Watanzania wengi hasa wanawake weikubali chadema kwa sababu ya hao wanawakeajasiri.
Wewe sio mzima, unamjua Zito Kabwe na Slaa enzi wako Chadema kazi yao unaweza kuilinganisha na hao watoto?
Kuwafukuza Wabunge walioapishwa kikatiba ni kosa kubwa sana.
Wanafukuzwa kwa sababu wamekiuka matakwa, itikadi na katiba ya chama na sio katiba ya nchi.
Litakuwa kosa kwenu ccm.
Adhabu ya kuwafukuza watu waliotekeleza matakwa ya Kikatiba ni Kukifuta hicho chama.
Kwa mujibu wa sheria ipi?
Na adhabu ya mwanachama kuvunja katiba au itikadi za chama cha Demokrasia na Maendeleo ni ipi?
Nitahakikisha Chadema inafutwa kwenye Orodha ya vyama vya siasa endepo hao wabunge watafukuzwa ili eti wapoteze sifa ya kuwa wabunge.
Bahahahahahahahahahaha! Huna uwezo huo narudia huna! Chadema ipo kabla hujawa na akili timamu au pengine kuzaliwa kabisa.
Hivi Nyie Chadema bado mnataka kuwaumiza Watu kama CCM.
Ungeenda ofisi za chama ukawaulize.
Wabunge 20 tena wanawake kuwafukuza kwa sababu tu hawakishirikishwa kwenye nafasi za maamuzi ya kwao kama wanawake ni kuua Demokrasia.
Ulichokiandika hapa unakielewa vizuri?
Chama hakijaandika majina ya wabunge wa viti maalumu kwenda NEC hayo majina kaandika nani?
Na baada ya kutajwa majina hayo msimamo wa Chadema kama chama ulikuwa ni upi?
Chama Chenye katiba na viongozi wanaopingana na matakwa ya katiba ya nchi ni chama cha Kigaidi kinapaswa kufutwa haraka sana.
Katiba ya Chadema inasemaje dhidi ya huu usaliti au ukiukwaji wa itikadi zake?
Kumbuka Chadema ina itikadi huwezi kuwa mfuasi wa chadema kama una itikadi za kimama za kununuliwa, kuhongwa ama kudanganywa na Katiba yake imethibitishwa na msajili wa vyama.
Tueleze matakwa ya katiba ya nchi yaliyovunjwa?
Mbowe kuwa makini na maamuzi yasoyojali maslahi ya Taifa la leo na kesho.
Maslahi ya taifa au maslahi ya ccm?
Uwepo wa watu wasio heshimu viongozi, itikadi na katiba ya chama chamani una umuhimu gani kwa CHADEMA?
Makamanda Mdee na Bulaya wameshapata ajira yao kwa miaka mitano hivyo busara itumike wabaki kwenye Chama ili chama kinusurike kufutwa.
Labda kitafutwa na bibi yako.
Wameteuliwa na uongozi bila wao kujua na majina yepelekwa bila wao kujua kwa hiyo wao hawana makosa. Aliyepeleka majina ndiye wakuhojiwa.
Aliyewateua ni nani? Na CHADEMA inasemaje juu ya huo uteuzi? Kama uchaguzi tu hawautambui hao wateuliwa wametoka wapi?