Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kitu cha kinyama sana US walichofanya Iraq na other countries inasikitisha sana unamnyonga 70s years old female and 5month old child unyama uliopitiliza afu unalipua ili ijulikane walikufa kwa bomu [emoji174]anyway hiyo video inasikitisha,,,afu kutwa wanaongelea human rights
 
Urusi sio Libya,sio Iraq,sio Syria,sio Afghanistan,sio Panama.
Urusi ni tajiri ina technolojia na Ina nguvu za kijeshi.
Kuiwekea vikwazo n hi yenye viwanda vya kila kitu ni kujichosha TU.
 
Uchumi kutikisika lazima japo ni ngumu kulinganisha pande mbili. Wao na mlengwa wa vikwazo. Tukirudi nyuma tunaelewa kua Nishati ni "uti wa mgongo" wa uchumi...

Na kwa hapa tunaona Germany anakuwa mkali zaidi ukizingatia kwa Europe yeye ndio number 1 kwa uzalishaji akifuatwa na Italy, na yeye anato about about 5.3% of Global Manufacturing output.

So tunaona mbali na matumizi ya kawaida ya Raia Sekta ya Viwanda inatumia zaidi nishati nchini kwake kukurupuka kufanya maamuzi kutapelekea gharama kubwa za uendeshaji ambazo zitapelekea pia kufungwa kwa viwanda...

Athari yake inaenda hadi kwa raia wa mwisho upande wa ajira. Kupanda kwa gharama za usafirishaji kunapelekea pia mfumuko wa bei kwenye bidhaa so lazima uchumi wake uumie.

Tukiacha ushabiki wa kwenye hii thread kama huwa unafatilia taarifa tofauti tofauti nje ya mlengwa wa kisiasa nazan utakuwa na mtizamo mwingine juu ya haya yanayoendelea...

Kingine [emoji23][emoji23] Umeona Hungary alivokuwa mkali kuhusu Kutemana na Oil n Gas supply kutoka Russia?

Kwenye vikwazo vitamteteresha kiasi chake Russia ila wamshukuru Muumba wao kwa kuwajazia alot of natural resources kwenye ardhi yao... Nawaza wangekua kama nchi zingine ambazo zinategemea kujiendesha kwa resources hasa zile muhim nje ya mipaka yake hivi sasa tungekuwa tunazungumza mengine...
 
Hata kama ichukue 20,lakini wameweka heshima ya kulinda Nchi yao na mwisho wa siku Nchi itajengwa lvizuri tu akini wakati huo kuna Russia amerudishwa nyuma ki uchumi vile vile tena siyo kidogo.Ngoma droo.

Itajengwa na hao hao wenye ardhi yao(URUSI) au sio kamanda!! Na itakua chini ya himaya ya (URUSI) au sio!
 
"Bila shaka" ni mahali papesi (Kiswahili sanifu hivyo?) pa kuanza, lakini mahali pagumu pa kufika! Kiuchumi Urusi ni kibete ukilinganisha na Marekani.
Maana ya vikwazo ni: unakataa kufanya biashara na yeyote anayefanya biashara na yule aliye chini ya vikwazo, unakataa kununua kutoka kwake au kumwuzia. Anayefanya biashara naye haruhusiwi tena kununua au kuuza kitu ndani ya nchi yako.
Pamoja na marafiki wa Urusi ambao si wengi hakuna uwezo wa kutisha uchumi wa Marekani.

Tazama nchi zilizopinga azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kukemea uvamizi wa Ukraine, jumla ni tano tu: Urusi, Belarus, Korea Kaskazini, Eritrea na Syria. Mataifa 141 walikubwali azimio. Nchi 35 hazikusimama upande mmoja. Kati ya hizo 35 kuna nchi muhimu kama China, Uhindi na Afrika Kusini.
Kwa sasa ni China pekee inayoweza kusumbua Marekani. Ila ningehisi kwa gharama kubwa sana kwake yenyewe.

Pamoja na hayo; si rahisi kuwa na marafiki kwa nchi ambayo inavunja Kanuni Kuu ya sheria ya kimataifa: usilazimishe kubadilishwa kwa mipaka kwa njia ya vita na mashambulio.
Hatua hii kwa sasa ni Urusi pekee duniani (nimesahau mtu??) - Marekani katika vita zote alizoendesha tangu miaka 120 haikugusa mipaka ya nchi nyingine, haikujaribu kutwaa sehemu ya Kuba au Afghanistan au Irak.
 

Russia wanapoint maeneo muhim tu
 
[emoji298]️President Putin declares that European payments for gas supplies will be switched to rubles as soon as possible

[emoji298]️US dollar moves back below 100 rubles on Moscow Stock Exchange

Subscribe to RT t.me/rtnews
 
Umeshasahau kama kawapa wakurdi wa irak eneo wanajitawala kama nchi na anajenga military base ambayo juzi ilitwangwa missile na iran?
 
Haya makubaliano mbona Ni ya tarehe 17 March, na mapambano bado yanaendelea.

