Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Argument yenye mashiko.

Ila kulingana na taarifa ya Ministry of Defence nanukuu, “The Chief of the General Staff, General of the Army Valery Gerasimov, has been appointed Commander of the Joint Group of Troops (Forces). His deputies are: Commander-in-Chief of the Aerospace Forces, General of the Army Sergei Surovikin, Commander-in-Chief of the Ground Forces, General of the Army Oleg Salyukov, and Deputy Chief of the General Staff of the Armed Forces of the Russian Federation, Colonel Kim,”

Hapo hawajasema General Surovikin anaenda kuwa Deputy Chief of Staff (tuseme kama mnadhimu mkuu wa jeshi hapa kwetu), ila anakuwa Deputy wa Commander of Joint Group of Troops, cheo alichokuwa nacho Surovikin tangu 2022 October mpaka wiki jana na kinachotokana na hii operation, ikiisha nacho hakipo. Sasa hapo sijakuelewa unaposema anakuwa msaidizi ila amepandishwa cheo, kawa msaidizi wa cheo alichokuwa nacho. Labda sijaelewa kauli ya MoD

Kwa sababu hata hao wengine kina Salyukov na Colonel Kim nao ni deputies wa Gerasimov kwenye operation. Salyukov na Surovikin wako level moja.
 
Vikosi vipya vya Urusi vikiwa vimewasili front kwa ajili ya kuongeza nguvu zaidi


[emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635] Viva Russia






View attachment 2484603
Wakumbushe kuwa vijana wa mobilization ndiyo wanaingia kazini kuongeza nguvu, sasa wale walisema vijana walishaingia vitani wajue kuwa west waliwaongopea
 

Ukraine ya magharibi ni Galacians. Na wanataka their own homeland ambayo kwa sasa ndiyo nchi inayoitwa Ukraine. Lakini mazingira yenyewe ya Ukraine ni magumu sana.

Mpaka mwaka 1939 Ukraine ya magharibi hawa Galacians ilikuwa sehemu ya nchi ya Poland. Na hawa Ukraine wamagharibi (Galacians) hawapatani na Polish na ndiyo maana mwaka 1943 kulikuwa na mauaji ya Volin. Hawa wa Ukraine wamagharibi (Galacians) wafuasi wa Bandera waliwaua wa Polish vijiji kwa vijiji na ndiyo hawa manazi Azov, hawa wa Ukraine wa magharibi. Na hii akili mpaka sasa Western Ukraine wanayo; mpaka sasa bado wanajiita wafuasi wa Bandera na kwao ni shujaa na bado wanamuenzi.

Na hawa wa Ukraine wamagharibi kwao Polish ni raia daraja la chini na Russia kwao ni raia daraja la chini. Hata msemo wa Slava Ukraine haujaanza leo. Tangu kipindi cha Bandera walivamia vijiji vya Polish na kuvichoma moto na slogan yao ya Slava Ukraine.

Ukirudi kwenye historia baada ya Russia kumpiga Poland na kuchukua hilo eneo na kwa sasa kuwa sehemu ya nchi ya Ukraine lakini bado historia imethibitisha kuwa hawa wafuasi wa Bandera waliwaua wa Polish wengi, wayahudi wengi na warusi wengi, waliungana na Hitler WW2. Na watu hawa bado wapo Ukraine ndiyo hawa Nationalists hawa Azov. Waulize Polish kuhusiana na Wolyn na ndiyo maana miongoni mwa Poland wanaishangaa serikali yao.

Kitu kibaya ni kwamba NATO wamewatumia hawa ili kupambana na Russia. Na kibaya zaidi ni kwamba ukishajiunga NATO huwezi kupambana na pressure ya Marekani.

