RTI
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 2,422
- 7,173
Tatizo sio kusimamia unacho amini, tatizo ni pale unaposhindwa kusimamia unacho amini baada ya kupata madhara makubwa.Wananchi wamesimama na raisi wao kuamua walichoamua. Heshimu tu hilo. Ndo maana hawakuandamana kutaka atoke madarakani ila walichukua silaha na walioogopa waliondoka nchini. Sikia cardless, kama jinsi ambavyo unavyoona kuwa ni sahihi nchi ya Urusi kuivamia Ukraine basi pia waelewe Ukraine kuchukua maamuzi ya kukataa kuwa chini ya Urusi. Kuwa neutral, usitake kulazimisha.
Mkuu mm naona huyu raisi wa Ukraine ni mjinga kwa sababu madai ya Russia tangu mwanzo yalikuwa ni hakikisho la kimaandishi la Ukraine kutojiunga na NATO na ndicho kilicho sababisha Russia inaivamia Ukraine kitu ambacho kili kataliwa na viongozi wa Ukraine.
Lakini sasa hivi wanataka kukubali tena matakwa ya Urusi kutojiunga na NATO wakati maelfu ya waukrine wamesha uawa na mamilioni wameikimbia nchi yao miundo mbinu walio ijenga kwa miaka mingi ikiharibiwa vibaya ,
Sasa kama walikuwa wana jua hawangeweza kusimamia kile wanacho kiamini siwange kubali mapema ili kuokoa maelfu ya maisha ya watu na miundo mbinu?
Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app