Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

Kma umemuelewa alishindwa kusema moja kwa moja kwamba kwanini hawakuanza na Zuchu mwenyewe halafu wakafata walimu halafu na wwngine wakafata kuonea upande mmoja haifai wanatakiwa wawarudishe waalimu halafu zuchu ale Ban ya kwenda halafu ndo ziendelee mishe zingine
Zuchu hakuimbia wanafunzi. Ni jukumu la wazazi na walezi kuhakikisha hizi nyimbo haziwafikii wala kusikilizwa na watoto.
 
Mwenyewe nimeshangaa alafu nyimbo inapigwa daily , waufungie mziki ndo tutawaelewa, sio kuwaadhibisha watu kwa chuki binafsi wakati ngoma inapigwa daily na watoto wakiimba na kusikiliza kwenye televisheni na maredioni.

Waalimu warudishwe kazini.
Kwahiyo unachotetea wewe hapo ni kipi na huko kushangaa kwako mkuu? [emoji848]
 
Wanawalea kwa nidhamu ili waje kuwaongoza watoto wanaokata viuno shuleni kwenye vumbi. Watoto wa darasa la nne tayari akili ipo kingonongono, Waziri akisimama kulinda maadili wanamuita mjinga.
Yes anaonekana mjinga kwa sababu sheria na taratibu zipo za kufuata.

Yeye hayupo juu ya sheria. Kila kanuni na sheria vimeweka utaratibu wa kufikia maamuzi.

Waziri ni zao la wasomi ambao wanaamini ktk mtazamo wao pekee
 
Siyo kila nyimbo inapigwa kila mahali, watoto wanapaswa kufundishwa maadili mema, Maudhui ya ile nyimbo yanafaa watu walioko kwenye ma-bar na magenge mengine ya wahuni
Alichoongea ni sahihi. Wakati wa mikutano yao ya siasa na ziara za serikali, miziki hio hupigwa na watoto wakiwepo na hakuna anayekemea.

Kwanini leo washtuke?

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Siyo kila nyimbo inapigwa kila mahali, watoto wanapaswa kufundishwa maadili mema, Maudhui ya ile nyimbo yanafaa watu walioko kwenye ma-bar na magenge mengine ya wahuni
Basi serikali ndio ina wajibu wa kusimamia maadili ya muziki..mziki unapigwa redioni, kwenye tv, kwenye maduka, kwenye mabar..

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Amesema hayo akihoji kuhus Njia iliyotumika Kuwasimamisha walimu hao,Bila ya kufuata utaratibu wa kinidhamu wa kiutumishi,Hata hivyo ameongeza na kusema kuwa lisionewe kundi fulani tu kwani hata baadhi ya wabunge pia nao wanacheza miziki hiyo..

"Wapo mawaziri humu ndani na sisi wabunge huwa tunacheza mziki na hao wanafunzi, Tufafanuliwe hapa ili watu wajue nini cha kufanya la sivyo tutaendelea kucheza huo mziki na watoto wakiwepo shuleni alafu tutawapomza wale ambao watatakiwa kuchukuliwa hatua ,kwahiyo ni muhimu muwe na hatua zaidi ya hapa ili watu wote wawe na uelewa ni miziki gani inachezwa na ipi haichezwi itasaidia sana,Lakini tusiingize Huko hisia za kidini tusichanganye Imani ya dini na maadili ya mtanzania tusivichanganye" amesema Dkt tulia Ackson spika wa bunge la Muungano leo bungeni

hata hivyo aliendelea kumhoji waziri Njia iliyotumika kuwasimamisha walimu wao kazi na akasema kuwa njia hiyo haikuwa na usawa hivyo ameomba warudishwe makazini na njia sahihi zifuatwe

View attachment 2806039

View attachment 2805928
Wapigiwa kura wakiwaadaha wapiga kura.
Alete ushahidi wa videos watoto wao wakicheza huo muziki siku ya masomo akiwa ndani ya sare za shule wanakosoma.
 
Kwa
Amesema hayo akihoji kuhus Njia iliyotumika Kuwasimamisha walimu hao,Bila ya kufuata utaratibu wa kinidhamu wa kiutumishi,Hata hivyo ameongeza na kusema kuwa lisionewe kundi fulani tu kwani hata baadhi ya wabunge pia nao wanacheza miziki hiyo..

