Ndiyo, naona kuna busara kama serikali ya Ukraine iko tayari kusogea kiasi. Ila naweza kuwaelewa kama hawakuwa tayari kukubali moja kwa moja hadi ibaonekana Urusi haiweza kutenda jinsi inavyotaka.
Ungeamini wewe ahadi yoyote ya Putin ?????
Urusi iliahidi tayari kuheshimu mipaka ya Ukraine na kuitetea katika mkataba wa 1994. Matokeo yake tunaona.
Nato haiko Ukraine, haikuwepo Ukraine na imekataa mara kadhaa kupokea Ukraine.
Ukraine imepata hasara kubwa (kwa sheria ya kimataifa Urusi inatakiwa kulipa fidia).
Aliyepoteza vita ni Putin, hata akifaulu kuteka Kiev. Maana ameharibu nchi yake Urusi, amerudisha uchumi wake miaka mingapi, amefikisha mamilioni ya wananchi wake kwenye umaskini, Pia ameonyesha udhaifu wa jeshi lake (ambayo hakuna aliyetarajia tokeo hili).
Huyo raisi wa Ukraine ni mpumbavu hata nyinyi mnao muunga mkono ni wale wale.
Ni upumbavu mkubwa kujifanya unasimamia unacho kiamini alafu badae unakuja kukikana kile ulicho kiamini huku ukiwa umesha pata maafa makubwa sana.
Tangu mwanzo takwa la Urusi lilikuwa ni hakikisho la Ukraine kutojiunga na NATO lakini viongozi kwa kujazwa vichwa na wamagharibi wakawa wanatoa kejeli kwa Urusi, sasa hivi maelfu ya watu wamesha kufa watu wamepoteza makazi yao mamilioni wamekuwa wakimbizi ndo wana kuja kubali yale yale waliyo kataa ambayo ndio yame sababisha maafa yote upumbavu wa kiwango gani huu?
Eti Urusi ndo atakuwa amepoteza?
Hivi unajuwa kanuni za kushinda vita vita au unaongea tu ili na ww uonekane umechangia ?
Kanuni ya kwanza ya kushinda vita ni kutimiza lengo lililo kupeleka vitani na lenge kuu la Urusi kwenda vitani ni kuizuia Ukraine isijiunge na NATO ina maana kama Ukraine imekubali kutojiunga na NATO ni ushindi mkubwa kwa Urusi.
Eti jeshi la Urusi ni dhaifu?
Ngoja nikwambie kitu kimoja mpaka jeshi fulani liitwe jeshi lenye nguvu ni vigezo vingi sana vina angaliwa, hata Urusi ikishidwa vita nchini Ukraine bado lita baki kuwa jeshi lenye nguvu kubwa duniani.
Marekani kapigana vita nyingi na kushindwa lakini hilo halijawahi kuindoa kwenye nafasi yake ya kuwa taifa lenye nguvu za kijeshi duniani.
Marekani kapigana vita na Vietnam kwa miaka 10 lakini haikufanikiwa hata kuteka kijiji.
Israel kasha pigana vita na hamas zaidi ya mara 3 akijaribu kuidhibiti gaza lakini kashindwa wakati hamasi haina hata kifaru wala mzinga hata mmoja ,lakini hilo haliondoi ukweli ya kwamba Israel ni taifa lenye nguvu mashariki ya kati.
Ya kwamba Urusi imeharibu uchumi wake?
Juzi benki ya dunia inesema kutokana na vikwazo Uchumi wa Urusi uta pungua kwa asilimia 10.
Wakati Uchumi wa Ukraine mpaka sasa imesha poteza aslimia 35 ya Uchumi wake na kumbuka vita havijaisha ina maana vita ikienda wiki 2 zingine itapoteza zaidi ya hapo, bado huja weka miundo mbinu ya mabilion ya $ iliyo haribiwa, bado raia walio uawa, bado mamilioni walio poteza makazi na mbaya zaidi inaenda kukubaliana na matakwa ya Urusi sasa nani atakuwa amepoteza?
Sent from my TECNO BB4 using
JamiiForums mobile app