Haya mwenye kujua.Nimeshaona nyie team NATO hamjui kitu.urusi Hana uhaba wa ardhi lakini hayo maeneo yamekuwa na shida na serikali ya Ukraine since siku ya Kwanza kuhamishiwa Ukraine kutoka urusi walikataa kuwa chini ya serikali ya Ukraine kwahiyo zelisky alipoingia madarakani akaanza kuwaua viongozi na watu wa hayo maeneo ya kirusi.kwa hiyo urusi akaamua kuingia kuwasaidia.Thank God maeneo yamesharudi urusi yakiwa salama .
Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Uchunguzi unatakiwa ufanyike Mara moja kwa huyu kijana huwezi kijana mwenye umri mdogo utuambie habari ya misaada yaani wa Ukraine suala la misaada kwenu mmelichukuliaje? Ni udhaifu mkubwa kwa mwanaume kutegemea misaada yaani kuolewa kupo karibu Sana tunakukemea achana na hyo point kuanzia Sasa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sizitaki mbivu izi.Sio mipasho, tumekua humu, urusi ilivyo jaribu kuparamia Kyev na msafara wao wakafukuziwa mpaka leo wanagombea kamji ka chumvi, wameuawa zaidi ya 127,000 hiyo ni idadi mara nne ya JWTZ.
Kumbe kuhusu Ufilipino umeshakubali? Rais anakaribishe Marekani kwa sababu China inajionyesha kama mbepari mkuu kwenye bahari kati yake na majirani?Tumieni akili,hivi kwenye akili zenu hamjiulizi kwanini hizo tension US hapeleki huko America ya kusini?Kwanini anadeal na China na Russia pekee?
Kama unatumia ubongo wako vizuri utaelewa!
Viongozi wakipindi kile hasahasa USSR..ambao tayari walikuwa wameweka baadhi ya makombora Cuba tayari, na mengine yalikuwa bahari kwenye meli..-walikubali kukaa chini na kusolve.....Matokeo yake USSR akaondoa makombora yake Cuba, na US wakaondoa makombora yao Turkey...Hilo lilitatuliwa kwa mazungumzo tu na Cuba haikuvamiwa mpaka leo.
Mkuu naona ukiwa na matatizo kujibu maswali kuhusu jambo moja unakimbia unajaribu kuleta topic nyingine.US aliivamia Iraq Kwa sababu gani?Tena UN walikataa ila yeye akatumia mabavu!Hujamsikia Tony Blair akiomba radhi na kutubu Kwa kushiriki dhambi hiyo ambayo aliingizwa mkenge?
US alitaka kuivamia Cuba mwaka gani na Kwa Nini?
Usiongee tu maneno matupu!
Hakuna kitu nilichokubali ila nimeona unazunguka zunguka tu maneno utafikiri robot ndio anaamdika!Kumbe kuhusu Ufilipino umeshakubali? Rais anakaribishe Marekani kwa sababu China inajionyesha kama mbepari mkuu kwenye bahari kati yake na majirani?
1.Russia kuzuia Ukraine kujiunga na NATO (kuzuia NATO Expansion)mwisho wa Vita hii tegemea mkataba mwingine Kati ya NATO na urusi Kwa sababu hakuna anayetaka Vita vya nuclear. 2.kusaidia majimbo yanayotaka kujitenga na Ukraine Kwa sababu ya mateso wanayopata Kwa serikali ya Ukraine. 3 Kutengezea multipolar world (kuondoa dominance ya nchi moja(marekani)ndo maana nchi nyingi zinaacha matumizi ya Dola.baada ya hii Vita nchi za ulaya zitakuwa Hoi kiuchumi.- taja hicho kiini watu wachambue,
Mimi nimekujibu uliposema kuivamia nchi nyingine kisa sababu za kiusalama ni mambo ya miaka 200 iliyopita!Mkuu naona ukiwa na matatizo kujibu maswali kuhusu jambo moja unakimbia unajaribu kuleta topic nyingine.
