Kipala
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 3,763
- 700
Mkuu unamaanisha ahadi gani katika mapatano gani? Sikumbuki mkataba ambako Ukraine ilitia sahihi kutojiunga na NATO. Ukiweza kuutaja nitashukuru sana!!Na kwa bahati Mbaya Ukraine ilivunja ahadi yake kwa kutaka kujiunga NATO.
Ni sawa na mdogo wako wa damu umlee kwako toka mdogo kisha akishakuwa mtu mzima arubuniwe na jirani yako mwingine mwenye wivu na chuki zake juu yako avunje nyumba yako mnayoishi kwa kuwa amehaidiwa atasaidiwa kujenga kwake.
Kwenye kugundua hio njama unaamua kumtia kolokoloni kisha watu waje juu kuwa unamuonea mdogo wako.
Ninakumbuka tu mapatano ya Helsinki ambako Urusi ilikubali kwamba kila nchi ya Ulaya iwe huru kushiriki au kutoshiriki katika ushirikiano na nchi nyingine.