Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

Kuwafukuza akina mdee haiwezi kuyumbisha chadema bali itaiwezesha chadema kuheshimika zaidi Duniani

Serikali imetumia nguvu kubwa Sana kuhakikisha upinzani hawaingii bungeni eti wanakwamisha maendeleo,ajabu leo inatumia nguvu kubwa kuhakikisha upinzani wanaingia bungeni. Tukisema serikali inavuta bangi tunakosea?
 
Spika wa bunge Job Ndugai amemtaka katibu mkuu wa CHADEMA akajifunze namna ya kuwa katibu mkuu kwa Bashiru Ally ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM...
Ndugai kisha sahau yaliyowapata Membe, mzee Makamba, mzee Kinana na wengine waliotangazwa hadharani na Bashiru huyuhuyu anaetaka akamfundishe Mnyika jinsi na maana ya kuwa katibu mkuu.

Amesahau jinsi alivyotambua kwa kasi ya mwanga maamuzi ya genge la Prof Lipumba wa kuwafukuza uanachama wabunge wa viti maalum wa CUF kambi ya maalim na yeye kuidhinisha na kutambua wabunge walioteuliwa na genge la Prof Lipumba.

Alidiriki hata kupuuza ukweli kwamba wabunge waliofukuzwa walikuwa na kesi mahakanani ya kupinga kufukuzwa kwao. Hata kesi ilipoisha na mahakama kuamua kuwa kufukuzwa kwao haikuwa halali bado Ndugai alishikiria kuwatambua hao walioteuliwa kiharamia.

Ni Ndugai huyuhuyu aliyemwambia Cecil Mwambe aendelee kuhudhuria vikao vya bunge pamoja na kutangaza hadharani kuwa yeye amejivua uanachama wa chama kilichomdhamini. Ndugai anatunga, kutekeleza na kutetea kanuni anazotunga mwenyewe kulingana na mazingira.
 
Ila wachache kutaka kuonewa katika kiwango hiki kabla uliwahi kuona?
Mpaka sasa sijaona aliyeonewa. Kama wamekwenda kihalali it's well and good. So far kuna utata hasa baada ya Katibu Mkuu kuwakana.

Kama wewe huoni tatizo hapo then it's fine. No need to continue with our argument.
 
Ndugai, ebu tueleze utawalindaje?
 
Hayo sio mambo ya CHADEMA tu,katika hilo sakata bunge linahusika moja kwa moja, hivyo yeye kama spika anayomamlaka ya kusema kitu.
[emoji23] [emoji23] Mnatapa tapa sana, mfano akina Lijualikali na Mwembe walivuliwa ubunge na vyama vyao but Spika akawabakisha bungeni, kinyume kabisa na katiba ya nchi. Lakini nyie, very unfortunately you don't see that as problem, yaani mnafurahia mhimili mmoja ukivunja katiba ya nchi openly. Sasa huwa najiuliza tatizo ni umbumbumbu au kushikiwa akili?
 
Me nafikiri mbumbumbu ni wale waliomuamini mdee na Mbowe kupita kiasi.
 
Ndugai bana; kwa hiyo unamtaka Mnyika ajifunze namna ya kutofuata katiba na taratibu cha chama badalanyake aje kujifunza wizi wa kura..bac saw.
 
Mkuu mbona unaongea pumba hivyo? Adhabu ya hao ni kufukuzwa tu na so vinginevyo halafu endapo chama kitafutwa basi nakifutwe tuanze at scratch kuliko kubaki na chama kisichokuwa na wanachama wenye di

Demokrasia gani hiyo?
Utajengaje Demokrasia kidikteta halafu uilaumu CCM?

Aisee ,Chadema hakijajua kuwa kila ni chama cha siasa na siasa zina michezo mingi ya kupambana na mshindani wako?
Hivi huoni kuwa CCM imeona kosa kubwa walilofanya la kuvuruga uchaguzi lakini nafasi 19 ni za kikatiba na kugoma kuzichukua ni kuvunja katiba ya nchi . Chadema inabidi muwaze mbali zaidi ya jaziba ambazo hazina tija yoyote.

Yana kuna chama tena kinataka kuitoa CCM mdarakani lakini kina hulka ya kuwaumiza watu kwa kufukuza fukuza badala ya kulinda katiba ya nchi?

Unadhani sasa hivi itakua ni rahisi kuunda chama kingine kirahisi?
Unajua nguvu waliyotumia BAWACHA kukijenga chama kikakubalika kwa akina mama mpaka vijijini halafu muwafukuze kwa hasira tu .

Hivi mziki utakaotokea wa kuvuliwa nguo Chadema endapo watadukuzwa viongozi 19 kwa pamoja utakua ni mdogo au ndio kukiua kabisa chama na ofisi kufungwa baada ya kufutwa?
Nani atanufaika kama chama kitafutwa?

Kwa nini tusisubiri bunge likianza ili tuone watakavyokiwakilisha chama na kutangaza Sera zake mbadala kuliko kuwafukuza ili tu waishi kwa tabu mitaani wakati wana familia?
Mbona waafrika mna roho Mbaya hivyo ? Roho mbaya za kuona wenzenu wanateseka tu kwa sababu ambazo ungesamehe wala usingedhurika chochote?
 
