Kwanini Russia alitumia bombers ndani ya Syria zikadondosha mabomu, alikuwa na airbase pale Latakia. Si angetumia hizo missiles unazosema za 7000km range. Missiles are expensive ndio maana pro NATO walivyotutisha na Kinzhal hypersonic missile niliwaambia shangwe yao haitadumu Russia haiwezi afford kutumia very expensive missiles kila mission. Tangu wafyatue siku moja hadi leo sijawahi sikia habari za Kinzhal.
Su-25 ni ground attack, inafanya kazi yake vizuri, Ka-52 ni attack helicopter na ina performance ya chini navyoiona. Sababu kubwa ni kutotumia smart munitions wanapenda sana kutegemea unguided rockets na anti tank missiles zao zina range ndogo. Hizi ndege mbili sio air superiority, multirole wala omnirole kama Su-30, Mig-35 na jamii zake. Mi-28 siioni sana sijui kwanini.
Na si kweli kusema Russia inashindwa control ya anga la Ukraine kisa air defence systems za misaada. Hizo systems zimeanza letwa Russia ishachoka ilipoanza kuharibu miundombinu kwa makombora na nyingi zililetwa suicide drones za Iran zilipoanza kuingia. Miezi ilipita kabla Ukraine haijapokea AD system hata moja.
Suppression of Enemy Air Defense (SEAD) mission huanza kabla hata mwanajeshi mmoja hajakanyaga ardhi ya adui. Russia sio wendawazimu kusubiri waanze vita, wapigwe misururu yao kutoka Belarus, wafanye retreat kutoka Kiev na Kherson, wafyatue makombora miezi kadhaa ipite NATO waanze kutoa AD systems kisha ndio Russia waseme hatuwezi fanya SEAD kisa systems za misaada. Huo uwezo haupo, haupo kabisa. Wangekuwa na uwezo huo ndio jambo la kwanza wangefanya. Badala yake siku ya kwanza walifyatua makombora kama 100 hivi ambayo accuracy yake na effectiveness sio sawa na attack ya jets, pale jets zilitakiwa zifuatie kupunguza kabisa enemy air defence