Kwa bahati mbaya NATO wamekosea kupiga mahesabu. Kwa bahati mbaya Ukraine hawana jeshi limeteketezwa! Wanachukua kijana yeyote na kupelekwa jeshini. Wanapewa mafunzo machache kisha wanapelekwa vitani na kuachwa wanazagaa wenyewe. Kinachotokea ni kwamba wanauliwa wengi. Wanajeshi wengine wanasalimu amri, wengine wanaendelea kupigana kwa sababu kuna special police ambao yeyote atakayesalimu amri walimuona wanamuua. Na wao wanasema haya si maagizo yetu ni maagizo ya NATO. Na ndiyo maana wachambuzi wengine wanasema mbeleni kuna asilimia kubwa wanajeshi wa Ukraine kuwageuka viongozi wao na hao NAZI AZOV. wakipigana wao kwa wao. Kupindua serikali ya Zelensky.
 
Mwaka 1982 Uingereza ilitembelea kilomita 13,000 kutoka kwake kwenda pwani ya Argentina kupigana vita ya Falklands. Argentina wakiwa na ndege za kisasa kipindi kile kutoka France, Super Etendard ambazo hazikuwa hata na miaka 10 tangu zianze kutengenezwa. Argentina wakiwa na one of the best anti ship missiles zile Exocet za Ufaransa hadi leo zinatumika.

Uingereza ilitumia wiki 10 kumaliza vita. Jeshi lake lilivuka maji 13,000km na likashinda. Russia ina miezi 11 inapigana na jirani ambaye hata wanajeshi wake ikiamua wavuke mpaka kwa kuruka kichura wanaweza.

Uzuri wa UK huwa inaprove wrong wanaojifanya wajuaji. Alikuwepo Napoleon Bonaparte, ego kubwa maradufu kupita Putin. Alikuwa anajua hapigiki, basi dharau za kutosha, ikaja Battle of Waterloo kamanda Mwingereza mmoja smart akamtimua Napoleon na kuikomboa Spain, Portugal na kuiepusha Ulaya nzima. Unahisi ni mchezo nchi nane (8) kumpa rank ya Field Marshall Duke Arthur Wellesley, ana batons za Field Marshal nchi zote hizo wakati Field Marshal wengine wana baton moja ya jeshi lao. Tukianza kutaja vyeo vyake alivyopata kihalali tutakesha.

Second World War pale Hitler alijua Britain ni dhaifu. Operation Sea Lion ilifeli hakuna meli ya Ujerumani ilivuka kufika Britain, ikaja The Blitz, ikaja Battle of Britain. Pote uko Nazi Germany ikaangukia pua. Kisha Hitler akaamua avamie nchi dhaifu nyinginezo, akapiga Operation Barbarossa kuitafuta USSR.

Ukweli mchungu msiotaka kuambiwa, Britain ndio ilitangaza vita dhidi ya Ujerumani baada ya uvamizi wa Poland. USSR na Stalin wake walikuwa na non-aggresion pact na Ujerumani maarufu kama Molotov-Ribbentrop pact. Na Marekani ikatangaza vita dhidi ya Ujerumani. UK na USA zilikuja kukomboa mataifa dhaifu ambayo Ujerumani ilivamia na kunyanyasa. Britain na US wangeamua kuufyata ila sio utamaduni wao, na hata sasa utaratibu ni uleule kwenye Ukraine hii. Hujatuvamia sisi ila cha moto utakipata.

Kuidharau Britain ni kujifurahisha tu. Mjenzi mwenyewe wa Russian Navy ya kwanza kabisa aliacha nchi akaenda kupiga kambi Uingereza akajifunza kuunda meli. Bila Uingereza, Russia melivita sijui ingezijulia wapi. Peter the Great, one of the best Russian Tsars in history aliufyata pale London akapigwa shule jinsi ya kufanya navigation baharini na kuunda meli. Russia ilikuwa na maji mengi haijui kufanya navigation, shukuruni Waingereza ebo!
 
