Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hizi comedy haziishiii....
 
Hujui kwanini wanarudi nyuma,? Sio woga. Wakiingia vitani wanaingia kwa sababu..pia kuna itifaki ya NATO kwamba mwanachama mmoja akiwa vitani wote wanakua vitani, ..hivyo usa akiingia vitani ni kundi lote liko vitani. Urusi atakuwa na haki ya kupiga yeyote.
 
Soon Zelensky atatiwa mikononi mwa watesi wake , na huo ndio utakuwa mwisho wake.
 
Kuna mswahili apa anasema Atakufa njaa Mrusi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii ni sawa sawa una mke mmoja na unamkazia mkeo hutaki akuguse wakati mwisho wa siku mnaumia wote.

Vikwazo vyengine havifai!
 
Huge queues of customers lined up at McDonald's. Galip SV Liwagu
Your browser is not able to display this video.


Today is the last day of the restaurant in Russia. The network will temporarily close all of its 850 outlets due to a special operation in Ukraine, but will continue to pay the salaries of 62,000 employees.
 
Wewe jamaa ni very naive.

First of all vikwazo alivowekewa Russia sio vya kuleta matokeo kesho asubuhi ila vikwazo ambavyo vitamzoofisha in short and long term.

Russia uchumi wake kwa zaidi ya 20% unategemea mafuta, na kwa taarifa na wengi hawaijui ni kuwa USA na Canada ni wazalishaji wakuwa wa mafuta USA ni wa kwanza Duniani, Bei ya Mafuta haipangwi na taifa moja ndio maana Bei inapanda hata kwa mataifa ya yanayozalisha sana, ili kupunguza makali ya bei, Marekani huwa wanaakiba ya Mafuta, wenyewe wanaita Strategic oil reserve huitumia kipindi ambacho kuna emergency hasa kipindi hiki, Kwa taarifa yako USA wangekuwa wanatoa tu hii reserve wanaweza kuireplace Russia ndani ya mwezi kama muuzaji mkuu wa Mafuta.

Saudi Arabia ndio silaha kubwa ya marekani linapokuja suala la Nishati duniani, ni suala la muda tu Saudi Arabia ataongeza uzalishaji, Pia Marekani tayari amepata unlikely Ally kwenye hili naye Ni Venezuela, Venezuela ndio taifa lenye kiwango kikubwa cha mafuta kilichogundulika ila bahati mbaya hanufaiki nayo kwa sababu ya vikwazo (China na Russia hawajuzia kuathiriwa na vikwazo vy Magharibi)

Kuna watu wanasema Russia itaitumia China kukwepa vikwazo (at least watajaribu) wote wanaosema hivi hawajawahi kuwe kwenye Biashara za kimataifa ambazo zinahusiana na kuhamisha mitaji kati ya nchi na nchi, Kila mtu anayefanya Biashara na taifa fulani anaangalia kitu kinaitwa "Financial Risk of Doing Business", ahadi na ndoto hazishibishi hapa Pro Russia muelewe, Wiki Iliyopita Xiaomi kampuni ya China ilipunguza 50% ya Biashara zake inazofanya na Russia, na si Xiaomi pekee na hata Mabenki ya China yanakwepa kufanya miamala ya Benki za Urusi.

Unasema ticket za Ndege za Mataifa ya Ulaya zimepanda Bei, Hivi kupanda Bei na Shirika lako kufa Bora nini?
Kama hujui au kwa faida ya wengine Shirika la ndege la Russia ndege zake zote ni Airbus na Boeing isipokuwa 10 au 20 ndio zinaundwa Russia, hapo Boeing na Airbus wamejitoa kufanya biashara na Russia, this means they will not be able to get Spare parts and therefore lazima wapunguze Safari za nje au za ndege hizo, this means hadi Airline industry irudi kama kawaida sio zaidi ya miezi 12.
China mshirika wa Karibu wa Russia ndege zake karibu zote ni Airbus na Boeing, ameshindwa kumuungisha mshikaji wake (Hebu jiulize Kwa nini), au kama unajua maifa yanatumia Ndege za Russia hapa Africa yataje, now imagine kampuni inayoziunda ndege itakuwa na hali gani baada ya miezi 12?

Russia ana provide Rare Earth, Nickel na raw materials nyingi sana kwa Ulaya, na yeye hawezi kuuacha kuwauzia kwa sababu ndio msingi wa Uchumi wake, Kama hujui na kwa faida ya wengine Tanzania ina Deposit ya Nickel ambayo dunia nzima wakiacha kuchimba tutaweza kumuuzia kila mtu kwa miaka 30, na kambuni ya Kabambaga Nickel ni Kampuni ya Uingereza (Kwa usajili) so tutarajie speed ya ujenzi kuongezeka.

Umeitaja BRICS, hii sio formal wala informal alliance, kwanza wana tofauti za kimipaka, kisera, lengo lao lilikuwa ni kujaribu kuzichallenge IMF na WB ila hadi leo Nchi karibu zote za Africa na zinazoendelea zinakimbilia IMF na WB (Mfano Tanzania), hii ina imply Western financial Frameworks and Institutions are very strong kwa sasa labda itokee vita kubwa sana, that will destroy our civilazion.

Vita ni gharama na hii gharama ndio Silaha ya watu wa Magharibi
 
Kwani sisi Tanzania tuliiteka Kampala ndani ya muda gani? Maana tunaona unabwabwaja tu?
 
Uzuri wa Urusi historia yake inajulikana na uwezo na mshikamano wa watu wake unajulikana. Putin angeogopa vikwazo nina imani angeacha kufanya operation lakini kaona heshima na usalama wa warusi kwanza, ndio maana hakuna anayeandamana kupinga lolote na wote waliotaka kufanya hivyo waliwekwa mahali salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…