Inamaana yaligoma kufikiwa muafaka au vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo shirika la ndege la Urusi hiyo nafasi ya pili Kidunia inashikilia kwenye kipengele kipi,embu tujuze.
Ukubwa wa Aeroflot unaelekea kupungua haraka. Maana wanatumia hasahasa ndege za Airbus (Ulaya) na Boeing (MArekani), pamoja na Sukhoi chache za Kirusi. Hawapati tena vipuli wala usaidizi wa kitaalamu katika matengenezo.
Nimeona wanatafakari kufufush modeli za zamani za Kisovyeti aina ya Ilyushin - ambazo ni tekinolojia ya 1970s na 1980s. Baada ya anguko ka ukomunisti walikuwa na sababu za kutoendeleza ndege hizo na badala yake kununua ndege za kimagharibi.
Kama vijana wa Wikipedia wamefanya kazi sawa, hizi ni ndege za Aeroflot za 2021:
The Aeroflot passenger fleet consists of narrow-body and wide-body aircraft from six aircraft families: the Airbus A320, the Airbus A330, the Airbus A350 XWB, the Boeing 737, the Boeing 777, and the Sukhoi Superjet 100. As of September 2021, there are 202 passenger aircraft registered in the Aeroflot fleet. (Chanzo: https://www.aeroflot.ru/us-en/about/plane_park)
 
Wanataka kushindana na walikotoka[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ushabiki URusi wanaweza kupitisha ndege Zao hata Marekani achilia Poland.
Marekani ndio theoretically (not proved) wana uwezo wa kuingiza ndege anga la Urusi kwa vile wanadai wana stealth jets kama F-35, F-22 na bombers kama B-2 na hii mpya B-21 Raider.
Na historia inaonesha waliwahi fanya hivyo ile incidence ya U-2 Dragonlady spy plane ambayo ilikuwa ikatishe anga la Urusi kufanya uchunguzi ila ikadunguliwa angani. Marekani walizoea anga la Urusi ni uchochoro ukipita juu sana hawana interceptor wala radar za kukuona. Kumbe muda si mrefu Urusi ilikuwa imezindua ground to air missile mpya yenye uwezo ndio wakadondosha ile ndege. Hiyo ilikuwa miaka ya 1961 sijui 1960.

Baadae miaka ya 1980s kuna dogo kutoka nchi jirani hapo aliendesha ndege ndogo kama hizi Cesna akatua Urusi tena Red Square pale kupinga vita baridi.

Hakuna incidence ambayo ndege ya adui iliwahi ingia anga la Marekani, hakuna adui mwenye hizo ndoto za mchana. Ndio maana long range bomber ya Urusi Tu-160 Blackjack ina cruise missiles kama Raduga tangu zamani, wakati long range bombers za Marekani kina B-52, B2B Lancer na B-2 Spirit hazizingatii sana cruise missiles zenyewe zina mabomu zaidi.
Marekani inaweza ona ndege zote za Urusi zikiruka, in incidence of war. Airbases zinajulikana, ndege sio stealth, zenye range kubwa lazima zitoke airbase haziwezi toka kwenye airstrip, satellite za kijeshi za Marekani picha zake hatupati kiraia ni marufuku ila zina uwezo mkubwa wa kuona airbases za Urusi, kama picha za satellite za private companies tunaona na ndege zinaonekana sembuse za jeshi.
 
[emoji298]️President Putin declares that European payments for gas supplies will be switched to rubles as soon as possible

[emoji298]️US dollar moves back below 100 rubles on Moscow Stock Exchange

Subscribe to RT t.me/rtnews
Ha ha ha ......
Putin mtu smart Sana aisee.

Kwaiyo watalazimika kununua kwa rubee, afu watafuata exchange rate za benki kuu ya Russia.

Anaetaka anunue, asiyetaka aache[emoji1][emoji1][emoji1]

Hii ndo inaitwa BOSS HANUNIWI[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa marubani wa hizi Helicopter wana eject kupitia wapi maana kama ni juu si watachinjwa na mapanga?
Hili swali common sana, kuna rockets zimefungwa kwenye jetpack ya kurushia huyo rubani juu. Kwenye jet za kawaida hizo rockets zinafyatuka na kupasua ile canopy then jet ya ejection seat inafyatuka baada ya vioo kuondoka.

Kwenye Ka-52 kuna mechanism sikumbuki kama kuna vimilipuko kwenye base ya rotor au kitu gani, ila ile mechanism inakata zile rotor zinadondoka kisha mengine kama kwa jet aircraft. Hapa Kamov walifanya kitu revolutionary
 
Taiwan awe makini asifanye kitu ambacho kitamshawishi Putin aishawish Beijing kuivamia Taiwan nayo beijing ikaingia mkenge coz Taiwan ni jicho la Washngton Far East
China hawezi Fanya huo upuuzi kama anajipenda.Putin kiaina ametengwa mpaka na China,rafiki wa karibu🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…