Spika Ndugai: Nitawalinda wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA kwa nguvu zote, Mnyika akajifunze kwa Dkt. Bashiru kazi za Katibu Mkuu

Hayo sio mambo ya CHADEMA tu,katika hilo sakata bunge linahusika moja kwa moja, hivyo yeye kama spika anayomamlaka ya kusema kitu.

Aombe kiti kamati kuu saa mbili. Ahudhurie kabisa.
 
Spika Ndugai amesema kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao naye atafanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndugai amesema wabunge 19 wa CHADEMA wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu na kuwafokea kupitia vyombo vya habari.

Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.

Chanzo: TBC Aridhio

Maendeleo hayana vyama!

NOTE: Ilishadokezwa tangu juzi kuwa Ndugai ana mkakati huo > Ofisi ya Spika ‘kuwalinda’ wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA - Imevuja!

Kama kawaida yao anaweza kutumwa mamboleo kudai huu mkutano hauna kibali kuuzuia kufanyika.

Lini wonders ziliwahi kwisha udanganyikani?
 
Spika Ndugai amesema kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao naye atafanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndugai amesema wabunge 19 wa CHADEMA wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu na kuwafokea kupitia vyombo vya habari.

Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.

Chanzo: TBC Aridhio

Maendeleo hayana vyama!

NOTE: Ilishadokezwa tangu juzi kuwa Ndugai ana mkakati huo > Ofisi ya Spika ‘kuwalinda’ wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA - Imevuja!

Ndugai boya kwelikweli. Hajajibu hoja. Ameropoka Kama yupo chooni.
 
Huyu Ndugai ndio kawaharibia kila kitu, sasa waondolewe Chadema wakapewe ulinzi wa Ndugai.
 
Kuwalinda hao wabunge ni kuisaidia CHADEMA, kwa sababu kuna ubabe wa wanaume wachache wabinafsi dhidi ya akina mama. Mbona wao wanaume walipotangazwa 2015 hawakutambua uchaguzi, hawakutambua matokeo ya uraisi lakini walikwenda Bungeni? Kwa nini Leo wawanyanyase akinamama.
Wanajua kwamba wale wanawake sasa watakuwa na pesa kuliko wao na hivyo hawataweza tena kuwaendesha watakavyo.
 
Kuwalinda hao wabunge ni kuisaidia CHADEMA, kwa sababu kuna ubabe wa wanaume wachache wabinafsi dhidi ya akina mama. Mbona wao wanaume walipotangazwa 2015 hawakutambua uchaguzi, hawakutambua matokeo ya uraisi lakini walikwenda Bungeni? Kwa nini Leo wawanyase akinamama.
Wanajua kwamba wale wanawake sasa watakuwa na pesa kuliko wao na hivyo hawataweza tena kuwaendesha watakavyo.
 
Watu wanazidi kuharibu utamu wa siasa, siasa imekuwa sawa na ukibaka au mwizi
 
Ndugai hana kosa lolote, na wala hatuna shida nae. Yeye kapewa majina na mamlaka husika I presume kihalali kabisa na akatimiza wajibu wake.

Wenye utata hapo ni Tume na CHADEMA, kuna taasis ama imeingizwa mjini au imeamua kujiingiza mjini. Chadema tumewasikia tayari, bado Tume.

Kuhusu kuwalinda, hiyo sio kazi yake; kama wanakidhi vigezo, wataendelea vinginevyo itabidi watoke tu.
 
Spika Ndugai amesema kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao naye atafanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndugai amesema wabunge 19 wa CHADEMA wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu na kuwafokea kupitia vyombo vya habari.

Spika Ndugai amesisitiza kuwa Mnyika bado hajakomaa kisiasa hivyo amemshauri aende kwa Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru akafundishwe namna Katibu mkuu anavyopaswa kutenda kazi zake kwa ufanisi.

Chanzo: TBC Aridhio

Maendeleo hayana vyama!

NOTE: Ilishadokezwa tangu juzi kuwa Ndugai ana mkakati huo > Ofisi ya Spika ‘kuwalinda’ wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA - Imevuja!
Wale wabunge 8 wa cuf waliofukuzwa na lipumba je?
 
Back
Top Bottom