwa tegemezi" Trump. Hivo basi kwa fact hiyo ya Trump, Hoja yako hii pia ni dhaifu.
3. "Mrusi siyo muumini wa domokrasia ni dictatorship"
JIBU; mosi, Ni ujinga mtupu kufikiri mfumo wa democracy ndo mfumo pekee unaotakiwa kuendesha serikali za nchi zote duniani, kuna mifumo zaidi ya 15 ya kuendesha nchi na kila nchi huamua itumie mfumo upi kulingana na nature yake. mfano, China-Socialism, UK- Kingdomship na French-Democracy.
Pili, Mfumo unaotumika kuendesha serikali ya Russia siyo dictatorship bali ni Federal democratic state.
Tatu, USA unae dai anatumia pure democracy itakuwa hujui hata aina ya democracy anayotumia USA, Raia wa USA kura yake haina nguvu yeyote katika uchaguzi wa Rais je hiyo ndo maana ya democracy? Hoja yako hii pia haina mashiko.
4. "Urusi haina influence yeyote Africa, Ulaya na America" FUSO
JIBU; Mosi, Inaonekana hujui hata maana ya neno "Influence" kitendo cha Uchumi wa nchi za Ulaya kutemea uwepo wa Urusi hiyo siyo Influence? Russia mpaka leo hii ndo influencer mkubwa wa bara la ulaya bila Urusi ulaya nisawa na Afrika tu.
Pili, Kwenye bara la America ukiwatoa N.America (USA na Canada) the rest of Americans (Especially Southern part) wote wapo upande wa Urusi, mfano, Brazil, Argentina na nk.
Tatu; Kama Putin asingekuwa na Influences kwa bara la Africa nchi za Afrika zingebaki neutral kwenye kura ya kuiondoa Urusi kwenye baraza la usalama UN? Au Zelensky angeishia kusikilizwa hotuba yake kwa AU na Viongozi wanne tu kati ya viongozi zaidi ya 50 wa nchi za Africa au Mwenyekiti wa AU angeenda Urusi kuongea na Putin?
HOJA YAKO HII PIA HAINA MASHIKO.
5. "Hana bajeti yeyote kwa nchi za Afrika" FUSO
JIBU: Mosi, Kwani nani alikwambia afrika nisehemu ya Urusi hadi ihusike kwenye bajeti ya Urusi? Nitajie nchi za Afrika ambazo ni makoloni ya Urusi hadi aya include kwenye bajet yake.
Pili; Nchi karibia zote afrika ziliomba uhuru na zikaupata maana yake ziliomba zijitawale na kujiendesha zenyewe sasa bajeti ya Urusi inakuja vipi tena kwa mataifa huru?
Narudia tena kauli ya Trump "Kama nchi za Afrika zimeshindwa kujiendesha bila kutegemea misaada yetu basi zitawaliwe tena"
I STAND WITH RUSSIA [emoji635]
Makubaliano na ww mkuu
Kwa eu ya sasa ujeruman ndio mwenye uchumi mkubwaUjeruman Alikua mbabe Sana awamu ya Hitler, tangu jamaa afariki wamekua rojo Sana[emoji4]
Siku mkiweza kuteka Kiev uniamshe kwenye ndoto zangu, supapawa la hovyo sana, kainchi kadogo hapo jirani kameshindikana, halafu huyu ndiye waarabu humtegemea jameni....
READ MORE: Russia promises more disclosures on Ukraine biolabs
READ MORE: US-funded labs in Ukraine dealt with bat coronavirus, Moscow claims
READ MORE: Russia claims Ukraine destroying evidence of US-funded bioweapons programSoma hapo chini map not to scale maana yake hiyo raman haijazingatiwa scale hivyo basi vipimo havipo sawaMlikimbilia na kujaribu kuparamia haka kainchi kule Kyev kakashindikana.....
Ndio nimeshakubali kwa kweli ukubwa wa taifa sio kitu, kuna siku Watanzania walipiga makelele sana kumhusu Kagame nilikua najiuliza kainchi saizi ya mkoa kanasababisha nchi yote mlie lie kwani kana nini.... ha ha ha!!!
Hako kainchi ka-Rwanda pia kamekua kero kwa liinchi lote la DRC.
![]()
To the moment I can concur with other Pro Russia, though you're Pro-NATO but you really explain facts and otherwise you know what is opinions particularly emotions.[emoji1255] The problem of the Armed Forces of Ukraine is the lack of aviation. Here is another downed plane.
Soon we will face the complete absence of aviation, as such, which will further weaken the forces of the Armed Forces of Ukraine to counter the Russians, who continue to put pressure.