Utaratibu wa kibunge iko mikono mwako fanya upendavyo
 
Mwambieni huyo mzee hata afanyaje hakuna $900 m anajisumbua tu
 
Watanzania wengi hasa wanawake weikubali chadema kwa sababu ya hao wanawakeajasiri.
Wewe sio mzima, unamjua Zito Kabwe na Slaa enzi wako Chadema kazi yao unaweza kuilinganisha na hao watoto?
Kuwafukuza Wabunge walioapishwa kikatiba ni kosa kubwa sana.
Wanafukuzwa kwa sababu wamekiuka matakwa, itikadi na katiba ya chama na sio katiba ya nchi.

Litakuwa kosa kwenu ccm.
Adhabu ya kuwafukuza watu waliotekeleza matakwa ya Kikatiba ni Kukifuta hicho chama.
Kwa mujibu wa sheria ipi?
Na adhabu ya mwanachama kuvunja katiba au itikadi za chama cha Demokrasia na Maendeleo ni ipi?
Nitahakikisha Chadema inafutwa kwenye Orodha ya vyama vya siasa endepo hao wabunge watafukuzwa ili eti wapoteze sifa ya kuwa wabunge.
Bahahahahahahahahahaha! Huna uwezo huo narudia huna! Chadema ipo kabla hujawa na akili timamu au pengine kuzaliwa kabisa.
Hivi Nyie Chadema bado mnataka kuwaumiza Watu kama CCM.
Ungeenda ofisi za chama ukawaulize.
Wabunge 20 tena wanawake kuwafukuza kwa sababu tu hawakishirikishwa kwenye nafasi za maamuzi ya kwao kama wanawake ni kuua Demokrasia.
Ulichokiandika hapa unakielewa vizuri?
Chama hakijaandika majina ya wabunge wa viti maalumu kwenda NEC hayo majina kaandika nani?

Na baada ya kutajwa majina hayo msimamo wa Chadema kama chama ulikuwa ni upi?
Chama Chenye katiba na viongozi wanaopingana na matakwa ya katiba ya nchi ni chama cha Kigaidi kinapaswa kufutwa haraka sana.
Katiba ya Chadema inasemaje dhidi ya huu usaliti au ukiukwaji wa itikadi zake?

Kumbuka Chadema ina itikadi huwezi kuwa mfuasi wa chadema kama una itikadi za kimama za kununuliwa, kuhongwa ama kudanganywa na Katiba yake imethibitishwa na msajili wa vyama.

Tueleze matakwa ya katiba ya nchi yaliyovunjwa?
Mbowe kuwa makini na maamuzi yasoyojali maslahi ya Taifa la leo na kesho.
Maslahi ya taifa au maslahi ya ccm?
Uwepo wa watu wasio heshimu viongozi, itikadi na katiba ya chama chamani una umuhimu gani kwa CHADEMA?
Makamanda Mdee na Bulaya wameshapata ajira yao kwa miaka mitano hivyo busara itumike wabaki kwenye Chama ili chama kinusurike kufutwa.
Labda kitafutwa na bibi yako.

Wameteuliwa na uongozi bila wao kujua na majina yepelekwa bila wao kujua kwa hiyo wao hawana makosa. Aliyepeleka majina ndiye wakuhojiwa.
Aliyewateua ni nani? Na CHADEMA inasemaje juu ya huo uteuzi? Kama uchaguzi tu hawautambui hao wateuliwa wametoka wapi?
 
Duh ukisikia watu kuvunja ngome ya chama pinzani mpaka wanachanganyikiwa ni hivi..
Wako hoi
 
Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.
Akafundishwe lipi kwa Bashiru? Kuimba mapambio? Kuamuabudu Jiwe? Lipi
 
Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.
Akafundishwe lipi kwa Bashiru? Kuimba mapambio? Kuamuabudu Jiwe? Lipi?
 
Mnyika hakutoa hukumu. Alirudia mara mbili mbili kuwa kamati kuu ndio itakayoamua.

Mnyika hakumfokea mtu, alirudia mara nne nne kufafanua taratibu za mbunge VM kuchaguliwa....
Huyu spika ameanza vibaya Bunge hili kama alivyomaliza vibaya Bunge lile dhaifu.
 
Mhe JOB , ukiwa chini ya mama Makinda ulionekana uko makini mno. LKN HII LEO UMEKUWA NI MMOJA WA VIONGOZI WA HOVYO KUPITA MAELEZO, hivi kama wewe ndio kiongozi wa kuwasimamaia watunga sheria za NCHI. unakuwa mbele kuzivunja , sheria , kanuni nk. HUONI KUWA WEWE NDIO CHANZO CHA KUIPELEKA NCHI KUSIKOJULIKANA.......?

BUNGE NI MUHIMILI UNAOJITEGEMEA , MAHAKAMA HALIKADHALIKA . lkn toka awamu hii ya TANO iingie madarakani mzee JOB umelifanya bunge kuwa ni sehemu ya mapambono yasio na mwisho kwa yeyote yule aliye na mawazo tofauti na wewe pamoja na wakubwa wenzako. umetoka kabisa ktk misingi ya kuisaidia NCHI hii kupiga hatua bali uanturudisha 1977. ila kubwa ambalo nakuomba usilisahua fanya yooote ila iko siku utakufa na historia itakukumbuka. unasahau kabisa kuwa kuna wajukuu zako ambao wanahitaji kuishi kama wewe kwenye NCHI yenye misingi mizuri ya uongozi.

NCHI MNAIPELEKA KUBAYA KWANI KIZAZI HIKI SIO KILE CHA NDIO MZEE . (R.I.P. MZEE SITTA)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…