Lengo kuu limefanikiwa mrusi yuko uchi
Hakuna cha lengo kuu wala lengo dogo.
Haya ntakayosema hapa ni mahsusi kabisa kwa wana jamii forums ambao wafuatilia kwa makini mambo haya.
Tukio hili limejigawa katika sehemu mbili:
Kwanza, ni kwamba vijana wa mjomba Sam na vijana wa Mfalme (majasusi) wamekuwa kazini kwa muda mrefu na wakafanikiwa kumnunua Prigozhin.
Hizi habari ni za kijasusi kabisa na hamtozisikia kutoka katika vyombo vya habari vya nchi za magharibi.
Sasa majasusi wa Ukraine walitengeneza kitu chaitwa cell au kikundi cha majasusi wa aina ya komando Tamimu na wakawa tayari wako ndani ya Moscow wakitengeneza yale uloyaona jana.
Prigozhin akapewa kazi na akaambiwa akifika Moscow hizi "cells" zitafunguka na kutakuwa na mapinduzi na utakuwa mwisho wa Putin.
Lakini muda wote wa mpango wa vijana wa Mjomba Sam na vijana wa Mfalme walikuwa wakimuandaa Prigozhin na kumpa support ya yale alokuwa akiyasema kupitia mtandao wa Telegram, ambayo lengo lake kuu ni kuwafikia vijana wa kirusi ambao bado hawaelewei kinoendelea kuhusu vita ya Ukraine.
Vijana wa kirusi wa FSB, GRU na vikundi vingine kikiwemo kile cha Wachechen wakaanza kazi tangia juzi usiku na wale wote walokuwa kwenye hizi "Cells" wakatiwa pungu na sasa yasemwa wapo mahala wametulizwa.
Prigozhin akidhani jamaa wamsubiri Moscow akaanza na kuteka kituo cha komandia pale mji wa Rostov-on-Don. Hapa ndipo majeshi ya Russia yajiandaa na operesheni zote dhidi ya Ukraine. Prigozhin akaamuru vikosi vya Wager kuanza msafara kuelekea Moscow kupitia barabara kuu ya M4 ili kwenda kuwatia adabu Sergei Shoigu na Yalery Garasimov.
Lakini lengo lilikuwa ni lilelile la kufanya mengine yalopangwa na kuratibiwa na vijana wa mjomba Sam na vijana wa mfalme. Walipofika mji wa Voronezh wakaambiwa waendelee na msafara. Wagner wakaendelea na msafara wao na walipofika mji wa Lipetsk ambao ni kilomita 200 tu kutoka Moscow.
Wakati wote huu Putin na serikali yake na viongozi wote wa jeshi walikuwa wakiwaangalia Wagner kupitia kwenye mitambo ya satelite na baadae FBS wakaamua kumwambia Prigozhin kwamba cells zote zimevunjwa na jamaa wote wapo ndani hivyo amebaki peke yake na asubiriwa aje.
Raisi wa Belarus Lukashenko ambae binafsi ni rafiki wa karibu wa Prigozhin kwa miaka zaidi ya 20 akaongea na Putin na kuomba ampigie Prigozhin ili kutafuta suluhu na kumuokoa Prigozhin kwani ni dhahiri alikuwa akienda Moscow kuuliwa.
Kuona mambo yamebuma na kimenuka mjomba Sam akaanza kupiga simu Paris, Berlin, London na Kyiv na huku waziri mkuu wa Mfalme akikaa kwenye kikao cha dharura kujadili suala hili zito.
Lukashenko akaongea na Prigozhin na wakakubaliana amuombee msamaha kwa Putin na wayamalize kiutu uzima. Putin akakubali lakini akamwambia Lukashenko kwamba kwa sasa Prigozhin aende Minsk mji mkuu wa Belarus ili vumbi litulie kwanza.
Lengo ni kwamba Wagner iandikishwe rasmi kisheria bila Prigozhin kuwepo na vikosi vingine viandikishwe na viwe sehemu rasmi ndaniya jeshi la Russia na wapate maagizo yote kutoka wizara ya ulinzi. Lengo hapa ni kuondoa mambo alifanya Prigozhin na pia kuweka usawa katika masuala kama malipo na utendaji wa kazi.
Hivyo utaona hapa kwamba:
1. Jaribio la kutikisa serikali ya Kremlin limefeli vibaya sana na wale wote walohusika wapo chini ya uangalizi.
2. NATO na washirika wote wamepigwa changa la macho na hadi sasa wamefubaa hawafahamu waanzie wapi kuchora ubao wa mipango.
3. Habari hizi za kutikisa Kremlin zote zilijaa katika vyombo vyote vya habari vya nchi za magharibu kwasababu voyte viliambiwa na vilikuwa na taarifa na mpango mzima, hivyo walikuwa kama wakishangilia kuona Wagner aelekea Moscow bila kupingwa au hata kuuawa kwa silaha za aina zote.
Pili, Russia walikuwa wakifanya kitu chaitwa "drill" ili kuona kama wana utayari kwa kiasi gani endapo nchi itavamiwa.
Katika hili yawezekana Prigozhin katumiwa tu na baadae atapewa majukumu mengine baada ya vumbi kutulia.
Hivyo kinachiangaliwa kwenye hili ni uwezo wa kuhimili (resilience) kwamba Russia kaweza mumudu hili tukio na kulidhibiti huku pia akiendelea na SMO yake bila kutetereka.
Pia kuwaandaa wananchi wake na tukio lolote la kitishia usalama wa Russia kwa kuwaelekeza wananchi wachukue tahadhari, kutotembea hovyo mitaani na kuelewa kwamba nchi iko vitani na lolote laweza kutokea.
Na mwisho ni kutoa onyo kwa nchi za NATO, US na Ukraine kwamba Russia ipo tayari kwa kila idara na yaweza kujibu mapigo saa yoyote ile.
Hivyo tukio hili tatufundisha kwamba si kila tukionacho ni cha kweli na si kila tukionacho na kusikia ni cha kukipuuzia.
Ila kwenye hili, vijana wa mjomba Sam na mfalme wameachwa mbali sana.