Tumalize Ukraine: wananchi wa Ukraine wanaotumia Kirusi kama lugha yao wamethibitisha mara kadhaa kwa kuura nyingi kwamba wanataka kuendelea kama raia wa Ukraine.
Urusi iliahidi kuheshimu mipaka na maeneo yote ya Ukraine (pamoja na Donbas na Krim) na kulinda mipaka hii. Ila Putin ameamua kuvunja ahadi na mikataba ya Urusi.
Tuko pamoja kuhusu jinai hizi za Kirusi? Baadaye tuanze kujadili jinai za Marekani. Au za mtu yeyote.
Kosa la Ukraine ni lipi ?...Viongozi wakipindi kile hasahasa USSR..ambao tayari walikuwa wameweka baadhi ya makombora Cuba tayari, na mengine yalikuwa bahari kwenye meli..-walikubali kukaa chini na kusolve.....Matokeo yake USSR akaondoa makombora yake Cuba, na US wakaondoa makombora yao Turkey...
Unajua kingetokea nini kama USSR wangeendelea kumpa kiburi Cuba na wao kukataa kuondoa hayo makombora???
US wangeisambaratisha CUBA...na wangekua na hiyo haki..
Ukraine acha avune alichopanda
Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Sababu moja wapo ya vita ya Ukraine.- taja hicho kiini watu wachambue,
Sababu moja wapo ya vita ya ukraine.Russia security.Nato walivunja mkataba.Haya mwenye kujua.
Kama masharti yenyewe ya western nikutaka kutufanya mashoga bora twende eastern
- kwani huko China misaada mnapewa bure? Si ndio wanaoongoza kwa kuchukua resources za nchi mbalimbali kwa mikopo yao yenye masharti ya kihuni au hujui?
- Mnapenda Sana kwenda East, China nk, Kwa sababu China wao hawaulizi au hawawekei masharti ya Kufuata/ Kuheshimu haki za binadamu nk kama kigezo cha kupata mkopo.
- Ww mwenye vision, Kagombee urais uonyeshe vision zako, na tena kwa Katiba hii hata Rais awe nani maendeleo ni vigumu Sana kupata, unless tuanze kumfunga mkanda/ Kubana matumizi ya serikali kuanzia Rais, Hadi Viongozi wengine wote wanaoishi kwa anasa,
Kasome vizuri mkuu.....hiyo Minsk ilikuja baada ya Crimea kuwa imeshaporwa na Vita vimekolea huko mashariki.....Urusi alishaona uelekeo wa misk agreement ndo maana alianza kuchukua maeneo kama Crimea ili yamsaidie kujilinda.hayo maeneo aliyopewa Ukraine Enzi za USSR wenyewe hawakuwahi kukubali kuwa chini ya Ukraine ndo maana kukawa na vita Kati ya serikali ya Ukraine na serikali ya maeneo hayo ndo maana urusi kaamua kuingia kuwasaidia ndugu zake Kwa sababu Ukraine walishindwa kufuata mkataba wa Amani wa maeneo hayo.
Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Kama ulikuwa hujui conflicts mashariki mwa Ukraine haijaanza Leo ilianza since Maeneo hayo yahamishiwe Ukraine wakati wa USSR.alafu mkataba wa urusi na NATO kutokuexpand ulianzia Miaka ya 90 huko.lakini marekani wakauvunja ndo maana urusi anachukua Maeneo kama Crimea kwa ulinzi Zaidi.kwa hiyo nakuelewesha mgogo mashariki ya Ukraine ni wa siku nyingi Sana na sio urusi waliouanzisha.urusi Hana shida ya maeneo.Kasome vizuri mkuu.....hiyo Minsk ilikuja baada ya Crimea kuwa imeshaporwa na Vita vimekolea huko mashariki.....
Halafu Vita huko mashariki mwa Ukraine vilianzishwa na Urusi mwaka 2014.
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Wa Ukraine wameisha, sahizi hadi vipofu wanapewa mikwasa waende frontMmmh ni hatari,ukiona Ukraine analazimisha kurecruit Hadi walemavu Ili wakapigane basi ujue wamepukutika sana!