Ila Russia Kwa visingizio ni balaa,hii vita imewavua nguo nadhani zile mbwembwe za kubrag silaha zao sasa zitapungua
1) Walipofurushwa Kiev; Wakasema Nia Yao haikua kuikamata Kiev Bali ni Donbas na Luhansk,kama Nia Yao ilikua ni Donbas kwann walikua wanapeleka msafara wa vifaa vizito vya Kiev?!
Wale Askari WA miamvuli walioshuka pale Kiev usiku wa February walifata nini kama nia Yao haikua kukamata mji Mkuu? Au walienda kufanya birthday party na Zelenksy [emoji23][emoji23][emoji23]
2) Moskva ilipozamishwa: Walisema ni ajali ya Moto,kama ni ajali ya Moto kwanini baada ya Moskva kuzamishwa waliondoa Meli zao na kuzikimbiza karibu na Sevastopol?!
3) Baada ya Crimea kulipuliwa: Walisema ni ajali na sio shambulizi,lakini cha ajabu baada ya shambulizi lile Urusi iliondoa ndege zake zote kutoka Crimea,Mmmmh Strange!!!!
4) Baada ya kukimbia Snake Island: Baada ya kukimbia Snake Island walisema eti wameondoka Kwa Nia njema,kama ilikua Nia njema kwanini walikua wanataka kuweka mifumo ya kudaka Makombora pale lakini baada ya Meli iliyobeba huo mfumo kulipuliwa wakatangaza wanaondoka Snake Island kuonyesha Nia njema Kwa Ukraine [emoji23]
5) Baada ya Ukraine kuwachakaza kwenye uwanja WA vita: Wakasema kwamba hawapigani na Ukraine Bali na NATO,hivi NATO ana wanajeshi kule Ukraine?![emoji848][emoji134]
6) Na sasa kuna hii Referendum,ngoja tusubiri watakuja na kisingizio gani!!!!!
TUUPE MUDA NAFASI.
*"This is not a bluff" in Putin's voice [emoji23]