Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

View attachment 2525661

⚡️The aircraft carrier Admiral Kuznetsov, which is undergoing modernization, left the dock and will return to the combat strength of the Russian Navy in 2024, said the head of the USC Rakhmanov.
Hili scrapper kumbe bado wanaliwaza. Tangu 2017 limeondoka dockyard leo. Meli inatumia muda mwingi nchi kavu kuliko majini
 
Huwa nablock mtu kama hana akili completely. Yani kama akichangia mada yoyote anakuwa hajaniongezea maarifa au kama anadeal na mada ambazo sigusi kabisa. Tofauti na hapo, mtu hata kama akiwa against me as long as kuna sehemu anakuwa smart naendelea nae. Na vilevile nachangia kulingana na tension, nikisema niwe smart 100% humu nitareply si zaidi ya mara mbili kwa siku na nitachangia mara moja kwa wiki. Mfano leo hakuna reply yoyote ningetoa. Sehemu za kuumiza akili nyingi zipo ila sio hapa.
Kila mtu ajibiwe kwa akili yake, kuna wengine hawawezi kuchangia lolote neno Ukraine lenyewe kalisikia 2022 sasa angalau umjibu kwa akili zake za apate amani.

Humu sasa kuna ushabiki, naweza kaa wiki sijachangia nikiignore notifications na nikirudi nakuta hamna kitu nimepoteza. Nilirudi tarehe 20 hadi 25 then nitoweke mpaka winter iishe kabisa hapo offensive ndio itakuwa kubwa na shifting of military balance itaonekana. Kuanzia March mwanzoni.
 

🤣🤣🤣🤣🤣 Huyu bingwa hatari sana dah! Eti "I hope you like my answer"
 
Mkuu, sivyo Super Power haikudumu hata miaka 10 dhidi ya Taliban? Yaani 1979 hadi 1989?
Wapi unapata miaka 20?
Super power iliwahi kukimbia Taliban mapema.
Au unammaanisha nani???
 
Mkuu, sivyo Super Power haikudumu hata miaka 10 dhidi ya Taliban? Yaani 1979 hadi 1989?
Wapi unapata miaka 20?
Super power iliwahi kukimbia Taliban mapema.
Au unammaanisha nani???
Sasa huyo si super power wa michongo kwa mujibu wenu hivyo hata akishindwa haina shida na wala hatushangai.

Tunaye mshangaa ni huyo super power wa kweli mwenye rundo la washirika aliye tumia zaidi ya $4 trion kupambana na kundi la wapiganaji wasio zaidi elfu 30 wasio pokea msaada wowote wasio kuwa na silaha zozote zaidi ya Ak47 na maguruneti wasio vaa hata viatu bali kanda mbili kwa zaidi ya miaka 20 na bado wakamshinda akakimbia.
 
Una pitia kwenye mateso makali sana kisaikolojia.

Yaani ww maoni yako yamejikita kwenye ushabiki alafu unawananga wengine kuwa ni madhabiki?
 
Kuna jamaa hum ndani alitabiri kutakuwa na reactions za idadi kubwa ya viongozi wa west watakao-react baada ya hotuba ya Putin.

Cha ajabu imekua ni kweli aloo, nmeskia bibi sii leo saa 12 asbh kelele za viongozi wengi akiwemo Old Man wanalalamikia baadhi ya kauli za Putin[emoji23]

Ila kweli huyu jamaa kawashika pabaya ase, yaani kama utani vile kumbe ni kweli Rusia ni very powerfull.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ila mgalala ni noma sana Kiongozi... Wazee wa kujichukulia Sheria mkononi.....
 
Jamaa yetu huyu tupunguze kumkazia asije akafanya maamuz magumu tukajuta sote humu ndan
Kuna maamuzi magumu kuliko haya aliyokwisha kuchukua?
Jamaa anaonekana elimu ya darasani anayo, historia anaijua vyema kwamba hawa mabeberu waliwatendea ukatili mkubwa sana babu na bibi zetu, wakachukua vyote vilivyokuwa vya thamani alafu mwisho wakatuita nyani huku wale ndugu zetu waliotangulia wakipewa jina la mizimu.
Tukija kwa upande wa Urusi yeye alitumia nguvu zake kutupigania na kutukingia kifua tusifutwe kwenye uso wa dunia.
Sasa mtu kama huyu hana maamuzi magumu tofauti na aliyokwisha kuyachukua sababu kuanzia ukucha wake mpaka unywele ni laana tupu mbele ya wazee wake waliotangulia hasa ukizingatia ukweli anauelewa...

Kibaya zaidi leo hii mabeberu haohao waliotenda na wnaoendelea kutenda ukatili juu yetu wanataka tuweke tamaduni zetu pembeni kisha tuhalalishe mapenzi ya jinsia moja alafu mtu huyuhuyu anakenua tu kama Malaya aliyeona bia 😏

Huyu bwana hakuna maamuzi magumu anayoweza kuchukua zaidi ya haya ya kujisaliti, kuwasaliti Waafrika wenzake pamoja na kuwasaliti wale wanaompa elimu ya kivitendo(Warusi).
 
Msaliti hana jema... Huyo ni wa kupuuzwa
 
Basi sawa andika barua uwasilishe hayo maombi yako ubalozi wa karibu wa Marekani. Ama anzisha jeshi lako ukampige North Korea au Russia
Mbona ninyi hamumuandikii barua Putin ampige Poland.... !!?? Si Kila mara mnakaa humu mkisema ajaribu aone ..vipi Mlimuandikia barua!!?? Mbona mwenzako anasema USA ampige Russia au N.K unasema aandike barua!?? Buraza umekuja kuwaje.....
 
March mwanzoni si ni Baada ya wiki ijayo tu kiongozi... Tukumbushane shifting of balance ikitokea.... Au basi ntakukumbusha.
 
Mkuu labda tunaweza kupata jiu tukiacha ushabiki na lugha ya aina hiyo?
Afghanistan ilikuwa wazi si rahisi kumshinda adui kama sehemu kubwa la taifa ni dhidi yako. Mrusi alijifunza, na Mmarekani alijifunza. Usipokuwa tayari kuua sehemu kubwa ya wananachi na hivyo kutishia wote wengine, upinzani utaendelea. Maana unapigana na taifa lenye watu wengi walio tayari kujitolea, ilhali wewe unatuma askari walio mbali na nyumbani
Siku moja unapaswa kupiga hesabu: je gharama za kuendesha vita zinalingana na yale unayopata au la?
Warusi walidumu miaka 10 tu, Marekani walifaulu zaidi kupata sehemu ya wananchi upande wao, lakini hatimaye nao waliona gharama zinazidi kila faida.

Sasa ni tena zamu ya Urusi kujifunza. Ni dhahiri Ukraine ina watu wengi walio tayari kujitolea hadi kifo. Warusi hawana idadi hiyo, ingawa wanaambiwa hadithi za kushambuliwa. Hapa wanapaswa kutumia hao wafungwa.
Kwa sasa Putin ana mamlaka zote huko Urusi, hata hivyo ana wasiwasi kuhusu raia zake, na hapo sababu kwamba hakutangaza "vita" bado anajaribu mchezo wa "SMO".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…