Fast forward, 2008 Russia ikavamia Georgia jirani yake na former Soviet Union kama yeye

Utaratibu ni uleule kama wa kupanga misururu ya magari na kulipua miji, ndio uleule utaratibu wa Syria.
Hii Vita ya Georgia ilionyesha udhaifu mkubwa sana wa Urusi ila walifanya maboresho kadhaa na walipovamia Crimea mwaka 2014 (japo inasemekana wale jamaa walioonekana huko Crimea na mavazi ya kijani wakiwa wamefunika sura walikuwa askari wa Wagner), walionekana wamefanikiwa Sana kwenye 'modernization of the military', ila hii Vita ya Sasa inaonyesha bado mageuzi hayakubadili hali....

Kufanya mageuzi kama hayo lazima ufumue mfumo mzima sio mtu/watu binafsi tu.
Watafiti wa mambo wanasema kwamba, kitendo cha Putin kumteua Gen Gerasimov kinaonyesha kwamba hii inaenda kuwa vita kamili ambayo inahitaji coordination ya Joint Chief of Staff, ambayo huyo Gen Gerasimov ndiye mwenyekiti wake.
Vita kamili tena?....hii iliyohusisha mpaka mobilisation bado unaiita SMO ?
 
M
Muwe munafuatilia ukweli wa taarifa kabla kuzileta humu. Aliyekimbilia Norway ni bwana mdogo tu, aliajiriwa na Wagner July, 2022 kwa kandarsi ya miezi minne tu na hakumaliza. Siyo Kamanda Mkuu, kampiganaji tu.
 
Hizi cheap propaganda Zina kusaidia nini?

Elezea basi waingereza walivyodundwa mara mbili pale Afghanistan na kuuwawa jeshi lote na kufanya wabakie India tu.

Mwaka 1982 kule Falk Island Argentina walikuwa na hizo siraha za kupambana na uingereza?
Ukiangalia hata vifo ni karibu elfu Moja tu Ile sio vita utakayo tuletea ili kuboost ego yenu.
 
Mbona hiyo hiyo Uingereza haikuishinda Talban baada kuitembelea maelfu ya kilomita kuwafuata nchini Afghanistan?

Kulinganisha vita ya Ukraine na vita za huko nyuma ndo upumbavu ambao tunaukataa lakini mmekuwa mkijizima data.
Kabla hujalinganisha vita ya Argentina na Uingereza na vita ya Ukraine unaweza kunitajia ni msaada gani wa silaha alio kuwa ana upokea Argentina kama ilivyo kwa Ukraine sasa hivi?

Kinacho fanya vita ya Ukraine kuwa ndefu sio kwa sababu Ukraine ina nguvu au Urusi ni dhaifu bali ni usambazaji wa silaha za nchi za magharibi kwa Ukraine.

Mpaka sasa tangu vita ianze Ukraine imesha zambaziwa silaha zenye thamani ya $75 bilion ambazo ni sawa na bajeti ya ulinzi ya Ufaransa , Uturuki na Israel kwa kuziunganisha kwa pamoja lakini bado hazijafua dafu sasa hivi wana taka kutuma kifurushi kingine.
Kwa msaada wa namna hiyo hata kama ingekuwa Tz au Burundi tungeweza kupambana na taifa lolote lile duniani.

Ukraine kwa sasa ni sawa na mgonjwa mahututi asiye jiweza kwa lolote ambaye hawezi kuishi bila msaada wa mashine ya kupumua ina maana Ukraine anategemea silaha za wamagharibi ili aweze kuendelea na vita tofauti na hapo Ukraine haijiwezi kwa lolote kwa sasa.

Nchi zaidi ya 50 zimeungana kupambana na taifa moja kiuchumi na kijeshi na bado kiuchumi zimesha shindwa na kijeshi ni suala la muda.
 
Sasa hadithi yako inatufundisha nini?

Jitahidi sana watu wasijue kwamba wewe ni mpumbavu
 
Boya kweli huyu mtu kanywa supu ya bendera za marekani na ukraine
 
Hollywood imewaharibu Hawa watoto sana
 
NB: Haya ni maoni yangu. Ni very honest kama una utimu shauri yako


Umemaliza vizuri MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…