Tusubiri matokeo siku vikifika na kusogeza mpaka niTAG, HIMARS, drones za US zimesaidia nini so far
NAKUKUMBUSHA TU
1.
Javerines na NLAW. Hizi Ni Ant-tank Missiles. Hizi zilisaidia kusambaratisha msafara wa 64km wa vifaru vya Urusi vilivyokuwa vinaelekea kuuteka mji mkuu wa Ukraine. Mpaka sasa mji mkuu wa Ukraine Hakuna hata mwanamgambo wa Urusi alisalia.
2.
Stinger Missiles. Hizi Ni Ant-Aircraft Missiles. Hizi zilisambaratisha Helicopter zote za Urusi (Gunship) Kama Ka-52 na kusababisha mpaka hii leo Urusi hawezi Kupeleka Helikopta kwenye Anga la Ukraine.
3.
NASAMS,IRIS-T. Hizi Ni Medium Range Ant-Aircraft Missiles ambazo mpaka leo zimeangusha zaidi ya Fighter Jets 300 za Urusi. Mpaka leo hi ndege za Urusi hazikanyagi Tena kwenye Anga la Ukraine badala yake zinarusha Makombora kutoka Black Sea.
4.
HIMARS.Hii Ni Silaha ya Kwanza ya Mashambulizi aliyopewa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi. Silaha hii iliingia Ukraine mwezi wa 7 Mwaka Jana. Tangu Mwezi huo Hakuna Tena mji ambao ulitekwa na Urusi zaidi ya SOLEDAR waliyoteka wiki iliyopita. Kabla ya HIMARS Urusi alikuwa anateka mji mmoja Kila mwezi kuanzia miji ya LYSCHANSK,SEVERODOTNESK.
Pia,HIMARS ilisambaratisha Madaraja,Maghara ya Silaha na Command Post za Urusi katika mji wa KHERSON na kusababisha Urusi kuukimbia mji huo.
NB. Mpaka Sasa,Ukiachilia mbali HIMARS,Hakuna Silaha nyingine ya Mashambulizi(OFFENSIVE WEAPONS) ambayo Ukraine ameshapewa na nchi za Magharibi.Kwa miezi 11 Ukraine imekuwa ikipewa Silaha za Kujilinda ili kuzuia Urusi kusonga mbele. Mpaka Sasa mji mkuu wa jimbo la DOTNESK wa KRAMATOSK umeshindwa kutekwa na Warusi licha ya kuwa na Usongo nao.
Silaha za Mashambulizi (OFFENSIVE WEAPONS) Ni Zifuatazo:
1.Figher Jets (Ndege za Kivita)
2.Tanks (Vifaru)
3.Long Range Missiles (Makombora ya Masafa marefu).
Silaha hizo 3 ndio Silaha za Mashambulizi ambazo zinaliwezesha jeshi kusonga mbele. Lakini mpaka Sasa,Ukiachilia Vifaru na ndege za Kirusi,Hakuna ndege Wala Vifaru vya nchi za Magharibi ambayo vilishatumwa nchini Ukraine. Tunaona nchi za Magharibi zimeanza kuanza kutuma Vifaru aina ya Leopards 2,Challenger na Abrams. Hii Ni Hatua ya Kwanza ya OFFENSIVE WEAPONS ambazo zinaweza kurudisha nyuma majeshi ya adui.
Natabiri kwamba
Vita hivi Ni vya mda mrefu na nchi za Magharibi zinaenda hatua kwa hatua kwenye Vita hii. Mwaka huu 2023 tutashuhudia Ukraine akipewa vifaru vingi kutoka nchi za Magharibi. Mwaka 2024 usishangae ukaona ndege za Magharibi kuanza kutumwa nchini Ukraine. Na mwa 2025 usishangae Ukraine ikaanza Kupewa Makombora ya Masafa Marefu.
TIME WILL TELL.