Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Sio masaa 96 Bali ni siku 96?Ulianza wiki,ukaja masaa 96 na Sasa unasema siku 96?
Kipi ni kipi,chutama tu,utaendelea kuumbuka!
 
I am a technical person si zungumzi mambo ya kubuni hapa. Raia wengi wa Ukraine wanazungumza kwamba wao waliona missiles za Urusi kwa macho yao zikivurumishwa na kupiga strategic targets karibu zote bila ya kipangamizi chochote, Mukraine mmoja tena mwanajeshi alisema kama kunamtu anasema eti missile za Urusi zilitunguliwa hiyo si kweli hata kidogo, labda dummy missiles lakini not a real one.

The truth of the matter ni kwamba siku ya tukio all Ukrainian air defense systems were redered ineffective ie ziligeuzwa kama toys baada ya Warusi kutanguliza kwanza dummy missiles kwa lengo la kusoma specs za Ukraine air defense systems taarifa hizo zinatumwa in real time kwa missiles za Urusi zinazo fuata nyuma ya Dummy missiles - missiles alisi za Russia zina uwezo wa kuingilia mawasiliano ya uongozaji wa missiles za Ukraine ADS baada ya kuzisoma - ndio maana ADS za Ukraine siku hiyo zilijikuta zinatiwa kiberiti kirahisi.
 
Ulisema Putin alisema anaipiga Kiev ndani ya siku tatu. Leta ushahidi acha manengo mengi yasiyoeleweka. Huna ushahidi piga kimya
Mkuu nilisema 'a week' kwa kuwa ulitaka usahihi ndio nikakuambia alitarajia within 96 hours, tatizo lipo wapi? Mkuu hakuna operation ambayo haina muda, na huwa operation huchukua muda mdogo na sio miaka. Nadhani sasa utaelewa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] bila shana na wewe unaitaji ile huduma pendwa ya kilainishi kama ilivyofanyiwa ndege yenu
 
Wewe ndio ovyo kabisa. Kweni Putin yupo peke yake.
 
[emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635]
America, send Ukraine more money and equipment, so they can make TikTok videos.

This is cringe…and people wonder why Ukraine is losing [emoji23]

#NATO #Biden #POTUS #Russians #Bahmut #China #Putin

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Dogo utakuwa huna kumbukumbu. Nashauri pitia tena uzi utaona mwanzo ulikuwaje. Nyie pro russia wa sikuhzi mmeibukia tu watoto wa juzi.

Mwanzo mwa huu uzi kulikuwa na wachambuzi manguli wa Pro russia wa jukwaa la kimataifa wakitamba na nguvu za Urusi sikuhizi wote wamekimbia mmeachiwa nyie wanywa kahawa vijiweni na waomba Mungu msojua lolote.
 
Tambua kuna kipigo Defensive na kipigo offensive. Mtu anaekuja mazima kukuangamiza haji kwa step bali anakuja kuharibu kila kitu.

Sasa Mrusi yeye anapigana kishakaji, sababu hataki kuiangamiza Ukraine. Hao US unaowasifia walienda kule na masilaha yote ya maangamizi.
 
Mkuu natambua kuwa wewe huna ushabiki uliopitiliza. Uhalisia wa jambo hili ni kuwa Putin aliwadharau sana wa Ukraine na ndio maana akaita ni operation lakini akakutana na nguvu ambazo hakutarajia, leo tupo mwaka wa pili hivyo huwezi kuita operation tena. Ila nasema muda utaongea.
 
Wewe unachotakiwa ni kuionea huruma tu ukrane maana itaaribiwa vibaya sana na kuijenga tena itachukua muda maana mpaka wakati huo uchumi wa ulaya na marekani utakuwa unapumulia mashine. HIFADHI HII KTK BICHWA LAKO, URUSI HAWEZI KUSHINDWA HII VITA KWA KIVYOVYOTE VILE
 
Hawana nguvu kiasi hicho, walitwangwa mpaka kibaraka wao US na NATO yake wakaona kitakachofata ni wataisha wote na nchi nzima itakuwa annexed na masilahi yao wanayotaka Ukraine watayakosa.

Ndio kuanza kupeleka masilaha, bila hivyo angeelemewa.
 
Mkuu ukweli ni kwamba Putin alikuwa anamtamani Ukraine sasa, hivyo sio kwamba Putin anapigana kishikaji, amejizatiti kabisa aitwae Ukraine, lakini hakujua kwamba naye ana rafiki ambao watamsaidia.

Kama uliona day 1 alivyoingia kwa mbwembwe akisindikizwa na vifaru kibao lakini vifaru viliishia kuangamizwa kwa kipigo cha mbwa koko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…