Mkuu mbona walalamika sana hivyo???
Faida ya kutumia hiyo silaha wanaijua warusi wenye kombora lao ambao ndio waliopiga na kuangamiza ngome hiyo ya kijeshi ya chini ya ardhi.
Russia wana silaha/makombora mengi tu, wanachagua ipi ya kutumia wapi, lini na kwa nini (sababu wanazijua wao wenyewe).
Yaani kombora walidizaini na kulitengeneza warusi wenyewe, halafu wewe ambaye hujui hata chemistry ya kombora hilo wataka kuwafundisha walitumie wapi, na lini! Hayo nayo maajabu ya mwaka!
Nchi zote za NATO ikiwemo US zafahamu fika kuwa Russia ana makombora ya haipasoniki, na aliyatesti hadharani-sio chini ya uvungu-na aka-publish hilo. Sasa hizo stori za kuwa asilitumie awafiche NATO zinatoka wapi? Utakaaje na kombora kama mdoli tu (ambalo ni ruhusa kutumika) halafu usilitumie vitani kujua uhalisia wa nguvu yake ktk kuangamiza nguvu za maadui ktk uwanja wa vita?
Hebu muache Russia atesti uwezo makombora yake kwenye field, kapata uwanja wa kivita wa kutestia.
Btw: Mie sio msemaji wa jeshi la Russia
View attachment 2157318