Wale wanaohisi kwamba maelezo yamekuwa marefu sana, waniwie radhi tu!
Suala zima la "neo-Nazism" ni kama ambavyo nimelisema kwa kifupi hasa kuhusiana na chimbuko lake mpaka kufikia hivi sasa. Kama ni suala la kulizungumzia kwa ukamilifu wake, basi kero za watu kushindwa kusoma maelezo marefu zingekuwa kubwa zaidi kuliko sasa.
Nimetoa challenge ndogo ama changamoto kwa wote hasa wale wanaodhani kuwa itikadi hii ni tatizo linaloikabili Ukraine pekee. Maana kumekuwa na propaganda nyingi sana hasa kutoka upande wa Urusi kuhusiana na serikali ya Ukraine kwamba ni yenye sera za mrengo huo.
Ndio maana nikaongeza kuwa, naendelea kusubiri hoja kutoka maeneo mbalimbali zenye kuthibitisha madai hayo. Facts zilizopo ni kuwa, suala la neo-Nazism limeenea karibu bara zima la Ulaya katika vikundi vidogo-vidogo (minorities) huku katika baadhi ya nchi kukiwa na taasisi zenye mrengo huo na zenye majeshi kamili ambayo yametumika mpaka na serikali za nchi husika katika migogoro mbalimbali ya kimataifa.
Hoja yangu ama challenge ambayo naendelea kusisitiza ni: je, matumizi ya taasisi zenye mrengo unaoshabihiana na Unazi mamboleo katika mipango na shughuli mbalimbali za serikali, mfano, RIM ya Urusi ambayo nimeielezea hapo awali, nao ni Unazi mamboleo ama si Unazi mamboleo? Je, serikali husika zinajiendesha katika mrengo huo?
Ni challenge ndogo tu! Ngoja niendelee kusubiri hoja kutoka kwa wadau mbalimbali!
Vizuri, nimeyapenda maelezo yako. Japo binafs hua mgum sana kuweka hundred percent ya kitu flan ni sawa mpk nijiridhishe [emoji847][emoji847][emoji847]
Kwa mfano Issue ya Neo Nazism apo Ukraine mwanzo sikuwah kuiamini kabisa na nilikuwa nachukulia kama ni "Sababu" ka wengine walivofanya Iraqi na kwingineko kama lengo la kujipa legitimate ya kumshambulia mwingine....
Ila mpaka apa juzi nikakutana na hizi ntaziweka apa uzione zikanifanya kiasi kuamini kua Neo Nazi huenda kweli wapo Ukraine... Ziangalie hizi picha vizuri. Za wanajesh wanaopigana hivi sasa n hizo alama zao...
View attachment 2151629
Hii picha naizoom
View attachment 2151631
Ntaizom tena kisha angalia hyo alama ya kifuani...
View attachment 2151630
Then angalia na hii pia...
View attachment 2151632
Moja wapo tutaikuza il tuione vizuri
View attachment 2151634
Kisha tena katika kuikuza kuna alama ile ile kama y mwanzo
View attachment 2151633
Ambayo ni hii
View attachment 2151635
Sasa kisha nikajiuliza ka Zelensky n Myahudi na kwamba etiii "Ana chuki na wanazi kwasababu waliua babu zake" iweje alama za wanazi ziwepo kwe jeshi lake...
Za ziada ni hizi
View attachment 2151636
Na hii
Kisha kuhusu hao Nazis kuenea Europe nzima [emoji23][emoji23][emoji23] sina hyo taarifa wala uthibitisho wa kuenea kwao Europe nzima ko binafs siezi shiriki kulisemea hilo apa narejea ile kauli ya "No research no right to speak"
The same na hio MRI uliyoizungumzia sina habari nayo ko siezi ikataa wala kuikubali vile vile nakazia kwenye ile kauli ya "No research no Right to speak"
So siezi nikazungumzia kitu ambacho sikijui kiundani labda nikikifatilia nikakipatia ujuzi nitarudi tena kukizungumzia...
Mwisho labda niseme t na huu ni mtizamo wangu... Ambacho nakiamin taarifa nyingi sana hasa kwe ulimwengu wa siasa ziko much twisted kiasi cha kujua ipi kweli ipi sio ni ngum mno hasa ukiwa umeegemea upande mmoja...
Nachoamin hakuna Politicians msafi, wana mambo mengi sana nyuma ya pazia. Na yale wanayoyatoa huyatoa vile namna wanavotaka yapokelewe.