"Wapo mawaziri humu ndani na sisi wabunge huwa tunacheza mziki na hao wanafunzi, Tufafanuliwe hapa ili watu wajue nini cha kufanya la sivyo tutaendelea kucheza huo mziki na watoto wakiwepo shuleni alafu tutawapomza wale ambao watatakiwa kuchukuliwa hatua ,kwahiyo ni muhimu muwe na hatua zaidi ya hapa ili watu wote wawe na uelewa ni miziki gani inachezwa na ipi haichezwi itasaidia sana,Lakini tusiingize Huko hisia za kidini tusichanganye Imani ya dini na maadili ya mtanzania tusivichanganye" amesema Dkt tulia Ackson spika wa bunge la Muungano leo bungeni

hata hivyo aliendelea kumhoji waziri Njia iliyotumika kuwasimamisha walimu wao kazi na akasema kuwa njia hiyo haikuwa na usawa hivyo ameomba warudishwe makazini na njia sahihi zifuatwe

View attachment 2806039

View attachment 2805928
Kwani walisimamishwa ama walivuliwa madaraka?
 
Siyo kila nyimbo inapigwa kila mahali, watoto wanapaswa kufundishwa maadili mema, Maudhui ya ile nyimbo yanafaa watu walioko kwenye ma-bar na magenge mengine ya wahuni
Labda kwakuwa wao wanapiga na kuruka sarakasi Bungeni mkuu. Wapiga kura wanaandaliwa kwa nguvu kubwa sana yaani.
 
Hawa walimu ingekuwa mimi ningewafukuza kabisa kazi. Ningekuwa tayari kupoteza uwaziri kwa sababu yao
Wana makosa gan walimu? Kama wimbo hauna maadili waufungie, maana unaweza kataza watoto wasiucheze shulen, wakaucheza mitaan ama nyumban, hapo unakuwa umesaidia nnn?
 
Siyo kila nyimbo inapigwa kila mahali, watoto wanapaswa kufundishwa maadili mema, Maudhui ya ile nyimbo yanafaa watu walioko kwenye ma-bar na magenge mengine ya wahuni
akiwa inapigwa radion wanao sikiliza wakinanani? unaweza kuniambia mwimbaji alikua ana maanisha nini?
 
Nakumbuka kuwahi kuwasikia wabunge wanawake wakati walipokuwa Rwanda kwenye michezo Fulani wakishangilia na kuomba wimbo wa Diamond uliopigwa marufuku wa nyege nyegezi.

Hawa wanasiasa nao ni tatizo kubwa. Maana kweli nyimbo zisizo na maneno mazuri huimbwa katika mikutano Yao ,haswa ya CCM.

Hawa walimu walionewa, na walipaswa tu kuelekezwa
 
Yes anaonekana mjinga kwa sababu sheria na taratibu zipo za kufuata.

Yeye hayupo juu ya sheria. Kila kanuni na sheria vimeweka utaratibu wa kufikia maamuzi.

Waziri ni zao la wasomi ambao wanaamini ktk mtazamo wao pekee
Mamlaka ya nidhamu ya walimu wa kuu wa shule ni Waziri?
 
Hawa walimu ingekuwa mimi ningewafukuza kabisa kazi. Ningekuwa tayari kupoteza uwaziri kwa sababu yao
Waziri hana mandate ya kumfukuza mtumishi wa umma.
Ajaribu aone kama hajamlipa fidia na kumrudisha kazini. Usitumie mihemko. Mtumishi akikosea Kuna utaratibu wa namna ya kumshughulikia na siyo anakuja mtu mmoja tu anamfukuza kazi.
 
Huwezi kumsimamisha mtu bila kumsikiliza. Viongozi hawajui taratibu za utumishi
 
Amesema hayo akihoji kuhus Njia iliyotumika Kuwasimamisha walimu hao,Bila ya kufuata utaratibu wa kinidhamu wa kiutumishi,Hata hivyo ameongeza na kusema kuwa lisionewe kundi fulani tu kwani hata baadhi ya wabunge pia nao wanacheza miziki hiyo..

"Wapo mawaziri humu ndani na sisi wabunge huwa tunacheza mziki na hao wanafunzi, Tufafanuliwe hapa ili watu wajue nini cha kufanya la sivyo tutaendelea kucheza huo mziki na watoto wakiwepo shuleni alafu tutawapomza wale ambao watatakiwa kuchukuliwa hatua ,kwahiyo ni muhimu muwe na hatua zaidi ya hapa ili watu wote wawe na uelewa ni miziki gani inachezwa na ipi haichezwi itasaidia sana,Lakini tusiingize Huko hisia za kidini tusichanganye Imani ya dini na maadili ya mtanzania tusivichanganye" amesema Dkt tulia Ackson spika wa bunge la Muungano leo bungeni

hata hivyo aliendelea kumhoji waziri Njia iliyotumika kuwasimamisha walimu wao kazi na akasema kuwa njia hiyo haikuwa na usawa hivyo ameomba warudishwe makazini na njia sahihi zifuatwe

View attachment 2806039

View attachment 2805928
Tatizo ni uislamu kuingizwa mashuleni serikalini kuliko anzia kwenye hijabu
 
Back
Top Bottom