Mkuu kama nimemwelewa Medvedev sawa aliwatisha wakurugenzi wa viwanda kwa maneno ya Stalin. Maana yake: angependa kupata vifaru vipya 1500 kwa mwaka, anajua hawezi kupata, hivyo ana watisha kwa matumaini watapata njia kuongeza idadi kidogo.
Makadirio ninayoona kwa sasa ni hizi:
How quickly can Russia rebuild its tank fleet?
It has one tank factory, and is increasingly reliant on refurbishing old models
It has one tank factory, and is increasingly reliant on refurbishing old models
www.economist.com
na hii:
Russia has just one tank factory churning out 20 tanks a month, with demand outstripping production by a factor of ten, says report
Joshua Zitser Feb 28, 2023, 1:24 PM
Pamoja na kurudisha vifaru kutoka maegesho (vinavyohitaji matengenezo baada ya kukaa miaka mingi kwenye maegesho porini) wanatoa labda vifaa 90 kwa mwezi.
Ila vipuli kwa elektroniki ya kisasa ni haba. Elektroniki hasa za darubini zinaleta tofauti kama kamanda wa kifaru anaweza kulenga kilomita 2 au 4, na kama anaweza kuona chochote wakati wa usiku. Kwenye mapigano mara nyingi ni tofauti kati ya kifo na uhai.